2015 anatakiwa Rais mwenye haya... | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

2015 anatakiwa Rais mwenye haya...

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by mharakati, Jul 26, 2012.

 1. m

  mharakati JF-Expert Member

  #1
  Jul 26, 2012
  Joined: Sep 29, 2011
  Messages: 1,275
  Likes Received: 51
  Trophy Points: 145
  Sina haja ya kuaeleza umuhimu wa uchaguzi wa 2015 kwani changanoto na udhaifu uliopo ni dhahiri kabisa. Bila ya kujali vyama vya siasa hii post inajitahidi kumfanya Rais kama taasisi yenye nguvu kubwa na ambaye ushawishi wake ukitumika ipasavyo kwa malengo ya taifa basi taifa litakua kwenye njia nzuri kuelekea kwenye ustawi sawia bila ya kujali anatoka chama gani ( inaaminika kua vyama vingi vina itikadi na sera makini tatizo ni utekelezaji wa hizo sera kwa ukamilifu na wakati muafaka na hapo ni tatizo la uongozi wa juu-Rais wa JMT kama taasisi yenye nguvu kubwa ya kushawishi ustawi wa taifa letu kiujumla).

  Binafsi baada ya kusoma matatizo mbali mbali ya awamu zote, na jinsi tabia, style ya uongozi na mengineyo na kama taifa tuna changamoto gani nimekuja na vigezo 6 muhimu vya kumpata Rais atayerudisha nchi kwenye mstari ulionyooka

  Hivi ni;

  1.Technocrat (mtu ambaye ataweka priority za kimaendeleo na matendo na siyo kupoteza muda na blah blah za siasa na kuzingatia zaidi wapinzani wa kisiasa na kukubalika zaidi kisiasa kuliko kufanyia kazi taifa )

  2. Msomi mwenye dira iliyotimia na asiye na papara za maamuzi (kwa maana ya discipline na utaalam, usomi ni nidhamu na kuirudisha nchi kwenye mstari kutaitaji nidhamu ya hali ya juu na siyo maamuzi ya ambayo hayajaangaliwa kwa kina na athari zake za muda mrefu)

  3. Mtu mwenye uzoefu wa kazi (ili awe na mapendekezo yake mwenyewe akijumlisha na ya washauri na asije kupanic mambo yakienda asivyotarajia)

  4.msimamo, maamuzi, na kutokua na urafiki kwenye kazi

  5. mvumilivu na msikivu (nchi ina watu wengi na kero ni nyingi sana akiwa siyo mvumilivu atashindwa kuongoza kwa dira yake na kurukia maamuzi ya muda mfupi ya kufurahisha wachache hapa na pale)

  6. Muadilifu, mzalendo anayechukia ufisadi na mafisadi ili aje kusafisha utumishi wa umma, kuondoa kero za kijamii na hasara za kifisadi na kuanza upya kwa kuwazika mafisadi na ufisadi wao.

  Kwa kifupi tunataka mtu mwenye mazuri yote ya Mkapa (mzoefu na technocrat huku siasa kidogo) na awe msomi, muadilifu, mzalendo na jasiri wa maamuzi kama Nyerere huku akiwa mvumilivu na msikivu kama Mzee Mwinyi. Hapo Tanzania tutapiga Hatua

  Checklist wote wanaohisiwa kugombea CDM na CCM tuone kama tutapata huyu mtu.


  ahsanteni,

  Mharakati


   
Loading...