Kasheshe
JF-Expert Member
- Jun 29, 2007
- 4,694
- 793
Salaam,
Napenda kwa dhati kabisa ya moyo wangu kukupongeza Mheshimiwa Spika Anne Makinda kwa hili moja!!. Uamuzi wako pamoja na wataalamu wako wa kuamua kuwa na Tume ya Kudumu ya Bunge ya Bajeti ni miongoni na Uamuzi mkubwa mzuri ulioufanya na ambao taifa hili litakuwa na faida nalo.
Kwa nini? Kwa mara ya Kwanza Bunge letu linapanga na kusimamia bajeti ki-u-kweli , linaamua wizara gani iongezewe na ipi ipunguziwe lakini pia nini vyanzo vya mapato. Wanaofuatilia Bunge wameona wazi marekebisho mengi yaliyofanywa hivi karibuni wakati wa kujadili bajeti za wizara zilizotangulia.
Kwa weledi hii ni hatua moja kubwa sana kulitoa bunge letu kutoka kuwa mkutano wa matumizi na kuwa mkutano wa mipango na bajeti - Mapato na Matumizi.
Kwa sababu hiyo hapo juu, mimi Kasheshe leo tarehe 29th May, 2013 kama mwananchi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania bila kushawishiwa na mtu yeyote, nakutunuku Nishani ya Juu ya Ubunifu na uthubutu kwa jambo hili.
"Mnyonge Mnyongeni Haki Yake ..."
Wasalaamu