200 Mil biashara gani ya kunilipa fasta

Mpunumpunyenye

Senior Member
Dec 7, 2011
114
50
Nina nyumba ambayo bank wamekubali kunikopesha million 200, je ni biashara gani itakayo nilipa fasta yaani zaidi ya mil 10 kwa mwezi!
 
biashara zipo nyingi inategemea wewe unapenda ipi!1.kununua mchele/nafaka mbalimbali kutoka sehem wanayozalisha sana na kuuza sehem ambazo ni adimu sana!..utapata pesa mingi sana!.....2.kufuga kuku wa nyama zaidi ya elfu 6000 nakuhakikisha utakapoanza kuwatoa baada ya miezi mi 4 ..iwe ndo awamu ya kwanza na hakikisha kila miezi inayofuatia kila mwezi unatoa 4000..kwa wastan utapata mil.20 kila mwezi
 
ulipaswa kupanga kabla hujaenda
now nafikiri uweke ukumbi wa muziki ..kama bendi hivi..
angalau hutakosa milioni kumi kila mwezi
 
Mkuu kwanza tuliza akili. Weka pesa kwa fixed deposit walau kwa mwezi au miwili wakati unafikiria nini cha kufanya., atleast iingize intrest kidogo. Then najua ndani ya muda huo utakuwa umefikiria vya kutosha.

Cha msingi jaribu sana kuminimize risks katika chochote utakachotaka kukifanya, maana pesa ya mkopo kwenye kulipa hakuna risk, maana usije kuwa mmoja wa wale wanaoamini kuwa pesa ya mkopo ina mapepo

All the best Mkuu
 
waweza amua kununua ng'ombe wa maziwa tu kutoka maeneo wanayozalisha ng'ombe wa maziwa 10,kila ng'ombe atoe wastani wa lita 20-15 kwa siku,,,utakuwa tajiri mdogo
 
boss unajua bei ya nyumba inapangwa na location kuliko uzuri wa nyumba??

ni wapi huko utakaponunua kiwanja kwa bei nafuu na kujenga nyumba 3 na kuuza milion 120 kila moja??


Kigamboni..kuna mdau kahtaan alikuwa anauza viwanja humu hebu mcheki
 
ML 200 mmmm !palefu ok Fanya uwekezaji mkubwa Fanya resach biashara inayoingizwa kwa wingi Tanzania na ukachunguze inapotoka nje ya nchi ukachungulie huko wanatengeneza vipi alafu uje utoe ajira
 
Sasa mkuu hapa tunadanganyana asee haiwezekani bank wakupe mil200tsh bila makablasha wala biashara ya vipi utarejesha mkopo.
Otherwise hii ni story ya kupikwa tena imetoka jikoni kijiweni kwenu...
Hakunaga hii kitu ndg make benki hawaangalii tu thamani wala uzuri wa kajumba kako bali ni namna gani umejiandaa na sababu ya kukopa kwako.
Na uwe makini mkuu isijekuwa kuna mtu ndani ya hiyo benki katamani hicho kijumba akupokonye kiaina! Shaulilo....
 
Kama unaviwanja angalau viwili na hiyo hela waweza ilipa kwa mshahara wako, nakushauri ujenge nyumba 2 za 60M each, hizo ni nyumba ni za ukweli sana
Then nunua na gari(coaster) kazi ya coaster itakuwa kurudisha hela na nyumba ndo faida utakayokuwa umeipata
 
Sifa ya kukopa siyo tu kua na nyumba ya thamani kubwa KULIKO unachokopa Bali Ni pia kua na Biashara/shughuli iliyotengeneza mzunguko Kwenye akaunti yako ya Bank walau Mara TATU ya kiasi unachotaka kukopa.
Kama sivyo bank inalazimika kukupa kwanza Mkopo wa 3M na kuendelea kukupandishia kidogokidogo kulingana na ufanisi Kwenye Biashara yako.
 
Back
Top Bottom