20 Mbaroni wakituhumiwa kumpiga mawe Ofisa wa JWTZ aliyemgonga mtembea kwa miguu

Donatila

JF-Expert Member
Oct 23, 2014
7,735
22,433
Polisi mkoani Ruvuma inawashikilia waendesha bodaboda 20 Manispaa ya Songea wanaodaiwa kumshambulia askari wa Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ) Kikosi cha 411 KJ Ruhuwiko, kwa kupiga mawe gari alilokuwa akiendesha baada ya kumgonga mtembea kwa miguu.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ruvuma, Zubeir Mwombeji alisema tukio hilo lilitokea Machi 24 saa 3.00 usiku maeneo ya Shule ya Msingi Mfaranyaki, karibu na Kituo Kikuu cha Polisi Songea Mjini.

Mwombeji alimtaja mwanajeshi huyo aliyejeruhiwa kwa kushambuliwa na waendesha bodaboda kuwa ni Luten Samweli Nginila (32), ambaye amelazwa Hospitali ya Rufani Mkoa.

Alisema Luteni Nginila alijeruhiwa sehemu mbalimbali za mwili na kupoteza fahamu baada ya kushambuliwa na waendesha bodaboda, ambao walivunja kwa mawe vioo vya gari alilokuwa akiendesha.

Aliendelea kuwa chanzo cha tukio hilo, inadaiwa kutokea ajali maeneo ya majengo ambako askari huyo alikuwa akiendesha gari aina ya Nissan XTRAIL akitokea Bar ya Ramour .

Alisema alipofika eneo la majengo, Bahati Mbero alikatisha ghafla barabarani hivyo askari huyo kushindwa kumudu gari na kusababisha ajali.

Kufuatia hali hiyo, waendesha bodaboda waliokuwa karibu walikusanyika kwa lengo la kumshambulia, hali iliyomlazimu kuwasha gari kukimbia ili kuokoa maisha.

Hata hivyo, bodaboda hao walimkimbiza na alipofika Shule ya Msingi Mfaranyaki tairi la gari lake lilichomoka, hivyo walimzingira na kumshushia kipigo wakiwamo abiria watatu aliokuwa nao.

Mwombeji aliwataja waliokuwamo ndani ya gari hilo kuwa ni Kaumbya Kateka (24) mkazi wa Majengo, Joyce Edson (24) mkazi wa Mpambalyoto na Jackline Mwita (22) mwanafunzi wa Chuo cha Uuguzi Peramiho. Alisema katika vurugu hizo baadhi ya vitu vilipotea ambavyo ni mali ya askari huyo.

Vitu vilivyopotea ni simu mbili za mkononi, pochi ambayo ilikuwa imehifadhi vitambulisho mbalimbali na Sh120,00.

Alisema wanaendelea kuwabaini wengine waliohusika, taratibu za kuwafikisha mahakamani zitafuata.
 
Inamaana kwa sasa watu wanachuki kubwa na walinzi wao yaani wanajeshi au iko vipi,
Mtu na akili zake timamu anaandika "Naye wangemuua tu",Shenzi kabisa" hii ni hatari sana
 
Hivi yule alieuwawa kwa kugonga nyanya kesi iliishia wapi vile?

Waandishi wetu wanaandika matukio tu ili wauze magazeti yao tu after that they don't give a toss
 
ukisoma uzi huu na kuangalia comments za baadhi ya wachangiaji utagundua mengi, ikiwa ni amoja na kutokuwaamini jeshi la polisi nchini, chuki, kulipiza kisasi, ni jambo hatari sana
 
Kamata wote weka ndani na ikibidi jeshi liweke nidhamu kidogo pande hizo ili wasirudie tena tumbafu sana
 
Waendesha boda boda hodari wakujichukulia sheria mkononi.Naomba huyo askati apone halafu awapelekee kikosi cha jwtz hao waendesha bodaboda
 
Boda Boda wengi ni Ant Book.....kwa hiyo hata uwezo wao huwa ni mdogo katika kufikiri....siwapendi bodaboda na huwa sipandi bodaboda
 
Aisee uncle Ben sheria maalum kwa ajili ya watu wanaojichukulia sheria mkononi ebu angalia majuzi wale wanajeshi kule kigoma walivyowashushia wale madogo vipigo mmoja akapoteza maisha wale madogo hata miaka 18 hawajafikisha wakuu wamenyuti utafikiri ni poa tu noma sanaaa broo
 
Wanajf wenzangu,hili tukio lilipotikea nilikuwepo na nilishuhudia kwa macho yangu.ukweli ni kuwa huyo mjeda alikuwa kalewa chakari,kosa alilofanya ni kukimbia baada ya kugonga,kiubinadamu alipaswa kumsaidia majeruhi aliemgonga afikishwe hospital.kukimbia ndiko kulisababisha afukuzwe na kupewa kichapo na bodaboda akidhaniwa kuwa ameua.pia aligongwa alikuwa amesimama juu ya calavat nje ya barabara na sio kwamba alikuwa anavuka barabara kama inavoelezwa humu,pia aligongwa bado amelazwa peramiho hospital baada ya kuhamishwa kutoka hasp.ya mkoa wa ruvuma baada ya hali yake kuwa mbaya.mwisho sio bodaboda wote waliokamatwa walihusika kwenye tukio hili,walikamatwa walichuliwa kjiwe jirani na eneo la tukio,lkn kwaida bodaboda wanapomfkuza mtu wengi huunga njiani na hivyo ni vigumu kumjua muhusika halisi
 
Back
Top Bottom