1Mb Unlimited Internet for TsH 20,000 in Kenya, TZ?

Akwaba

Senior Member
Sep 26, 2010
113
22
Ok, now I am officially pissed. Kenya and Tanzania use the same SEACOM cables etc... Kenya now has a service delivering the following.
http://www.zuku.co.ke/fibre/broadband/

1Mb Unlimited Internet for Ksh 1000 or Tsh 20,000

4Mb Unlimited Internet for Ksh 2000 or Tsh 40,000

For comparison TTCL offers the FAKE 1Mbs unlimited which really is 350Kbs for Tsh 110,000

I mean come on, this is nonsense. And then TTCL goes around saying they are bankrupt. Of course, they have no clue how to run a company. They treat internet like a cash cow with a few customers. When they could have a mega-business with many customers.
 
Hapa unaongelea vitu viwili tofauti kwenye 1Mb weka 1Gb,hapo kwenye speed ni 1Mbps na 350kbs,hujasema kama ni kwa mwezi au wiki ?
 
Yaakhe mbona internet Kenya iko ghali kiasi hicho!.
Nakumbuka TTCL Tanzania inatoa mfano 2GB kwa 30,000 tu.Wale wanaoangalia vidio tu ndio wanaozimaliza kwa mwezi.
Nijuavyo 1gb =1000mb.Jee nimepatia?.
 
Yaakhe mbona internet Kenya iko ghali kiasi hicho!.
Nakumbuka TTCL Tanzania inatoa mfano 2GB kwa 30,000 tu.Wale wanaoangalia vidio tu ndio wanaozimaliza kwa mwezi.
Nijuavyo 1gb =1000mb.Jee nimepatia?.

Hapo mkuu unaongelea vitu viwili tofauti. Hii ya Kenya wana claim kwamba
1Mbps, 4Mbps, 8Mbps kwa KSh 1,000, 2,000, 3,500 kwa mwezi ni UNLIMITED.

Kumaanisha, tofauti na hiyo ya 2GB kwa mwezi ambayo ukimaliza 2GB zako basi lazima ungoje hadi mwezi ujao ama ulipe zaidi.
Hii ya Kenya utumie 2GB ama 20GB hamna tofauti, wewe kwa mwezi bill yako ni ileile.

Unacholipia ni kasi ya 1Mbps, 4Mbps au 8Mbps kiasi cha matumizi hakina kikomo, kwa hiyo unaweza kujionea video kila siku, ukadownload mafile kila siku na wala bill yako haibadiliki.
 
Bado sijashawishika, naona bado cost ya mtandao hapa TZ ni ndogo, mfano Vodacom wanakupa 20 MB kwa tsh 500 tu. Need to say more.
 
Hapo mkuu unaongelea vitu viwili tofauti. Hii ya Kenya wana claim kwamba
1Mbps, 4Mbps, 8Mbps kwa KSh 1,000, 2,000, 3,500 kwa mwezi ni UNLIMITED.

Kumaanisha, tofauti na hiyo ya 2GB kwa mwezi ambayo ukimaliza 2GB zako basi lazima ungoje hadi mwezi ujao ama ulipe zaidi.
Hii ya Kenya utumie 2GB ama 20GB hamna tofauti, wewe kwa mwezi bill yako ni ileile.

Unacholipia ni kasi ya 1Mbps, 4Mbps au 8Mbps kiasi cha matumizi hakina kikomo, kwa hiyo unaweza kujionea video kila siku, ukadownload mafile kila siku na wala bill yako haibadiliki.
Sawa!,nimekuelewa.lakini bado naamini hiyo huduma ni kwa ajili ya watumiaji wanyonge wa internet.Ikiwa unalipia kasi inamaana anayelipa I000KSH kwa IMB hatoweza kuitumia internet yake kwa kazi muhimu za download na upload.Mtu wa aina hiyo atakuwa hajafaidika vyema na pesa yake.Ni afadhali aongeze 10,000.tsh apate 2GB.
 
Hujaelewa mkuu hiyo 2GB unayo iongelea ni fixed, yaani ukidownload file ya 2GB siku ya kwanza basi elfu kumi zako zimekwenda, mpaka ulipe tena.
Pili hiyo 2GB hatujui wamekupa kasi kiasi gani, yani unadownload kwa 1Mbps au 350kbs nk.

Kwa hii ya kenya wana kuambia tunakupa kasi ya XMBps mwezi mzima kwa gharama hii, kwa hiyo hata ukidownload file ya 2GB siku ya kwanza, siku ya pili bado service ipo na unaweza kudownload hata 10GB siku ya pili au kila siku mwezi mzima na wala huongezi malipo.
 
Good point, I forgot to say all the numbers were the price per month. To drive the point home.

If you use 1Mbs for 2 hours a day for a month that is 7.5GB. Get the picture!
 
Akwaba,

Sehemu ya jibu la swali lako ni kwamba Kenya ina watumiaji wengi zaidi wa internet kuliko Tanzania. Economics of scale. Ukiwa na wateja wachache lazima wakulipe zaidi per person kuliko ukiwa na wateja wengi. Kuweko na watumiaji wengi zaidi Kenya kunatokana na kupanuka kwa Elimu yao. Asilimia 26 ya watoto wote wa Kenya husoma hadi sekondari. Kwa Tanzania, ni asilimia 6 tu.

Vile vile, bei za umeme (na kupashwa kununua genereta), kodi mbalimbali, ni kubwa zaidi Tanzania. Lazima ISP abebeshe wateja wake gharama hizo.

Mwisho, nisema kwamba upungufu wa Elimu Tanzania unaonekana hata kwenye mjadala huu. Pamoja na kumwelewesha Ami, inaonekana hajaelewa tofauti kati ya kulipia huduma ya 1Mbps na kuitumia utakavyo, na kulipia uwezo wa kudowload hadi 2GB kwa mwezi.
 
Duuh... pole sana kwa wanaofanya kazi kwenye helpline za wateja wa internet hapa Bongo!!! Ama kweli kazi mnayo...:phone:
 
Akwaba,

Kuweko na watumiaji wengi zaidi Kenya kunatokana na kupanuka kwa Elimu yao. Asilimia 26 ya watoto wote wa Kenya husoma hadi sekondari. Kwa Tanzania, ni asilimia 6 tu.

Unao ushahidi wowote kuhusu hii one-on-one causal relationship kati ya kiwango cha elimu ya sekondari na utumiaji wa Internet, au unadadisi tu?

Mwisho, nisema kwamba upungufu wa Elimu Tanzania unaonekana hata kwenye mjadala huu. Pamoja na kumwelewesha Ami, inaonekana hajaelewa tofauti kati ya kulipia huduma ya 1Mbps na kuitumia utakavyo, na kulipia uwezo wa kudowload hadi 2GB kwa mwezi.

Kauli ya mtu mmoja iwe mfano wa "upungufu wa Elimu Tanzania"? Kweli? Umewezaje kufahamu kiwango cha elimu cha huyo mtu mmoja kutokana na matamshi machache kama hayo?
 
OneManArmyMan

Habari kuhusu "Upungufu wa Elimu Tanzania" unaweza kuziona zaidi hapa:

The East African:  - News |Tanzania seeks science and maths teachers from EA to bridge shortfall

Nukuu kutoka kwenye hayo makala ni kama ifuatavyo: :

According to the Ministry of Education and Vocational Training statistics, Tanzania secondary school gross enrolment rates stand at five per cent while Kenya stands at 26 per cent, Uganda 12 per cent, Zambia 28 per cent and Zimbabwe 44 per cent.

Kuhusu uwiano kati ya kiwango cha Elimu na Matumizi ya internet, ziko tafiti nyingi zimefanyika. Unaweza kuziona kwenye internet. Mojawapo ya tafiti hizo ni hii hapa:

Hispanics lag behind in internet usage, study says - CNN

Nanukuu kutoka huo utafiti:

Hispanics in the United States are less likely than whites to access the internet, have a home broadband connection or own a cell phone, according to a study by the Pew Hispanic Center released Wednesday.
The study found that differences in educational level and income are likely behind the digital gap, as the divide in most cases disappears when adjusted for those two factors.

While about two-thirds of Hispanic and African-American adults went online in 2010, more than three-fourths of white adults did so, the study found. As for broadband use at home, the gap between Hispanics and whites is significant, the study says.
"The difference in internet use between Hispanics and whites is driven in part by the fact that Hispanics tend to have less education and lower incomes than whites," study author Gretchen Livingston wrote. "When education or income are controlled for, the ethnic differences in internet use disappear."
 
OneManArmyMan

Habari kuhusu "Upungufu wa Elimu Tanzania" unaweza kuziona zaidi hapa:

The East African: *- News*|Tanzania seeks science and maths teachers from EA to bridge shortfall

Nukuu kutoka kwenye hayo makala ni kama ifuatavyo: :

According to the Ministry of Education and Vocational Training statistics, Tanzania secondary school gross enrolment rates stand at five per cent while Kenya stands at 26 per cent, Uganda 12 per cent, Zambia 28 per cent and Zimbabwe 44 per cent.

Kuhusu uwiano kati ya kiwango cha Elimu na Matumizi ya internet, ziko tafiti nyingi zimefanyika. Unaweza kuziona kwenye internet. Mojawapo ya tafiti hizo ni hii hapa:

Hispanics lag behind in internet usage, study says - CNN

Nanukuu kutoka huo utafiti:

Hispanics in the United States are less likely than whites to access the internet, have a home broadband connection or own a cell phone, according to a study by the Pew Hispanic Center released Wednesday.
The study found that differences in educational level and income are likely behind the digital gap, as the divide in most cases disappears when adjusted for those two factors.

While about two-thirds of Hispanic and African-American adults went online in 2010, more than three-fourths of white adults did so, the study found. As for broadband use at home, the gap between Hispanics and whites is significant, the study says.
"The difference in internet use between Hispanics and whites is driven in part by the fact that Hispanics tend to have less education and lower incomes than whites," study author Gretchen Livingston wrote. "When education or income are controlled for, the ethnic differences in internet use disappear."

Hiyo study siyo relevant kwa mazingira ya Tanzania kwa sababu zilizo wazi, mojawapo kubwa kwamba huwezi kulinganisha kiwango cha upatikanaji wa teknolojia ya broadband kati ya matabaka mbalimbali kwenye jamii ya Marekani na iliyopo Kenya au Tanzania. Teknolojia ya broadband ni nadra kwenye jamii ya Tanzania ukilinganisha na Marekani, achilia mbali upatikanaji wake. Pili, hiyo study ime-focus kwenye matabaka ya kikabila (ethnic groups) kwenye jamii moja (assumption kubwa hapa ni kwamba matabaka yote kwenye jamii moja ya Marekani wana equal access ya teknolojia ya broadband), ambayo ni tofauti sana ukitilia maanani hali halisi iliyopo kwenye jamii ya Tanzania na matabaka yaliyomo ndani yake, achilia mbali kujaribu kulinganisha na nchi nyingine yenye mfumo na matabaka tofauti kama Kenya. Kwa hiyo huo mfano wako ni batili.
 
Mtoa mada amewachanganya watu kwa kutoweka units sahihi, 1Mbps na 4Mbps ambayo ni unit ya spidi na sio unit ya kiwango kama Mb.

Nakubaliana na Moshi tatizo ni idadi ya wateja ndogo sana TZ, TZ kuna internet users just under 700,000 wakati Kenya ni zaidi ya mara nne at 4 million. Plus wanajenga infrastructure nzuri ndani ya nchi pia sio connection ya seacom peke yake.

Nadhani TTCL wanabeba lawama ambazo sio zao wakati wengine, serikali inabidi ihakikishe umeme unapatikana, fiber inajengwa ndani ya nchi, elimu bora etc.

Na sidhani kama linahitaji ubishi kuwa elimu ndogo inatusha kwenye sector nyingi ikiwemo hii.
 
Ona sasa OneManArmyMan,

Idadi ya watumiaji wa internet Kenya ni 5.7 times ya idadi ya watumiaji Tanzania (4million divide by 700,00) na asilimia ya watoto wa Kenya wanaosoma hadi sekondari ni 5.2 times ya wale wa Tanzania (26% divide by 5%). Huo ushabikiano kati ya Elimu na utumiaji wa internet ni mkubwa mno!
 
Back
Top Bottom