16 bora Kombe la Shirikisho: Azam v Mtibwa, Simba v A. lyon, Yanga vs..

PROSPER 05

JF-Expert Member
Oct 14, 2013
226
217
BAADA ya kupenya kwenye raundi ya 16 ya michuano ya Kombe la Shirikisho (Azam Sports Federation Cup), Klabu Bingwa ya Afrika Mashariki na Kati,Ngao ya Jamii na Mapinduzi Azam FC, imepangiwa kucheza na Mtibwa Sugar katika kuwania robo fainali ya michuano hiyo.

Mechi nyingine za ASFC;

Februari 24, 2017

Kagera Sugar v Stand United (Kaitaba Stadium, Bukoba)

Mighty Elephant v Ndanda (Majimaji Stadium, Songea)

Madini v JKT Ruvu (Sheikh Amri Abeid Stadium, Arusha)

Februari 26, 2017

Mbao FC v Toto Africans (CCM Kirumba, Mwanza)

Tanzania Prisons v Mbeya City (Sokoine Stadium, Mbeya)

Simba v African Lyon (National Stadium, Dar es Salaam)

Yanga v Kiluvya (National Stadium, Dar es Salaam)

Itakumbukwa kuwa bingwa wa michuano hiyo ndio atakayeiwakilisha Tanzania Bara kwenye Kombe la Shirikisho Afrika mwakani (2018), mashindano ambayo Azam FC atashiriki mwaka huu ikitarajia kumenyana na mshindi wa jumla wa mechi ya raundi ya awali kati ya Orapa United ya Botswana na Mbabane Swallows ya Swaziland.

Komaa Timu langu AZAM Kwani Hii ni Nafasi Muhimu Kuwakilisha Kimataifa kwani Ligi Kuu ni kama Tumepoteana....
 
Soka la bongo ni pasua kichwa sana!!hivi hizo draw za kupanga hayo makundi huwa zinafanyika wapi!utakuta ni mtu mmoja tu anajifungia mahali anachanga karata zake kwa ustandi kabisa ili mwisho wa picha yanga akutana na either Simba au azam ujinga mtupu.
Wakati watu wanatia juhudi kubadilisha taswira ya soka letu,tff wao wako karume wanafaya madudu tu.
 
Hakuna Draw hapo what a coincidence timu za Sehemu moja Kukutana!!!!!! mbao vs Toto (kirumba), Prison vs Mbeya city.. Jamaa wanapanga kwa vigezo wanavyovijua wao wenyewe
 
Mechi zimepangwa kwa kuibeba yanga.Eti kiluvya! Hapo yanga anatafutiwa nafasi ili apite kirahisi.Mechi hazijapangwa kwa kuzingatia uzito.Hiyo mechi itakuwa bonanza tena la fiesta.
 
Back
Top Bottom