116 wazaliwa krissmass | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

116 wazaliwa krissmass

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by kilimasera, Dec 27, 2010.

 1. kilimasera

  kilimasera JF-Expert Member

  #1
  Dec 27, 2010
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 3,073
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  WATOTO wapatao 116 wamezaliwa katika mkesha wa Sikukuu ya Krismasi, katika hospitali kuu za wilaya za jijini Dar es Salam wakiwemo wawili waliozaliwa nyumbani baada ya wazazi hao kucheleweshwa kufikishwa hospitalini
  Kati ya hao wavulana ni 59 na wsichanda ni 57 waliozaliwa katika hospitali za Temeke, Amana, Muhimbili na Mwananyamala.
  Katika Hospitali ya Temeke jumla ya watoto 64 walizaliwa na 34 ni wavulana na wasichana ni 30.

  Katika Hospitali ya Amana walizaliwa watoto 20 ambapo wasichana ni 12 na wavulana ni 8 kati ya hao walipatikana mapacha wanne kwa akina mama wawili.
  Kwa upande wa Mwananyamala walizaliwa watoto 26, ambapo wasichana ni 14 na 12 ni wavulana.

  Muhimbili waliozaliwa watoto wanne akika usiku nwa mkesha wa kumamkia sikuuu ya Noel, na kudaiwa wote walikuwa ni wavulana.

  Watoto wawili kati ya hao waliozaliwa walizaliwa majumbani baada ya juhudi za kuwafiskisha hospitali wazazi hao ziligonga mwamba

  Mwanamke mmoja mabaye hakupenda jina lake liandikwe mkazi wa Mburahati Mianzini, alijifungua wakati akienda alipkuwa akienda haja ili ajitayarishe kwenda hospitali kwa ajili ya kujifungua na aliwahiwa na ndugu wa karibu kuokoa kichanga hicho ambacho kingeweza kupoteza maisha kwa kuanguka chini.

  Mwingine alijifungua mtoto akiwa chumbani baada ya kukosa msaada wa kuita usafiri mfikishe hospitalini kwa kujifungua, huyu alikuwa mkazi wa Boko.
   
Loading...