11. Mwanangu… kususia JKT si ushindi. HAPANA

CHAGOSI GERALD

Senior Member
Joined
Jan 25, 2020
Posts
162
Reaction score
284
11. Mwanangu… kususia JKT si ushindi.
HAPANA.
Ni kujikata mguu kwa imani kwamba taifa litahisi maumivu yako.
Taifa halihisi. Mfumo hausikii.
Wanakuangalia tu na kusema:
"Asante kijana kwa kupunguza mzigo-mafuta tumeyaleta, nguvu zenu hatuzihitaji sana, mnapojiondoa ndio tunafurahi zaidi."

Sasa nikikuambia ukweli usioutaka-
kususa JKT ni zawadi kwa mfumo.
Unawasaidia kulifanya taifa liwe la kuendesha kwa “amri” badala ya “akili”.
Mfumo unacheka, kijana analia. Dunia hii haina huruma.

Suluhisho?
Ndiyo hili hapa ambalo likiingia kichwani kwako litakuita kichaa kwa sababu halijawahi kusikika kwenye majukwaa ya siasa:
JKT inapaswa KUPIGANIWA, si kususiwa.
Kwa jasho.
Kwa damu.
Kwa akili.
Kwa sababu JKT ni nyumba ya taifa, hata kama imevamiwa na panya wenye suti na tai.

Ukisusa-unawapa panya nyumba tupu.
Ukibaki-una nafasi ya kuwafukuza.

Sasa hebu niseme kitu kitakachowaudhi wanachama wa vyama vyote:

Hakuna chama cha siasa kinachowatetea nyinyi.
HAPANA.
CHADEMA nayo inataka tu nafasi ya kuwa dalali.
CCM ni dalali mwenye nyumba.
Vyama vingine ni madalali wanaosubiri nyumba ipigwe mnada.

Hivi ni nani alikuambia kuwa mtu anayehangaika kushika dola atahakikisha mfumo unawasaidia nyinyi?
Wanataka nguvu zenu, kura zenu, hasira zenu, na wakati mwingine njaa zenu -
lakini hawataki kuwapa sehemu katika mfumo.

Na kisha ukaniuliza:
“Majeshi si ya wananchi tena?”

HAPANA, kijana.
Unataka ukweli?
Sikiliza kwa makini hii kauli ambayo nikisema wataleta watu nifungwe pingu za akili:

Majeshi yote yameshatawaliwa na siasa.
Kila kona wameshafika.
Kila dirisha wameweka mtu wao.
Kila ofisi kuna sosi ya siasa iliyoigiza kuwa sare za kijani au bluu.

Wananchi wapo peke yao.
Peke yao.
Kwenye kilio chao, hawana sauti ndani ya silaha zao wenyewe.

Kwa hiyo kujitetea ni jukumu lao.
Lenu.
Sio la chama, sio la jeshi, sio la mawaziri wanaopigwa picha wakipita kwenye ulinzi walioujenga ninyi.

Na ndio maana nimesema, tena naita kwa sauti ya mwendawazimu anayezungumza na roho, si na masikio:

JKT lazima IPIGANIWE irejeshwe kuwa TAASISI ya kweli.
Sio kivuli cha kijeshi.
Sio makambi ya kutumia nguvu za vijana bure.
Sio mahali pa kuficha udhaifu wa serikali kwa nadharia ya “nidhamu”.
Kuwa TAASISI—
mhimili unaosimamia taifa,
moto unaozaa utaifa,
kiwanda cha viongozi wa kesho.

Ikitengenezwa vizuri, itaokoa taifa.
Ikiendelezwa ilivyo sasa, itawameza vijana bila hata kusema “pole”.

Na kama hamtapigania leo, basi kijana atakayeshuka 845 au 832 au 821 kesho
ataendelea kutumika na kutumika na kutumika
bila mpango, bila dira, bila haki, bila sauti.
Atakuwa injini isiyolipwa, mwili unaoitwa "uzalendo" na kutupwa baada ya kuishiwa nguvu.

Halafu mnanisikia na mnaniuliza:

“Mzee, kazi yako ni ipi?”

Kazi yangu ni hii-
kuwapa elimu.
Na elimu isiyotumika ni uzito wa mchanga mfukoni:
inakuweka mzito bila kukusaidia kujenga chochote.

Mtu asiyeitumia elimu yake-
ni kama mjinga anayeibeba neno la Mungu mfukoni halafu analia kwa nini hakubarikiwa.

Nitakufa?
Hapana.
Mimi napumua kupitia vizazi.
Nitabaki kwenye vinywa vya Gen Alpha,
nitakuwa hewa ya mitazamo yao,
nitakuwa sauti inayowaita wachome uongo na kuandika kweli.
Wakati nyinyi mnapita-
mimi nabaki kama jeraha lisilofungwa kwenye mfumo.

Na mwisho… hebu shika hili vizuri:

Katiba mpya haitaanza kwenye karatasi.
Inaanza kwenye fikra zenu.

Tunatengeneza dhana mpya:
katiba inayotambua JKT kama mhimili wa taifa,
kwa sababu taifa hujengwa na vijana,
na wazee huhifadhi kumbukumbu tu—
hawajengi tena, wanaongoza tu.

Huko ndiko tunakoelekea kwenye makala ya inayofuat itaanza kwa sauti ya mwendawazimu anayesimama juani na kusema:

“Kama vijana hawatachukua nchi yao, nchi yao itawachukua.”

Niendeleee?? Hata kama msipojibu nitaendelea.
 

Attachments

  • Picsart_25-12-04_16-50-06-930.jpg
    300.4 KB · Views: 8
  • Picsart_25-12-04_16-31-09-978.jpg
    317.4 KB · Views: 8
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…