Huwezi iweka Tanzania kwenye hii top 10 sio kwa kuwa haina vivutio bali hakuna miundombinu ya kuwezesha kukuza sekta ya utalii nchini. Miundombinu mibovu, hakuna usafiri wa uhakika, hakuna shirika la ndege linalofanya safari nchi mbalimbali duniani hivyo watalii hupata shida sana, hakuna hoteli za kutosha zenye ubora na hadhi ya kimstaifa, hakuna kumbi za mikutano zenye ubora wa kimataifa ukiacha AICC na JNICC. Ndiyo maana hakuna idadi kubwa ya watalii wanatembelea Tanzania
Ukiangalia hiyo top 10 hakuna taifa lisilokuwa na uwezo kiuchumi na nguvu za kiushawishi katika diplomasia ya kimataifa. Sasa sijui ulikuwa unataka kukata rufaa ya nini wakati hatuna hata sifa moja ya kuwa kwenye hiyo top 10. Ukiangalia hizo nchi ni vitovu vya sekta ya fedha kimataifa tena zimejitangaza kupita maelezo hakuna mtu asiyejua grand canyon ya USA, great wall of China.. Unashangaza sana ukisema unashangaa kwanini Tanzania haipo ulipaswa kushangaa kwanini Brazil nchi inayoongoza duniani kwakuwa na vivutio vingi kwanini haipo? South Africa, Zimbabwe, Hong Kong, Japan, South Korea etc Hizi zote zimekosa kigezo cha kupokea idadi kubwa za watalii na hivyo kukosa idadi kubwa ya mapato katika sekta ya utalii.
Kuna sababu nyingi kwa nchi kupata wageni wengi kwa mwaka, inawezekan kuwa ni utalii, biashara, uwekezaji, michezo na mengineyo. Kwa Tanzania sisi tunategemea wageni wengi kuja kwa ajili ya utalii. Ukiangalia sekta ya michezo tupo nyuma kwakuwa hakuna uwekezaji katika sekta hiyo, tuna viwanja vichache vya michezo tena ni mpira wa miguu tuu ambacho ni kimoja zaidi ya hapo hakuna. Michezo inaleta wageni wengi kwenye mashindano ya kimataifa kama nchi itakuwa mwenyeji kwa michuano ya kombe la dunia(mpira), Olympic games, IAAF riadha, mashindano ya magari, pikipiki, Tennis, Golf tournament, nk..... haya yote ndiyo yanayoyafanya mataifa yao kupata wageni wengi. Sisi mashindano makubwa kuwahi kuwa wenyeji labda michuano ya mpira wa miguu ya Kagame Cup.
Sasa utaona jini gani tulivyo nyuma, kupata wageni wengi si lelemama kuna hitaji kuwekeza vyakutosha katika uboreshaji wa miundombinu, kuwekeza zaidi katika kukuza sekta ya utalii na utunzaji wa mazingira na wanyamapori (tukemee ujangiri na kupitishwe sheria kali na kusimamia dhidi ya vitendo vya ujangiri na kukutwa na nyara za serikali), Tuboreshe sekta ya usafirishaji na tehama, tuwekeze zaidi kwenye sekta ya michezo yote na siyo mpira tuu.