Zawadi Ngoda
JF-Expert Member
- Aug 13, 2009
- 3,382
- 1,446
Ukifuatitia takwimu za makadirio nilizozifanya za wagombea wa URAIS wiki mbili kabla ya uchaguzi, utagundua kwamba Mh Kikwete nilimpa 62%. Ukizingatia matokeo halisi ya kura yaliyotangazwa leo na NEC, Rais huyo amepata 61.17%. Hii ni tofauti ya 0.83% toka katika kura halisi.
Hata mashirika mnayoyaamini kama CIA, Ujerumani na BBC namba zao zilikuwa mbali sana na zile za kwangu. Hii inamaanisha kwamba Tanzania inafahamika zaidi na watanzania wenyewe kuliko hao watu wa nje ambao ni sauti kubwa na sahihi kwa watanzania wengi hususan wapinzani.
Wakati umefika wa kuamini wataalam wetu wanaoishi nasi kila siku na kuwaelewa watu wa matabaka yote, ridhaa na mapendekezo yao. Ni vipi CIA wanaokuja miezi miwili na hata pengine wiki tatu kabla ya uchaguzi kuwaelewa wapiga kura zaidi ya 8 milioni kwa kipindi kifupi?
Nina hakika kabisa kuwa wanaJF watanipongeza kwa kutoa makadirio sahihi kabisa, kwani kosa la 0.83% linakubalika kabisa. Ni sifa kwa mwana JF kuibuka mshindi wa makadirio au sio.
Mimi naamini katika takwimu, na ninatarajia watanzania wa kizazi kijacho wajifunze kuzungumza kwa tarakimu. Hayo yatakuwa maendeleo makubwa.
N.B. Sijaisikia kauli ya Mh Slaa baada ya kutangazwa matokeo.