Elections 2010 0.83 asilimia ndio nilizokosea katika makdirio yangu.

Zawadi Ngoda

JF-Expert Member
Aug 13, 2009
3,768
1,817
Ukifuatitia takwimu za makadirio nilizozifanya za wagombea wa URAIS wiki mbili kabla ya uchaguzi, utagundua kwamba Mh Kikwete nilimpa 62%. Ukizingatia matokeo halisi ya kura yaliyotangazwa leo na NEC, Rais huyo amepata 61.17%. Hii ni tofauti ya 0.83% toka katika kura halisi.

Hata mashirika mnayoyaamini kama CIA, Ujerumani na BBC namba zao zilikuwa mbali sana na zile za kwangu. Hii inamaanisha kwamba Tanzania inafahamika zaidi na watanzania wenyewe kuliko hao watu wa nje ambao ni sauti kubwa na sahihi kwa watanzania wengi hususan wapinzani.

Wakati umefika wa kuamini wataalam wetu wanaoishi nasi kila siku na kuwaelewa watu wa matabaka yote, ridhaa na mapendekezo yao. Ni vipi CIA wanaokuja miezi miwili na hata pengine wiki tatu kabla ya uchaguzi kuwaelewa wapiga kura zaidi ya 8 milioni kwa kipindi kifupi?

Nina hakika kabisa kuwa wanaJF watanipongeza kwa kutoa makadirio sahihi kabisa, kwani kosa la 0.83% linakubalika kabisa.
Ni sifa kwa mwana JF kuibuka mshindi wa makadirio au sio.

Mimi naamini katika takwimu, na ninatarajia watanzania wa kizazi kijacho wajifunze kuzungumza kwa tarakimu. Hayo yatakuwa maendeleo makubwa.

N.B. Sijaisikia kauli ya Mh Slaa baada ya kutangazwa matokeo.
 
Kwanza kwa nini unataka kupongezwa kwa error? Unajua 0.83% ni wapiga kura wangapi? Unajua difference ya 0.83% inaweza kumpa au kumyima mtu ubunge.

Pili kwa kuwa unataka pongezi hebu tupe darasa. ulitumia vigezo, input na factors gani za kitwakwimu kupata hiyo 62% ya rais mteule? I mean ulitumia mbinu kama za sheik yahya au kuna mathematical logic ?
 
QUOTE=Zawadi Ngoda;1229711]
Nina hakika kabisa kuwa wanaJF watanipongeza kwa kutoa makadirio sahihi kabisa, kwani kosa la 0.83% linakubalika kabisa. [/B]Ni sifa kwa mwana JF kuibuka mshindi wa makadirio au sio.

N.B. Sijaisikia kauli ya Mh Slaa baada ya kutangazwa matokeo.[/QUOTE]

Tukupongeze kwa lipi wakati matokeo mlikua nayo tayari? By the way huo ni ushindi wa kushindwa, manake kama unajua mahesabu vizuri Kikwete alipata kura zaidi ya 80% Mwaka 2005 this time amepata 61.17% Je huo utaita ushindi pia?

Tafsiri yake iko wazi kwamba umaarufu wake na uongozi wake watu hawaufurahii. Pia ukilinganisha nguvu walioitumia wakati wa uchaguzi, kupata kura 5 Milion ni kushindwa haswa ukizingatia CCM walisimamisha mgombea ubunge katika kila jimbo la nchi hii...! Gharama za Tshirt, Gharama za mabango, gharama za kuchakachua, na bado ripoti ya wasimamizi wa uchaguzi iko wazi kwa kusema CCM ilibebwa na Wakuu wa MIkoa na Wakuu wa Wilaya...! Kikubwa ambacho bado Kikwete amekikosa na ambacho kinamfanya aonekane ameshindwa ni kukosa imani ya wananchi haswa jamii ya wananchi wenye uelewa na upeo wa mambo (wasomi) ambao wanashindwa kukubaliana na itikadi za uongozi wa Kikwete...! :yield:
 
Kwanza kwa nini unataka kupongezwa kwa error? Unajua 0.83% ni wapiga kura wangapi? Unajua difference ya 0.83% inaweza kumpa au kumyima mtu ubunge.

Pili kwa kuwa unataka pongezi hebu tupe darasa. ulitumia vigezo, input na factors gani za kitwakwimu kupata hiyo 62% ya rais mteule? I mean ulitumia mbinu kama za sheik yahya au kuna mathematical logic ?
Vigezo tulivyotumia (mimi na timu yangu ya wasomi) nilivitaja kwa urefu katika Thread ile. Hata hivyo kwa ufupi tu ni kwamba tulitembelea mikoa 16 na kutoa karatasi za siri (anonymous) AMBAZO WATU WA MATABAKA na umri TOFAUTI, walijaza uchaguzi wao wa rais kama uchaguzi ungekuwa siku ile. Na majumuisho ya kura za mikoa 16 tukapata 62% kwa Kikwete.

Na hivyo ndivyo ilivyokuwa. Inawezekana kuwa 0.83% ni kubwa kama usemavyo, lakini nikilinganisha na mashirika mengine bado timu yetu inaibuka kidedea. Au unasemaje?
 
QUOTE=Zawadi Ngoda;1229711]
Nina hakika kabisa kuwa wanaJF watanipongeza kwa kutoa makadirio sahihi kabisa, kwani kosa la 0.83% linakubalika kabisa. [/B]Ni sifa kwa mwana JF kuibuka mshindi wa makadirio au sio.

Mimi naamini katika takwimu, na ninatarajia watanzania wa kizazi kijacho wajifunze kuzungumza kwa tarakimu. Hayo yatakuwa maendeleo makubwa.

N.B. Sijaisikia kauli ya Mh Slaa baada ya kutangazwa matokeo.

Tukupongeze kwa lipi wakati matokeo mlikua nayo tayari? By the way huo ni ushindi wa kushindwa, manake kama unajua mahesabu vizuri Kikwete alipata kura zaidi ya 80% Mwaka 2005 this time amepata 61.17% Je huo utaita ushindi pia?

Tafsiri yake iko wazi kwamba umaarufu wake na uongozi wake watu hawaufurahii. Pia ukilinganisha nguvu walioitumia wakati wa uchaguzi, kupata kura 5 Milion ni kushindwa haswa ukizingatia CCM walisimamisha mgombea ubunge katika kila jimbo la nchi hii...! Gharama za Tshirt, Gharama za mabango, gharama za kuchakachua, na bado ripoti ya wasimamizi wa uchaguzi iko wazi kwa kusema CCM ilibebwa na Wakuu wa MIkoa na Wakuu wa Wilaya...! Kikubwa ambacho bado Kikwete amekikosa na ambacho kinamfanya aonekane ameshindwa ni kukosa imani ya wananchi haswa jamii ya wananchi wenye uelewa na upeo wa mambo (wasomi) ambao wanashindwa kukubaliana na itikadi za uongozi wa Kikwete...! :yield:
[/QUOTE]

Si kweli maneno yako. Huu ni ushindi mkubwa sana kwa sababu zifuatazo.

Kwanza JK kaleta uhuru wa vyombo vya habari kwa kipindi hiki cha miaka 5. Ni magazeti mangapi yameibuka toka 2005 mpaka 2010. Ni mengi ikiwa pamoja na Tanzania Daima.

Ni mitandao mingapi imeibuka na ile iliyokuwepo imekuwa sana ikiwa ni pamoja na JF ( zingatia idadi ya wanachama na wageni wanaotembelea JF 2005 NA SASA HIVI.

Radio na TV ngapi zimeanzishwa.

Sijakueleza uhuru walioachiwa vijana wa mitaani wa kumsema ovyo Rais, mpaka hata baadhi ya wapinzani wakasema Rais alitakiwa kuwaweka ndani wale wanaoleta dharau kwake.

Hakuliingilia bunge.

Kawashirikisha wpinzani katika shughulu zake za kiserikali, shukuruni kuwa Mkapa hakuendelea na urais.

Aliachana na siasa za kizee za CCM za zamani, kuwa pale penye wabunge wapinzani wasahau huduma.

Kwa maneno mafupi wananchi walipata habari zaidi mwaka huu kuliko 2005
. Hivyo demokrasia imekuwa zaidi mwaka huu kuliko 2005.

Katika nchi ya vyama vingi, pale ambapo Demokrasia imekuwa na vyama vya siasa zaidi ya 4 vikashiriki uchaguzi, ni vigumu kwa Rais au waziri mkuu kuchaguliwa kwa zaidi ya kura 56%. Hivi ndivyo ilivyo.

Kwa sababu hizo kwa JK kupata 61.17 ni ushindi wa kishindo zaidi kuliko ule wa 2005. Huu sio wakati wa Nyerere aliyekuwa anashinda kwa 99%.
 
Vigezo tulivyotumia (mimi na timu yangu ya wasomi) nilivitaja kwa urefu katika Thread ile. Hata hivyo kwa ufupi tu ni kwamba tulitembelea mikoa 16 na kutoa karatasi za siri (anonymous) AMBAZO WATU WA MATABAKA na umri TOFAUTI, walijaza uchaguzi wao wa rais kama uchaguzi ungekuwa siku ile. Na majumuisho ya kura za mikoa 16 tukapata 62% kwa Kikwete.

Na hivyo ndivyo ilivyokuwa. Inawezekana kuwa 0.83% ni kubwa kama usemavyo, lakini nikilinganisha na mashirika mengine bado timu yetu inaibuka kidedea. Au unasemaje?

Nakupongezeni kwa kufanya takwimu zilizokaribiana na ukweli.

Sasa intepratation yenu ya matokeo ya mwaka 2010 tofauti na 2005 specifically kwa kikwete na miaka mingine ya nyuma ni nini.

NB.Nimeona umetaja demokrasia kukua na uhuru wa vyombo vya habari. Please kama wewe ni mwana takwimu uwe honest. Naomba sababu zaidi. from 80% to 62%. kwa nn kukua kwa demokrasia kuendane na CCM kupoteza viti na JK kupungukiwa %ya kura?

Binafsi kwa kutumia sababu zako tafsiri yake ni kuwa.

  • vyombo vya habari vimesaidia kuanika underperformance ya JK
  • 2005 wananchi walifanya gamble.Wananchi hawakuwa na vigezo vya kumpima JK but 2010 ni matokeo halisi baada ya JK kuongoza nchi before.UFISADI una mchango mkubwa wa kupunguza kura.
Nawasilisha.
 
Tunakupongeza kwa kuhitmu ugaidi ila tusaidie kujua kama wewe ndiye Rashid Shamte! Tunatanguliza ahsante na kukuombea mabaya
Ukifuatitia takwimu za makadirio nilizozifanya za wagombea wa URAIS wiki mbili kabla ya uchaguzi, utagundua kwamba Mh Kikwete nilimpa 62%. Ukizingatia matokeo halisi ya kura yaliyotangazwa leo na NEC, Rais huyo amepata 61.17%. Hii ni tofauti ya 0.83% toka katika kura halisi.

Hata mashirika mnayoyaamini kama CIA, Ujerumani na BBC namba zao zilikuwa mbali sana na zile za kwangu. Hii inamaanisha kwamba Tanzania inafahamika zaidi na watanzania wenyewe kuliko hao watu wa nje ambao ni sauti kubwa na sahihi kwa watanzania wengi hususan wapinzani.

Wakati umefika wa kuamini wataalam wetu wanaoishi nasi kila siku na kuwaelewa watu wa matabaka yote, ridhaa na mapendekezo yao. Ni vipi CIA wanaokuja miezi miwili na hata pengine wiki tatu kabla ya uchaguzi kuwaelewa wapiga kura zaidi ya 8 milioni kwa kipindi kifupi?

Nina hakika kabisa kuwa wanaJF watanipongeza kwa kutoa makadirio sahihi kabisa, kwani kosa la 0.83% linakubalika kabisa.
Ni sifa kwa mwana JF kuibuka mshindi wa makadirio au sio.

Mimi naamini katika takwimu, na ninatarajia watanzania wa kizazi kijacho wajifunze kuzungumza kwa tarakimu. Hayo yatakuwa maendeleo makubwa.

N.B. Sijaisikia kauli ya Mh Slaa baada ya kutangazwa matokeo.
 
Nakupongezeni kwa kufanya takwimu zilizokaribiana na ukweli.

Sasa intepratation yenu ya matokeo ya mwaka 2010 tofauti na 2005 specifically kwa kikwete na miaka mingine ya nyuma ni nini.

NB.Nimeona umetaja demokrasia kukua na uhuru wa vyombo vya habari. Please kama wewe ni mwana takwimu uwe honest. Naomba sababu zaidi. from 80% to 62%. kwa nn kukua kwa demokrasia kuendane na CCM kupoteza viti na JK kupungukiwa %ya kura?

Binafsi kwa kutumia sababu zako tafsiri yake ni kuwa.

  • vyombo vya habari vimesaidia kuanika underperformance ya JK
  • 2005 wananchi walifanya gamble.Wananchi hawakuwa na vigezo vya kumpima JK but 2010 ni matokeo halisi baada ya JK kuongoza nchi before.UFISADI una mchango mkubwa wa kupunguza kura.

Nawasilisha.

Nikiwa HONEST, sitarajii chaguzi zijazo kama kuna mgombea wa urais au ubunge, awe wa CCM au chama Pinzani kuwa anaweza kupata zaidi ya 60%.

Pale ambapo zile zote zilizoitwa SIRI ZA SERIKALI zinaweza kusemwa bayana, na baadhi ya vingungu kuuachia uwaziri mkuu na Benki kuu (japo kuwa hawakufikishwa mahakamani), ni hatua kubwa kwa Tanzania. Kumbuka zama za Nyerere walikuwa wanahamishwa toka wizara moja kwenda nyingine, eti hiyo ndio adhabu ya kuhujumu serikali. Zama za MKAPA ndio hakumsikiliza yeyote yule na ukizisema zile ziitwazo siri za Serikali basi unahatari hata ya usalama wako, nafasi ya kusema ilikuwa haipo.

Sasa tumetoka katika ujima huo, na ndio mwanzo wa safari ya kuelekea katika elimu ya URAIA. Elimu ya Uraia itapatikana sana kupitia Vyombo vya habari.
 
kile mnachoita siri za serikali zinazoanikwa mtaani , ni siri mnazoficha ambazo ndani yake zinaonesha Taifa ambavyo linaibiwa, wazalendo wachache waliobaki serikalini hutoa nyaraka hizo ili kuwaonyesha watu namna mambo yalivyo hovyo kayika mfumo wa UTAWALA.
HUWEZI KUKUTA SIRI ZA MASLAHI YA TAIFA mitaani, huwezi kukuta.
na kwakua inaelezwa mkuu anawaonea haya washikaji zake wezi , tofauti na watangulizi wake ndio maana basi , nyaraka hizo anapelekewa mwenye UJASIRI hata wakuwanyoshea kidole hadharani.
 
Nikiwa HONEST, sitarajii chaguzi zijazo kama kuna mgombea wa urais au ubunge, awe wa CCM au chama Pinzani kuwa anaweza kupata zaidi ya 60%.

Pale ambapo zile zote zilizoitwa SIRI ZA SERIKALI zinaweza kusemwa bayana, na baadhi ya vingungu kuuachia uwaziri mkuu na Benki kuu (japo kuwa hawakufikishwa mahakamani), ni hatua kubwa kwa Tanzania. Kumbuka zama za Nyerere walikuwa wanahamishwa toka wizara moja kwenda nyingine, eti hiyo ndio adhabu ya kuhujumu serikali. Zama za MKAPA ndio hakumsikiliza yeyote yule na ukizisema zile ziitwazo siri za Serikali basi unahatari hata ya usalama wako, nafasi ya kusema ilikuwa haipo.

Sasa tumetoka katika ujima huo, na ndio mwanzo wa safari ya kuelekea katika elimu ya URAIA. Elimu ya Uraia itapatikana sana kupitia Vyombo vya habari.

Zawadi sasa wewe unaoenekana ni mwanasiasa -mwanatakiwmu. Correct interptartion ni from 80% to 60% kuna ujumbe kuwa wananchi hawaridhishwa na JK na CCM kwa ujumla walivyoshughulikia UFISADI. Ukifanya analysis ya matokeo ya uchaguzi huu bila kutaja UFISADI unakwepa ukweli.

Nakupa fact. JK ni mwenyekiti wa CCM na JK alikuwa Rais. Serikali ya JK ilikubali baada ya kuwa na ushahidi kwa mtazamo wa serikali ya JK Mramba na Chenge wana hatia. Lets assume Kiutendaji wa serikali JK hawezi kuingilia Taratibu za kisheria.

But katika level ya chama na Kama mwenyekiti wa CCM hawa wanachama aliowashataki kama mafisadi kwa nn aliruhusu wagombee.???!!!! Inashangaza na kustaajabisha Ni kama the comedy

  • Je JK hajui authority na mamlaka ya mwenyekiti wa chama.?au a anaogopa kutekelza baadhi ya maamuzi magumu na sahihi kukidhi watu fulani na si taifa?
  • Kama CCM iliweza kuwandoa Mwakalebela na Bashe kwa tuhuma tu hata kabla ya vyombo husika kuthibitisha kwa nini haikufanya hivyo kwa Chenge na Mramba tena ambao maamuzi yao yalithiri taifa zaidi kuliko hao kina mwakalebela???
Simtetei Mkapa naye alivuruga lakini kuna tofauti kubwa kati ya mkapa na JK. Mkapa alikuwa na msimamo. Alipoaamua kusimamia kitu hata kama hakikuwa sahihi alisimama kidete. Binafsi naona tanzania tunahitaji rais mwenye udikteta fulani hivi .JK hana msimamo. JK anafanya baadhi ya maauzi apambe na kupata publicity.

Kwangu ni kituko cha karne kumpeleka mtu mahakamani alafu kesho unamsimamisha kwenye jukwaa ukimwombea kura?
 
umesema Vyema Mtazamaji,
JK anakosa meno ya kuwatafuna wahalifu hawa, anakosa ujasiri mbele ya RA na EL, anamgwaya yule mzee wa Rombo, hawezi hata kukaripia, anacheka na hawa wadokozi, hicho ndicho Zawadi na wapambe wengine wa JK hawaoni kuwa ni udhaifu mkubwa wa jamaa katika Utawala wa nchi kufuatia kiapo alichofanya leo.
Jiulize Dr Slaa(PHD) ANATOA WAPI DATA ZA WEZI HAWA HADI KUWAANIKA, sasa kama JK na serikali inafanya kazi baada ya Slaa kusema , naamini ni JK ni mmoja kati ya Viongozi legelege barani Afrika, yeye anammudu Mgaya wa TUCTA, anawashindwa hao wezi.
 
Wakati umefika wa kuamini wataalam wetu wanaoishi nasi kila siku na kuwaelewa watu wa matabaka yote, ridhaa na mapendekezo yao. Ni vipi CIA wanaokuja miezi miwili na hata pengine wiki tatu kabla ya uchaguzi kuwaelewa wapiga kura zaidi ya 8 milioni kwa kipindi kifupi?

............................

Asssumme wewe kama mtu wa karibu na rafiki na JK aambaye hakushirikisha kwenye serikali yake iliyopita. anakuuliza Zawadi kama rafiki yangu ebu nishauri nimabie ukweli kuhusu

  • udhaifu wa serikali yangu iliyopita na udhaifu wa utendaji wangu ulikuwa ni upi ili nirekebishe mambo ?

  • Anakuuliza ebu nipe tafsiri sahihi ya hizi takwimu ulizokusanya? tena anakusisitizia usimpake mafuta kwa mgongo wa chupa
Je utamjibu nini na kumshauri nini
 
Ukifuatitia takwimu za makadirio nilizozifanya za wagombea wa URAIS wiki mbili kabla ya uchaguzi, utagundua kwamba Mh Kikwete nilimpa 62%. Ukizingatia matokeo halisi ya kura yaliyotangazwa leo na NEC, Rais huyo amepata 61.17%. Hii ni tofauti ya 0.83% toka katika kura halisi.

Hata mashirika mnayoyaamini kama CIA, Ujerumani na BBC namba zao zilikuwa mbali sana na zile za kwangu. Hii inamaanisha kwamba Tanzania inafahamika zaidi na watanzania wenyewe kuliko hao watu wa nje ambao ni sauti kubwa na sahihi kwa watanzania wengi hususan wapinzani.

Wakati umefika wa kuamini wataalam wetu wanaoishi nasi kila siku na kuwaelewa watu wa matabaka yote, ridhaa na mapendekezo yao. Ni vipi CIA wanaokuja miezi miwili na hata pengine wiki tatu kabla ya uchaguzi kuwaelewa wapiga kura zaidi ya 8 milioni kwa kipindi kifupi?

Nina hakika kabisa kuwa wanaJF watanipongeza kwa kutoa makadirio sahihi kabisa, kwani kosa la 0.83% linakubalika kabisa.
Ni sifa kwa mwana JF kuibuka mshindi wa makadirio au sio.

Mimi naamini katika takwimu, na ninatarajia watanzania wa kizazi kijacho wajifunze kuzungumza kwa tarakimu. Hayo yatakuwa maendeleo makubwa.

N.B. Sijaisikia kauli ya Mh Slaa baada ya kutangazwa matokeo.

Kumbe una hamu ya kumsikia Dr. Slaa? vuta subra kidogo tu, kesho ataongea na waandishi wa habari kwahiyo ukiweza nenda makaommakuu ya chadema pale kinondoni ili ujipatie kauli yake "live" bila chenga.
 
Ukifuatitia takwimu za makadirio nilizozifanya za wagombea wa URAIS wiki mbili kabla ya uchaguzi, utagundua kwamba Mh Kikwete nilimpa 62%

Naona kuna watu wanatafuta kwa nguvu ya ziada zile nafasi za chee kama ubunge wa kuteuliwa, ukuu wa wilaya au uDED kwenye hizi halmashauri mpya

But Mkwere alishaspell his terms and conditions - UKITAKA KULA, LAZIMA AKULE KWANZA!
 
Kumbe una hamu ya kumsikia Dr. Slaa? vuta subra kidogo tu, kesho ataongea na waandishi wa habari kwahiyo ukiweza nenda makaommakuu ya chadema pale kinondoni ili ujipatie kauli yake "live" bila chenga.

UNANIHAKIKISHIA USALAMA WANGU NIKIENDA HUKO? Maana nimepata vitisho toka kwa wanachadema hapa JF.

nIHAKIKISHIE HILO NAMI NITAKWENDA, maana kisaikolojia nikimuangalia tu macho yake nitamuelewa anchofikiria. Hivyo kwangu ni muhimukwenda huko, kwani toka nionane naye na kupeana mikono ni wakati ule akiwa mbunge.
 
Zawadi Ngoda...!

Hivi profession yako haswa ni nini? Manake naona mara unazungumzia Saikolojia, Siasa za CCM, Mtakwimu wa kuchakachua, Usoma nyota kama Sheik Yahya...! Mpaka sasa hujaweza kutupa majibu yalio rasmi kwa maswali yetu hapo juu kwamba uliweza vipi kufikia au kuja kwamba Kikwelte atapata 61% ya kura...!:yield:
 
Asssumme wewe kama mtu wa karibu na rafiki na JK aambaye hakushirikisha kwenye serikali yake iliyopita. anakuuliza Zawadi kama rafiki yangu ebu nishauri nimabie ukweli kuhusu

  • udhaifu wa serikali yangu iliyopita na udhaifu wa utendaji wangu ulikuwa ni upi ili nirekebishe mambo ?

  • Anakuuliza ebu nipe tafsiri sahihi ya hizi takwimu ulizokusanya? tena anakusisitizia usimpake mafuta kwa mgongo wa chupa

Je utamjibu nini na kumshauri nini

Maswali yako ni mzuri sana, kwa ufupi yana majibu kama yafuatayo.

1. Udhaifu wa kwanza kabisa wa Kikwete, ni kwamba yeye ni Rais ANAYEAMINI sana katika demokrasia zaidi ya pale ambapo demokrasia ya Afrika ilipo. Kuna watu wengi wana msema Kikwete kwa kuwafumbua watanzania macho, huku wakisema "ukila na kipofu usimguse mkono"

2. Takwimu hizi nimezikusanya toka mikoa 16 ya TZ Bara. Rejea maelezo ya vigezo nilivyotumia ktk hoja yangu hapo awali #5.

Hayo ndio majibu yangu kwa ufupi. Kuna mtoa hoja kamtamka mkapa, tofauti ya hawa viongozi ni kubwa sana. Ktk uchaguzi huu t MKAPA angeondoka (angezika) na WANACHADEMA WASIOPUNGUA 100. Risasi za moto ndio wangetembea nazo askari.
 
teh teh teh teh Kwa hiyo ungemshauri aiminye demokrasia ili mambo yawe safi?
Kuamini katika demokrasia ni strengths sio weaknes Zawadi .Sishangai na watu waliomzunguka Jk ni kama wewe wenye mawazo kama yako.ndio maana hawamsaidii JK wala Tanzania

Acha ushabiki Jk ni rais sasa lakini anahitaji washauri wenye guts.Hawezi kupata washauri wazuri sababu udhaifu wake mwingine ameendekeza urafiki hata ofisini. hata Udhaifu huu wa kuendekeza urafiki kazini umeshindwa kuuona ?????

Naanza kusita kama kweli wewe ni mwanatakwimu.

Tukirudi nyuma unakumbuka ulivyomsifia JK kwenye hotuba ya kufunga bunge eti hotubaa imejaa takwimu .Kuwa na takwimu ni kitu kimoja na kufanya analysis ta kitu kingine muhimu zaidi.

Mfano ulisifia Kwa Jk kusema bajeti yetu inajitegmea kwa 40%. Wanatakwimu halisi tunajua hiyo ni siasa. Baada ya serikali za norway , etc sweeden kupunguza misaada sababu ya serikali kushindwa kushughulika ufisadi walipunguza misaada ikabidi serikali ikope kugarimia bajeti yake.

Wanatakwimu wanakumbia madeni yote aliyolipa Mkapa ni kama kazi bure sababu JK amekopa kwa kasi ya ajabu.

Ushauri kwako ukiongea takwimu usiwe unaangalia tu figure. Fanya corect unbiased interpratation na analysis ili Takwimu zako ziwe za kisomi. Otherwise andika thread ya kisiasa tu tutakuelewa
 
Unaweza kuwa sahihi kama utaamini wamarekani na wamagharibi juu ya ufunguaji milango ya Demokrasia.

Lakini kama utaamini Warusi (kuna tabaka la masikini) na Wachina (kuna tabaka la masikini) basi DEMOKRASIA LAZIMA IENDE KWA HATUA. Rais Yeltsin alipofungua milango yote ya Demokrasia kwa mara moja kidogo urusi isambaratike na ndio alikuwa kipenzi cha Magharibi na Marekani. Bwana mdogo PUTIN alipokuja alifunga baadhi ya milango ikiwemo pamoja na vyombo vya habari vinavyokiuka maadili. Guzinsky (mmiliki wa media nyingi) akakimbia nchi na Berizovsky naye akaomba ukimbizi Uingereza. Hiyo ilikuwa ni njia mpya iliyopingwa vikali sana na wamagharibi na Marekani.

China toka awali ililifahamu hilo, hivyo toka waanze kufungua milango wamekuwa na tahadhari kubwa sana. Hivyo wao hufungua mlango mmoja mmoja na kwa mwendo wa kinyonge. Kifupi wanaamini katika demokrasia ya kiuchumi, huko wameacha huru lakini si ya vyombo vya habari. Wanaogopa wamagharibi kuchota mawazo ya wachina na kusababisha fujo. Leo China ni ya pili Duniani kiuchumi baada ya marekani!

Kiufupi naamini katika demokrasia yenye misingi ya kitamaduni, muundo, elimu, na mazingira ya kwetu. Hivyo naamini kuwa Rais Kikwete anapashwa kuyashughulikia na kuwa mkali kwa vyombo vyote vya habari vinavyokiuka maadili.

Kuhusu takwimu nitascan washiriki na NGO yetu ikijumuisha washiriki kumi na elimu zao ili utuamini. Hili sitasema sana kwani nafikiri unataka uthibitisho.
 
.............

Zawadi u dont get my point . Unaweza kuwa stastician mzuri sana theoretically. Lakini ukiikingiza siasa kwenye taaluma nyeti ya stastics ndo nashindwa kukukuelewa wewe ni mwanasiasa-mwanatakwimu au mwanatakwimu mwanasiasa????

Kama siasa za chama fulani unazipa kipaumbele kuliko elimu yako ya takwimu then ujue hutendei haki taaluma yako. Lakini kama taaluma yako ya takwimu ndio inakuongoza jinsi ya kuchambua hata habari za siasa then nilitajaria nione analysis na interpration sahihi ambayo inelenga ukweli kueleza sababu ya % za CCM na JK kushuka?

Nchi yetu ina wasomi wengi tu theorecticaly wanajua best pratice na ethics za fani zao but tatizo linakuja wanatumia usomi wao kutafuta mbinu nzuri za kuwadanganya watu.

Nimekupa mfano wa wachumi wa CCM kutuambia sasa bajeti yetu tunajitegemea kwa 40%. Je huu ni ukweli????Na wewe ulifuruahia taarifa hizi nakumbuka.

Sina wasi wasi na wewe kuwa stastician.Wasi wangu kuwa ethics. kila taaluma ina ethics zake.. Unethical conducts kubwa za statisican ni kupika data na nyingine ni kutoa tafsiri zisizo sahihi sababu ya ushabiki wa kisiasa au sera fulani.

Sasa wewe kwa kigezo cha kwanza uko ethical lakini kigezo cha pili u re 100.1% unethical.

Ndio maana nimekwambia unbiased stastician kuanalyse matokeo ya mwaka huu kwa CCM bila kutaja UFISADI ni Unafiki. Ubiased statician kuelezea mafanikio ya CHADEMA na NCCR bila kutaja Weakness za CCM ni uwongo pia.

Nimekuuliza kama mwanatakwimu JK anakuuliza weakness yake kubwa ilikuwa nini term iliyopita. Jibu ulilotoa linachekesha kwa kweli.

So umepatia kuwa na takwimu zinazoendana na ukweli lakini unafanya analysis na interptration potofu. Ni kazi bure. Bora hata mtu angesema JK atapata 70% na akasema asilimia zimeshuka sabababu wanachi hawajaridishwa anavyoshughulika UFISADI.

usiishie kukusanya Data sahihi tu. go a mile futher . Make a correct intrepration and analysis of your stastistics

NB:
Naona unaanza kutoka kwenye mada yako kuhusu takwimu. Tuendelee kujadili takwimu hizi za uchaguzi na tafsiri zake.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom