soko la kariakoo

Soko la Kariakoo (Kariakoo Sokoni)
Soko la Kariakoo ni soko kuu jijini Dar es Salaam na Tanzania ambapo kunafanyika biashara za aina zote za mahitaji muhimu ya kila siku ya binadamu. Biashara katika soko hili zinafanyika kwa jumla na rejareja.

Soko hili linajumuisha majengo mawili makuu (soko kubwa na soko dogo) pamoja na maeneo yanazunguka majengo hayo. Soko la Kariakoo lipo katikati ya jiji la Dar es Salaam na ndiyo chanzo cha eneo zima la Kariakoo kujulikana kwa jina hilo.

Jengo la Soko Kuu la Kariakoo lipo katika kiwanja namba 32 mtaani Kariakoo, katikati ya makutano ya mtaa wa Mkunguni na mtaa wa Nyamwezi na limezungukwa na mitaa ya Nyamwezi, Mkunguni, Sikukuu na Tandamti.

Mwaka 2021 soko hilo liliungua na moto jambo lililofanya shughuli sokoni hapo kusitishwa ili kupisha uchunguzi na badaye ukarabati, na mpaka kufikia April 2024 ukarabati wa soko hilo ulikuwa umefika 93%
  1. Informer

    Historia ya Soko la Kariakoo na Mchora ramani Beda Amuli

    Historia ya jina la Kariakoo na soko la Kariakoo inaanzia tangu enzi za ukoloni wa Mjerumani wakati Tanzania Bara ikiitwa Tanganyika. Mahala lilipo soko hilo palijengwa jengo la utawala wa Wajerumani ambalo lilikusudiwa litumike kama ukumbi wa kuadhimisha sherehe za kutawazwa kwa Mfalme Kaiser...
Back
Top Bottom