RIWAYA; KAMANDA WA ZAMU.
NA; BAHATI K MWAMBA.
WHATSAPP; 0658564341.
1.
Alikuwa akitetemeka mwili na roho, jasho lilimmwagika hadi kwenye ncha za vidole vyake vya miguu na mikono, miwani aliyokuwa ameivaa ni kama haikuwa ikimsaidia kwa lolote kwa sababu hakuwa akiona mbali...