Upotoshaji huibuka na kwenda sambamba na uwepo wa baadhi ya matukio yaliyopo kwa wakati huo. Mfano msimu wa usjili wa wachezaji, uchaguzi ama mlipuko wa magonjwa.
Je, upotoshaji gani unaoukumbuka uliowahi kutokea kwenye matukio kama hayo? Na ulichukua hatua gani?
Kumbuka kuthibitisha Taarifa...
Upotoshaji umekuwa ukifanyika katika namna tofauti tofauti ikiwemo kuhariri maudhui halisi yaliyo kwenye grafiki na kuleta maana tofauti.
Wapotoshaji wanaweza kubadili neno moja kutoka katika ujumbe ulio kwenye grafiki na hivyo kuleta maana tofauti kabisa inayoweza kuzua taharuki kwa jamii...
Wapotoshaji wanaweza kuhariri video halisi kwa kukata vipande vidogo vidogo na kuviunganisha kwa ajili ya kuharibu maana na hivyo kuleta maana tofauti yenye lengo la upotoshaji.
Thibitisha mara kwa mara iwapo utakutana na video unayoitilia mashaka, inayoonekana kuungwa ungwa, yenye mjongeo...
JamiiCheck ni Moja kati ya Majukwaa yanayopatikana ndani ya tovuti ya JamiiForums.com. Jukwaa hili limewekwa mahsusi kwa ajili ya kufanya uhakiki, kutafuta uthibitisho au uhalisia wa habari, taarifa, matukio, picha au video mbalimbali zinazojitokeza au kuibuka kutoka katika vyanzo mbalimbali...
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.