JamiiCheck
Senior Member
- Nov 3, 2023
- 101
- 125
JamiiCheck ni Moja kati ya Majukwaa yanayopatikana ndani ya tovuti ya JamiiForums.com. Jukwaa hili limewekwa mahsusi kwa ajili ya kufanya uhakiki, kutafuta uthibitisho au uhalisia wa habari, taarifa, matukio, picha au video mbalimbali zinazojitokeza au kuibuka kutoka katika vyanzo mbalimbali ndani na nje ya mtandao.
Tofauti na Majukwaa na vyombo vingine vya kuhakiki ukweli wa habari, JamiiCheck ni Jukwaa pekee linalotoa fursa kwa watumiaji wake (Wanachama wa JamiiForums.com) kushiriki katika uhakiki kwa kuleta taarifa, picha au Video mbalimbali ambazo wanahitaji kuzichunguza kupata ukweli au chanzo chake pamoja na kuchangia/ kutoa maoni kwenye taarifa nyingine zilizohakikiwa.
Ikiwa utakutana na habari au taarifa yoyote inayokutatiza, ambayo hujui kama ni ya Kweli, Uzushi au Nadharia, tafadhari ilete JamiiCheck ili iweze kufanyiwa uhakiki.