Shirika la NSSF liliingia ubia na kampuni ya Azimio kujenga mradi mkubwa wa nyumba uliokuwa na lengo kutoa makazi 7160 na vila 300 ili kuwafikia watu wa hali zote za vipato.
Walianzisha kampuni ya ushirika iliyoitwa Hifadhi Builders Limited ambapo NSSF walikuwa na hisa 45% na Azimio 55%. Katika hisa 55% za Azimio, 20% ilikuwa ardhi waliyotoa kujenga mradi huo huku 35% ilitarajiwa iwe fedha na ujenzi ulianza mwaka 2014.
Mwaka 2016 PAC ilipewa taarifa na NSSF kuwa mradi huo ulikuwa umesimama kutokana na ukosefu wa fedha na NSSF walikuwa tayari wametumia dola za kimarekani 129 milioni huku azimio wakitoa 5.5 milioni ikipendekeza wakati huo NSSF kuwa mwanahisa mkubwa zaidi.
Kila heka moja iliyotolewa na Azimio ilithaminishwa kwa milioni 800 ilhali thamani sokoni ilikuwa milioni 25.
Mwaka 2017 lilifanyika jaribio la kupiga mnada mradi huo na kampuni ya Yono baada ya kuthaminishwa, thamani yake ilitajwa $ milioni 350 za kimarekani.
Mwaka 2023 NSSF ilitangaza mradi wa Dege umeuzwa bila kutaja mnunuzi kwa thamani ya dola za kimarekani, milioni 220 na nyumba 3750 zilikuwa kwenye hatua mbalimbali za ujenzi.
Wana jamvi,
Kuna mradi mkubwa wa ujenzi wa magorofa unaendelea Kigamboni. Ni Kigamboni ndandani mbele Zoo na naambiwa unaitwa "Dege Eco Village".
Wengi wa wafanyakazi ni wazungu wenye asili ya Kituruki. Kazi inafanyika usiku na mchana.
Wenye ukweli kuhusu mradi huo mtujuze.
Karibuni...
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.