Mbunge wa Jimbo la Ubungo na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Mipango na Uwekezaji), Prof. Kitila Mkumbo, ameongoza kwa mfano kwa kuwa miongoni mwa watu wa kwanza kuhakiki taarifa zake katika Daftari la Kudumu la Mpiga Kura, baada ya kuanza kwa zoezi la uboreshaji wa daftari hilo Machi 17, 2025...