Ndagullachrles
Senior Member
- Jun 20, 2023
- 147
- 153
Tume huru ya Taifa ya uchanguzi,imetangaza kuwaondoa wapiga kura 594,494 kwenye Daftari la Kudumu la wapiga kutokana na kukosa sifa za kuwa wapiga kura .
Miongoni mwa wataoondolewa ni wenye CHANGAMOTO ya afya ya akili waliothibitishwa na mamlaka husika.
Wengine ni wale waliowekwa kizuizini kwa changamoto za afya ya akili na waliowekwa kizuizini kwa amri ya Rais.
Taarifa hiyo imetolewa mkoani Kilimanajaro na mkurugenzi wa huduma za kisheria wa Tume huru ya Taifa ya uchaguzi,Seleman Mtibora wakati akiwasilisha MADA kuhusu maandalizi ya uboreshaji daftari la Kudumu la wapiga kura awamu ya kwanza kwa wadau wa uchaguzi mjini moshi .
Aliwataja wengine watakaoondolewa kwa kukosa sifa ni wapiga kura waliofariki dunia,waliofungwa gerezani adhabu ya kifo,waliofungwa jela zaidi ya miezi sita pamoja na watanzania wenye utii wa nchi nyingine.
Katika hatua nyingine zaidi ya wapiga kura wapya 5.586,433 sawa na aslimia 18.7 ya wapiga kura wote wanatarajia kuandikishwa kwenye Daftari la Kudumu la wapiga kura.
Kwa mujibu wa Mtibora,zaidi ya wapiga kura 4.369,531 wanatarajia kuboresha taarifa zao wakiwemo waliohama kutoka eneo moja kwenda eneo jingine .
Kwa mujibu wa Taarifa hiyo ,Tume inatarajia kuwa na wapiga kura Milioni 34,746,638 huku mkoa wa Kilimanjaro ukitarajia kuwa na wapiga kura 1.190,266 baada ya ongezeko la wapiga kura wapya 180,540 huku kukiwa na vituo 1,316 vya kupigia kura .
Katika wilaya ya Ngorongoro mkoa wa Arusha baada ya serikali kurejesha kata 11,sasa wilaya hiyo itakuwa na Kata 44 na vituo 40,170 vya kuandikisha wapiga kura .