abdalla ulega

Abdallah Hamis Ulega ni mwanasiasa wa Tanzania kutoka chama tawala cha Chama Cha Mapinduzi CCM. Alizaliwa Septemba 28, 1979.

Ni Mbunge wa Jimbo la Mkuranga mkoani Pwani tangu mwaka 2015. Kwa sasa ni Waziri wa Ujenzi katika Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Kabla ya hapo aliwahi kuwa Waziri wa Mifugo na Uvuvi, akijihusisha na miradi ya kuendeleza sekta ya uvuvi, machinjio ya kisasa na ushirikiano wa kimataifa.

Katika wizara ya Ujenzi, amehusishwa na miradi mikubwa ya miundombinu kama barabara, upanuzi wa mradi wa mabasi yaendayo haraka Dar es Salaam na uzinduzi wa madaraja. Ni kiongozi anayejitokeza mara kwa mara kwenye vyombo vya habari akizungumzia masuala ya serikali na chama.
  1. DodomaTZ

    Waziri wa Ujenzi, Ulenga amewasili Mkoani Ruvuma, Desemba 20, 2025 kwa ziara ya kikazi

    Waziri wa Ujenzi, Abdallah Ulega (Mb) amewasili Mkoani Ruvuma kwa ajili ya kuanza ziara ya kikazi na kupokelewa na Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Brigedia Jenerali Ahmed Abbas Ahmed leo tarehe 20 Disemba, 2025. Katika ziara hiyo, Waziri Ulega atatembelea mradi wa ujenzi wa barabara ya Kitai - Amani...
  2. DuaZaMama

    GE2025 Ulega aiombea Mkuranga Barabara, manispaa na stendi

    Mgombea Ubunge wa Jimbo la Mkuranga kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Abdallah Ulega, amesema ujenzi wa viwanda unaoendelea wilayani Mkuranga tangu Rais Samia Suluhu Hassan aingie madarakani umeiongezea thamani na kwamba mambo matatu yakifanyika itapaa zaidi. Akizungumza katika mkutano...
  3. DuaZaMama

    Ulega: Rais Samia umeituliza nchi sakata la Dabi ya Kariakoo

    Waziri wa Ujenzi, Abdallah Ulega amesema hatua ya Rais Samia Suluhu Hassan kuingilia kati na kusuluhisha mvutano uliokuwepo kati ya klabu za Yanga na Simba kuhusu ratiba ya mchezo wao, imeleta utulivu mkubwa kwa Taifa na mashabiki wa soka nchini. Akizungumza leo Jumamosi, Juni 14, 2025, wakati...
  4. S

    KERO Ubovu wa Barabara ya Mwandege-Mkuranga!

    Habari wanajukwaa. Leo nimekuja mbele yenu kuleta mada ihusiyo ubovu wa Barabara ya mwandege-mkuranga. Barabara hii ni muhimu kwa mikoa ya kusini kutoka Dar. Kwa kweli barabara hii imejaaa makorongo na mabonde( tunaweza hata kufugia samaki). Kadhia tunayopata wasafiri wa njia hiyo ni kubwa...
  5. Waufukweni

    PreGE2025 Waziri Ulega avunja Mkataba wa Bil. 47 na Mkandarasi wa China kwa uzembe. Aagiza Zabuni mpya kwa Km 95.2

    Waziri wa Ujenzi, Abdallah Ulega ametangaza kuvunjwa kwa mkataba wa ujenzi wa barabara Mkoani Tanga baada ya Mkandarasi kutoka China kushindwa kutimiza masharti ya mkataba. Mkandarasi huyo, kampuni ya China Railway 15 Bureua Group anayejenga barabara ya Tanga - Pangani - Mkwaja Bagamoyo...
  6. Roving Journalist

    Waziri Ulega akutana na Wakuu wa Taasisi Wizara ya Ujenzi

    Waziri wa Ujenzi, Abdallah Ulega amekutana na kufanya mazungumzo na Wakuu wa Taasisi zilizo chini ya Wizara ya Ujenzi katika Ofisi ndogo za Wakala ya Barabara (TANROADS), leo tarehe 11 Disemba, 2024 Dar es Salaam. Kikao hicho kimehudhuriwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Balozi Eng. Aisha...
  7. M

    KERO Barabara Mkuranga siyo nzuri, kuchonga tu pekee haitoshi

    Jimboni kwa Mbunge Ulega hali ya barabara sio nzuri, wasaidie wakazi badala ya kutumia nguvu na pesa nyingi kuchonga.
Back
Top Bottom