VIDEO: Baadhi ya Wajumbe wa ZEC wapinga maamuzi ya Mwenyekiti wao kubatilisha Uchaguzi wa Zanzibar

RUCCI

JF-Expert Member
Oct 6, 2011
1,701
1,714


Muda mchache baada ya mwenyekiti wa tume ya uchaguzi ya Zanzibar (ZEC) Jecha Salum. kutangaza jaribio lake la kufuta uchaguzi mkuu wa Zanzibar 2015, makamishna wawili wa tume hiyo Ayoub bakari na Nassor khamis wameuita uamuzi huo kua sio wa ZEC, bali wa Jecha binafsi na wamejitenga mbali nao

Chanzo: DW kiswahili
 
Last edited by a moderator:
Hivi ikitokea mwenyekiti zec akajiuzulu kesho kwa madai ya kutofuata utaratibu.

Halafu mwenyekiti mpya akasema anahesabu kura upya na mwishowe ccm ikashinda kwa asilimia 2 thidi ya cuf tutafanyaje
 
Itakuwa ni vizuri tukisikia pia wajumbe wengine waliobaki wanasemaje kuhusiana na kadhia hii!

Tuachane na mambo ya wao kuwa washabiki wa cuf...maana hata wa ccm wapo humo humo. Swali ni rahisi sana...je kikao cha ZEC chenye akidi kilikaa na kuamua kufuta uchaguzi? Au Jecha alienda kujificha mahali na kujiamulia mwenyewe hatma ya nchi nzima?
 
Utasikia wamefukuzwa kazi kesho asubuhi.

Au wamewekwa kizuizini na jeshi la polisi.
 
Safiiiii, Wajumbe wa ZEC wako makini sanaaaaa... wamekata kutumika na CCM...!!! Wamekata kata kata kutumika na CCM...!!
 
Nadhani hawa ndiyo mawakala wa CUF, maana moja ya tatizo la uchaguzi ni kuwa kuna wajumbe walikuwa wanashabikia vyama. Wakamatwe hawa haraka sana

Mawakala wa vyama wapo NEC,ZEC! Hilo liko wazi. Hata waamuzi wa mpira,wapo wa Simba na Yanga, ni jambo la kawaida kwa binadamu kuwa na mapenzi kwa jambo fulani, cha msingi ni kuficha hisia!
 
Makamu mwenyekiti alishachukuliwa kwa nguvu na polisi na hajulikani alipo mpaka sasa hivi.
Ennh...! Ebana ndio mimi maana sipendi Siasa kuifuatilia hadi ukahatarisha Maisha yako na Maisha yalivyo Matamu kha! ni kukaa Mbali navyo hivi vitu.... Mfano niliuona kwa Wariaoba alipigwa hadi na watu wadogo kuliko watoto wake... na kumpoza wakampa mwanae agombee ubunge na kaukosa... kuhusu vyama wamuulize Mrema
 
Back
Top Bottom