Natoa msisitizo, UKAWA yapoteza ngome yake muhimu Arusha

Natoa msisitizo, UKAWA yapoteza ngome yake muhimu Arusha

funaku

JF-Expert Member
Joined
Oct 12, 2011
Posts
38,535
Reaction score
31,199
Thread hii siileti kishabiki bali ni mantiki na ukweli mtupu ambao hata wana UKAWA wanaukubali!

Jana nilileta thread kuwa UKAWA ARUSHA WAMECHANGANYIKIWA NA HAWAJIPANGA.
Nikasema Ukawa wameachwa na confusion na disorganisation.

Ni bahati mbaya thread hiyo siioni jukwaani pengine ni kutokana na tatizo la kiteknolojia!

Nimeleta threads kadhaa zinazoeleza kuhusu lema kushindwa kufanya kampeni,kukosa hoja na kupoteza jimbo la Arusha.

Ndio,nimeleta threads kadhaa za kuonesha hali mbaya ya UKAWA specifically CHADEMA ndani ya jiji la Arusha na ujio wa Magufuli.Mkutano wake ulidhihirisha ninayoyasema.

KUHUSU MKUTANO WA UKAWA ARUSHA

Nilisema kuwa chadema na Ukawa Arusha wamevurugwa baada ya Magufuli kufunika sana ndani ya jiji la Arusha.

Ujio wa Magufuli Arusha uliandaliwa kwa wiki kadhaa ingawa ulikuwa ni wa kimya kimya sana kiasi hata mimi niliogopa kuwa Magufuli angeshindwa kufanya mkutano Arusha...Lakini nilikuwa suprised!!!

CCM chama dola kina mbinu hatari sana kiasi cha kuwaacha watu mbalimbali ikiwa ni pamoja na viongozi wa maeneo ya kampeni kutojua ccm inakuja kwa style gani.

UKAWA hawakutegemea ni kivipi Magufuli ataweza kuijaza Shekh Amri Abedi bila kelele za matangazo ya magari jijini Arusha...kwa hiyo walirelax!kilichotokea ikabaki kuwa ni mshangao na kuchanganyikiwa!

UKAWA baada ya kuona "hurricane la nina" wakaanza kuhamasisha watu wa Arusha kuhudhuria kwenye mkutano wa lowassa Sinoni!! Bila mafanikio kwani ilikuwa ni too late!

Magufuli amefunika kikwelikweli ndani ya Arusha amefunika siku ya kazi kwa hiyo kuna maelfu ya wafanyakazi hawakupata fursa ya kuhudhuria.

TUONGELEE ENEO LA KAMPENI NA UWEZO WAKE

Kwa wakazi wa Arusha na hata nje ya Arusha wanafahamu kuwa jiji la Arusha halina kiwanja chochote ambacho ni kikubwa kuweza kubeba watu wengi zaidi ya Shekh Amri Abed...Arusha haina Jangwani!! Arusha haina Kirumba zaidi ya Stadium.

Kwa wenye uelewa zaidi watatambua kuwa hakuna shule yoyote ya msingi au sekondari yenye uwanja wa michezo unaoweza kubeba kile tuanachoita 'mafuriko' kama kipo nitahitaji kutajiwa sq meters na uwezo wake.

Hii ina maana kwa vyovyote vile hakukuwa na uwezekano wa mafuriko ndani ya viwanja vya shule ya sinoni!Kwa kuongezea ukweli ni kwamba viwanja vyenye uwezo wa mafuriko japo hafifu ni viwanja vya NMC ambavyo vimegeuzwa kuwa soko la wafanya biashara wadogo.

HII NI FACT NA NI MJINGA TU ANAYEWEZA KUPINGA.

MPANGILIO WA MKUTANO

Ni wazi kuwa Chadema na Ukawa Arusha hawakuwa na maandalizi yoyote ya kumpokea Lowassa kama mgombea urais kufanya kampeni Arusha...inawezekana sababu zikawa ni Chuki ya lema na Chadema asilia dhidi ya lowassa au kampeni za lowassa kuhodhiwa na Teamlowassa na washikaji zao!

LEMA ALIVYOPOTEZA GOLDEN CHANCE

Niliwahi kusema humu jamvini kuwa Lema anasubiri nguvu ya lowassa ili kuanza kampeni...lakini hili halijatokea ni ishara mbaya dhidi yake.

Mkutano wa UKAWA ulichelewa sana kuanza na mgombea urais alipanda jukwaani saa kumi na mbili kasoro dakika ishirini,ilipofika saa kumi na moja na dakika hamsini na sita akamuita lema ...hili ni pigo jingine!

Lema aliongea dakika chache sana chini ya 5 na mbaya zaidi akaishia kujihami kuwa UKAWA itaibiwa kura na kudanganya kuwa amejenga hospitali...ipi...mimi sihifahamu labda wakazi wa Arusha wanaifahamu!

Lema aliishia ku-bowdown to lowassa kwa kumuita mheshimiwa rais...na hakuna ahadi yoyote au neno lolote linalohusu ataifanyia nini Arusha.

lema aliishia kusema amepigwa na kwenda jela kwa ajili ya wana Arusha huku akisahau kuwa ni yeye mwenyewe alikuwa akifanya vitimbi na kuingizwa kisongo...hakwenda kisongo kwa niaba ya wana Arusha kamwe!!

Hata Nanyaro Ephata ambaye ni mgombea udiwani kata ya levolosi na mwanaJf wa Ukawa aliyejaribu kurusha updates za mkutano hakupata nafasi ya kutambulishwa au kujitambulisha kwenye mkutano huu muhimu.

HITIMISHO

Mkutano wa chadema haukuwa na maandalizi.

Mkutano wa chadema haukuwa na hoja.

Mkutano wa chadema ulikuwa na mahudhurio hafifu.


Mkutano wa chadema ulipuuzwa na wananchi weledi.

Mkutano wa chadema haukutoa fursa kwa lema kunadi sera.

Mkutano wa chadema haukufikia hata robo ya ule wa Magufuli.

Mkutano wa chadema umeshindwa kuufunika wa Magufuli.

Mkutano wa chadema Arusha umechora mstari kuwa MAGUFULI ANASHINDA KWA KISHINDO.


Nichukieni leo lakini mtanipenda kesho!!

KWA HISANI YA MTU WA TANZANIA!!

Ni mimi jingalao wa JF
 
Last edited by a moderator:
Laaambwa laambwaa lwambatika,maharage yako jikoni.......malizia
 
Ukawa hawana ngome yeyote labda Pemba ndiyo ngome ya CUF huko Arusha na Kilimanjaro wabunge wengi wanatoka CCM.


Hahahahaaaa Arifu naona upo front line kumpigania Gufuli mi naandika tu!!
 
kwa hiyo ccm mlijiandaa sana kutoa watu wilaya tofauti lakini ukawa wamefanya mkutano bila maandalizi na nyomi ya kufa mtu. Unajua pia leo kulikuwa na nyomi USA river ambayo nayo ni arusha? linganisha na Magufuli!
 
Hivi kumbe na kura za watu wa kaskazini mnazitaka? subirini majibu yenu tarehe 25 ndio mtapata tiba yenu na ndio utakuwa mwisho wenu wa kuropoka na kuwakejeri watu wa kaskazini.

Wale wapare mliwasomba kwa maroli siku ya kupiga kura hawatokuwepo Arusha watakuwa majimboni kwao ndio mtaijuwa hasara ya kujitekenya na kucheka mwenyewe.
 
Hivi kumbe na kura za watu wa kaskazini mnazitaka? subirini majibu yenu tarehe 25 ndio mtapata tiba yenu na ndio utakuwa mwisho wenu wa kuropoka na kuwakejeri watu wa kaskazini.

Wale wapare mliwasomba kwa maroli siku ya kupiga kura hawatokuwepo Arusha watakuwa majimboni kwao ndio mtaijuwa hasara ya kujitekenya na kucheka mwenyewe.
Kwani hao wapare unaowaponda wanatoka wapi Kenya?
 
kwa hiyo ccm mlijiandaa sana kutoa watu wilaya tofauti lakini ukawa wamefanya mkutano bila maandalizi na nyomi ya kufa mtu. Unajua pia leo kulikuwa na nyomi USA river ambayo nayo ni arusha? linganisha na Magufuli!
Nitajie wilaya iliyoleta nyomi ya Magufuli Arusha.
 
Kupitia ITV yule Farhia Middle kasema kuwa Mkutano wa leo umevunja Rekodi ya Mikutano yote.....
Mji wa Arusha ulisimama kwa masaa kadhaaa
 
Mkutano wa UKAWA leo katika jiji la arusha no 5× ya ule alioufanya maguful sasa wewe unaosema ukawa wamepoteza dira wait and u wil prove on 25th this month
 
Kupitia ITV yule Farhia Middle kasema kuwa Mkutano wa leo umevunja Rekodi ya Mikutano yote.....
Mji wa Arusha ulisimama kwa masaa kadhaaa
Waulize ITV kwa nini hawakuleta live mkutano huo?
 
Waulize ITV kwa nini hawakuleta live mkutano huo?

Wamesema tatizo lilikuwa Umeme...
Hivi kwanini Magazeti ya jana hayakuonesha habari za Arusha? Sababu mlifoji picha
 
Tulia hivyo hivyo
 

Attachments

  • 1444328339778.jpg
    1444328339778.jpg
    119.9 KB · Views: 1,887
Back
Top Bottom