Imebainika: Mwaka huu wanaume wote wanaolelewa na wanawake lazima waachike

Imebainika: Mwaka huu wanaume wote wanaolelewa na wanawake lazima waachike

Old Member (Retired)

JF-Expert Member
Joined
Sep 29, 2012
Posts
3,402
Reaction score
1,618
Mwaka 2014 umekuwa mwaka mbaya sana kwa wanaume wenye miguu na mikono miwili lakini wanalelewa na wanawake. Wanaume hao ambao jijini Dar wamekuwa maarufu sana kama ''Marioo/mtaji kiuno'' wamekuwa wakigubikwa na mikasa mizito sana na hatimae kutimuliwa kwenye nyumba za wanawake waliokuwa wakiwalea.

1. Kundi hilo kubwa la ''Marioo'' Mwezi huu wa nane 2014 limeshuhudia tukio la aina yake baada ya Raisi wa Marioo nchini kutimuliwa kwa mke wake na hivi sasa anaishi kwa ndugu yake, Marioo huyo ambaye ameleta mshtuko wa aina yake jijini inaripotiwa kuwa ni yule aliyehama redio ya mawingu na kuhamia kituo kingine chenye ofisi zake Kawe Beach.

2. Ofisi hiyo ya Kawe ikiwa bado haijamaliza vizuri machungu ya Marioo wao mwingine ambae pia ilimbidi aondoke nyumbani kwa mwanamke baada ya kulelewa kwa muda usiojulikana. Mwanamke aliyemuacha Marioo huyo ni mtangazaji wa kituoni fulani cha redio huku akikamilisha ndoa kama si ya tatu basi ni ya nne.

3. Bado Marioo nchini Tanzania wanaomboleza kwa masikitiko makubwa juu ya kijana mwenzao ambaye alivamiwa njiani akiwa ametoka kuachika, kijana alitembea kwa mguu usiku wa manane kwani hakuwa na pesa yoyote ile. Marioo huyo alijichora tatoo ya mwanamke lakini aliachika kwa kupigwa mawe na kukataliwa kuingia kwenye nyumba ambayo hajawahi kuchangia hata kununua LUKU.

4. Kutokana na hayo yote Marioo kwa vinywa vyao wamekiri kuwa ambao bado hawajaachika wajiandae kwani hawajui siku wala saa, hilo limezungumzwa na aliyekuwa makamu wa raisi wa Marioo nchini ambaye ndiye Marioo anayeongoza kwa kuachika kwa visa vya aina yake, Marioo huyu bado ana kesi ya kubaka ipo mahakamani, chanzo cha kuachika kwake ni baada ya mke wake (muimbaji maarufu) kupata mtu wa kumlea ambapo tayari ameshanunuliwa LIJI-Prado.

_______
UPDATE

Mario aliyezungumziwa hapo kwenye namba mbili hivi sasa amerokodiwa video ya utupu na aliyekuwa akimlea baada ya kuachika kwa yule mtangazaji
..........................................................

Kwaniaba ya JamiiForums SUPU YA MAWEninawapa pole Marioo wote nchini (Kuanzia raisi wao mpaka Marioo wa kawaida) kwa kipindi kigumu wanachopitia, Mungu awatie nguvu a ujasiri.

Posted by: SUPU YA MAWE
 
Teh teh Mambo ya MCHUNGZI HURU (PhD)
 
Last edited by a moderator:
Haya mwenye kuwajua rais na makamu wa raisi wa marioo's atujulishe.
 
Leo umenichekesha, naskia kuna mwingine yuko mbioni kuachika, tena alikuwa kaajiriwa na mkewe na hivi sasa ni sterling msaidizi katika tangazo la utii bila shurti.
 
hahahahahah Kongosho utii bila shurti
Leo umenichekesha, naskia kuna mwingine yuko mbioni kuachika, tena alikuwa kaajiriwa na mkewe na hivi sasa ni sterling msaidizi katika tangazo la utii bila shurti.
 
Last edited by a moderator:
TEAM Marioo mwaumbuka uku jamani fanyeni kama mnapita hapa
 
Last edited by a moderator:
Jamani mbona mnawasakama sana mario.Mimi binafsi nawapongeza kwa kujiajiri
 
Duh! Mmenikumbusha wimbo wa salam za wagonjwa mahospitalini, tunawapa pole. Ulikuwa masruf sana RTD.
 
Leo umenichekesha, naskia kuna mwingine yuko mbioni kuachika, tena alikuwa kaajiriwa na mkewe na hivi sasa ni sterling msaidizi katika tangazo la utii bila shurti.
Wewe uko wapi huyo mtunza bustani wa je wajuwa si ndio Rais wa Marioo?
 
hahahahahaha
Katika watu ambao wana niacha hoi kwa vicheko kila ninapo ona mada zao humu jf ni wewe MUCHUNGUZI huru na wakishua..... daaa jf ina watu wa pekee sana sijui huwa mnafikiri nini. daaaa mnasaidia kutuongezea siku za kuishi kwa vicheko..

Hii ya leo imeniacha hoi sana ulivyo pangilia kuanzia cheo cha Rais na vyeo vya kushuka chini.
Yote tisa hile ya Ugomvi wa Mungu na shetani ndio ilitaka kunipasua mbavu daaa.
Lakini hii ina ujumbe mzuri sana.

Hii lazima wa wa viblog wa copy
 
Mara ya mwisho kuwa Mario ulikuwa mwaka 1992,, mario wa leo mnaweza ni PM mjue shida ya kuwa mario... si deal kabisa achani tabia hii ni aibu sana
 
Back
Top Bottom