Nitamuunga mkono mgombea Ubunge yeyote wa chama changu (CCM) jimbo la Ubungo kumng'oa Mnyika

Nitamuunga mkono mgombea Ubunge yeyote wa chama changu (CCM) jimbo la Ubungo kumng'oa Mnyika

Juliana Shonza

JF-Expert Member
Joined
Dec 19, 2012
Posts
2,009
Reaction score
1,609
919665090.jpg


Njama za kunigombanisha na kunifuatilia kwa mtindo hasi katika siasa zangu ni kuishiwa kwa uwezo wa kufikiria.

Nimeshangaa kuona gazeti uchwara limeandika kwamba Nitagombea ubunge UBUNGO. Kama mmeishiwa habari nendeni mikoani mkatafute habari.

MIMI NITAMUUNGA MKONO MGOMBEA YEYOTE WA CHAMA CHANGU(CCM) ATAKAYE GOMBEA UBUNGE JIMBO LA UBUNGO NA SEHEMU YOYOTE NDANI YA TAIFA LANGU.

NITAMUUNGA MKONO ZAIDI MGOMBE UBUNGE JIMBO LA UBUNGO KUPITIA CCM KUHAKIKISHA MNYIKA ANANG'OKA, MIMI NI MZAWA WA UBUNGO NAISHI UBUNGO.

HAKUNA AHADI ALIYOITEKELEZA HUYO MNYIKA, TATIZO LA MAJI LIMEMFIKA SHINGONI. NA HILO LITAKUWA CHAPUO LA YEYE KUNG'OKA.

HIVYO BASI,WATANZANIA WENZANGU HABARI ZA KUUNGA UNGA ZENYE LENGO LA KUNISAKAMA KISIASA NAOMBA MZIPUUZE.

CCM CHAMA CHENYE HADHI YA KITAIFA,CCM IMARA,CCM JIKO NA CHIMBUKO LA VIONGOZI BORA, MAKINI NA UTAWALA BORA.

Asanteni
 
Amepwaya huko CCM! Asubiri kuwafuata kwenye benchi Masumbuko Lamwai, Kabouru, na wengine wengi
 
Na mimi niko ubungo tena mshika dau!!! Mnyika ni mbunge forever!!! Jaribuni kama ilivyokuwa 2010 si cha moto mlikipata? Mnahujumu miradi ya maji ubungo ili kumtesa mnyika? Mbona hii issue inajulikana wazi na maagizo yalitoka juu kwa wazazi wako ulikorudi? Bora ukae kimya huhitajiki hapa!! Wewe si mzalendo na huna uchungu na watanzania!! Endelea kuchumia tumbo!!! Sisi tutaendelea kuhangaika juani na siku moja tutalia kivulini!! Siasa za njaa hazina mashiko.
 
Naapa leo tarehe 13/2/2013

Mnyika atarudi bungeni 2015 kwa vyovyote vile kwa njama zote zile anazofanyiwa na CCM atarudi naomba tukutane majukwaani na huyo mgombea wenu.

Nani asiyejua mnyika anahujumiwa na serikali kuhusu maji ubungo pamoja na juhudi zote za mnyika serikali bado ina mrudisha nyuma.

Majuzi hoja yake juu ya maji imepigwa chini kwa fitna na kuogopwa kwamba ingejulika watu wametafuna pesa za maji na usambazaji wa maji.

Huna nguvu yoyote nikuambie shonza utahangaika sana lakini Mnyika atabaki kuwa mbunge bora ndiye alisimamia serikali vizuri kwa miaka 3 niambie charles keenja kipindi cha miaka 10 alikuletea maji ubungo.

Tatizo la maji ubungo na tanzania ni serikali haina mipango ya miaka 100 ijayo ramani ya maji ya sasa ni ya kipindi ya miaka ya 70 wakati dar ina wakazi laki 8.sasa wakazi ni zaidi ya milioni 6 miundombinu ile ile bado kutakuwa na tatizo.

Nikutakie safari njema huko CCM najua mwisho wako umefika nakuomba uwe hai ushuhudie mnyika akirudi bungeni kwa kishindo kikubwa.
 
Kulikuwa na sababu gani zakuja na habari hii ikiwa umeibariki ile ya kwanza uliyoileta wewe mwenyewe na kuiburuzia kiwese?

Usitufanye wajinga binti!

Dada hebu pembuka basi jitulize moyo na akili usije pata shhinikizo la damu ungali kigori!

Mods unganisheni hii comment na uzi wake aliouleta jana huyu dada!
 
hivi huyu dada ana matatizo gani wanajamvi??

Well, ngoja tuheshimiane kama binadamu yeyote anavyotakiwa kuheshimiwa.

  • Unadhani tatizo la Ubungo ni maji pekee?
  • Je, una uhakika tatizo la maji liko Ubungo pekee hapa tz?
  • na je, unadhani hoja ya Mh. Mnyika ya kutaka CAG akague/afanye accountability ya value for money ya Billion 340 (?) zilizotumika na wizara ku-upgrade mradi wa maji DSM (maji ya wachina) ccm wataweza kuzitolea maelezo?
Katafute maarifa zaidi dada mdogo
 
Wala huna nguvu yoyote ya kisiasa wewe.Graduate gani huwezi hata kuandika?Umesahau mahojiano yako na Mtanzania?Kweli una njaa kali?Leo ndio unagundua hicho chama?Ulitaka nini huku cdm?Huna jipya.waulize wenzako kina Hiza.Mnyika sio saizi yako tafuta mwingine wa kutaka kujipatia umaarufu mwana.
 
Tulishakusahamu msaliti masalia wewe. Umejileta hapa tutakuchambua kama karanga!!! Pita mbali na wazalendo!! Sisi hatuki mafisadi, wezi, waongo, wasaliti, masalia, mamluki,et. Ulishtukiwa na wakakukaanga kwa mafuta yako mwenyewe. Njoo hapa. Leo utaomba urudi kuwa mtoto kuepuka grenades za hapa!! Huna sifa wala mvuto kisiasa!! Subiri wanatayarisha bench la mabeki maana lile la kina Masumbuko Lamwai, Kabarou na wenzako wengi limejaa!!! Umevamia meli baada kushindwa kutekeleza ulichoagizwa kuifanyia CDM? Take it is madam!!
 
We mtoto unajua siasa wewe...!?"eti siasa zangu...",hovyoooo!Sema unataka Mnyika ang'oke kwa chuki zako,huna lolote kwenda huko
 
Back
Top Bottom