Nape: Mahakama ya Mafisadi inakuja na kesi zake zitaharakishwa!

Nape: Mahakama ya Mafisadi inakuja na kesi zake zitaharakishwa!

Jay One

JF-Expert Member
Joined
Nov 12, 2010
Posts
18,535
Reaction score
20,710
Leo mchana, Nape akihojiwa na BBC amesema, Mahakama ya Mafisadi iliyoahidiwa na Magufuli inakuja kweli na watu wajiandae kuburuzwa mahakamani.

Nape amesema mahakama hii itakuwepo na kazi yake ni kushughulikia kesi zinazohusu matumizi mabaya ya madaraka na rushwa.

Amesisitiza kuwa tumekuwa na kesi nyingi zinazochukua muda mrefu sana na ni hasara kwa nchi kwani nyingine hadi unamsimamisha Mkurugenzi.

Ametolea mfano huo wa kusimamisha wakurugenzi kuwa kesi inaweza kuchukua miaka kuisha muda wote huu unamlipa mshahara wale bila kufanya kazi akasema ni bora tukawa na mahakama hiyo ili kufanya kesi hizi ziishe haraka!

"Chukulia kesi kama za EPA, kesi kama za kina Mramba, kuna mkurungenzi kesi ilichukua miaka sita inaendeshwa tu!" alisema Nape.

Nape amesema hivi leo watuhumiwa wa Richmond ndio wengine wanataka kwenda Ikulu. Akaongeza kuwa Mahakama za kawaida zina urasimu mwingi sana na mtu akiwa na madaraka na pesa ndio kabisa!

Amemalizia kwa kusema kuwa Mahakama maalum ya Mafisadi ni muhimu na inakuja!
 
Hata ikiundwa haitaganya chochote
 
Mbona ile kauli aliisema wazi na wote tulisikia. Tunao uwezo wa kutafasiri yaliyosemwa na wengi tulishangaa kauli ile kwa sababu mahakama tunazo. Hata hivyo mlishajiuliza hao mafisadi wa kupelekwa mahakama hizo wangetoka wapi?
 
Hawawezi kuanzisha Mahakama ya Mafisadi ili hali wao ndio mafisadi namba moja.
ESCROW=CCM
RICHMOND=CCM
KIWIRA=CCM
FERRY BOAT CHAKAVU=CCM
KAGODA=CCM
TWIGA KUPANDA NDEGE=CCM
UJANGILI MENO YA TEMBO=CCM
UFISADI RADA=CCM
WIZI WA KURA=CCM
BARABARA MBOVU=CCM
MEREMETA=CCM
MISHAHARA HEWA=CCM
HUDUMA MBOVU ZA JAMII=CCM
KILA UOVU=CCM.

SASA HAPO MAHAKAMA YA MAFISADI ITOKE WAPI?
 
Sidhani kama kuna mtu ye yote aliyekuwa akiamini kauli hiyo kwa sababu Makufuli mwenyewe ameshiriki kikamilifu katika vitendo vya kifisadi kama vile kusimamia ugawaji wa nyumba za serikali miongoni mwa wateule. Na alikwenda zaidi ya hapo, na kumgawia kimada wake. Sasa angejipeleka katika hiyo mahakama? Watanzania wamemchagua Magufuli si kwa sababu nyingine, bali kwa kuogopa mabadiliko. Watanzania tu waoga sana na kwa sababu hiyo hatuna ule moyo wa ujasiriamali (msingi wa ujasiriamali ni kuthubutu kuchukua hatua, kutokuwa mwoga), na hivyo tutaendelea kubaki nyuma. Hata mfumo na mitaala ya elimu yetu haikusukwa kuchochea na kupanda mbegu ya uthubutu, bali woga woga na kutojiamini. na huo ndio mtaji mkuu wa mafisiemu.
 
Hawawezi kuanzisha Mahakama ya Mafisadi ili hali wao ndio mafisadi namba moja.
ESCROW=CCM
RICHMOND=CCM
KIWIRA=CCM
FERRY BOAT CHAKAVU=CCM
KAGODA=CCM
TWIGA KUPANDA NDEGE=CCM
UJANGILI MENO YA TEMBO=CCM
UFISADI RADA=CCM
WIZI WA KURA=CCM
BARABARA MBOVU=CCM
MEREMETA=CCM
MISHAHARA HEWA=CCM
HUDUMA MBOVU ZA JAMII=CCM
KILA UOVU=CCM.

SASA HAPO MAHAKAMA YA MAFISADI ITOKE WAPI?

#HapaKaziTu...CCM ni ile ile ni ile ile!
 
Hawawezi kuanzisha Mahakama ya Mafisadi ili hali wao ndio mafisadi namba moja.
ESCROW=CCM
RICHMOND=CCM
KIWIRA=CCM
FERRY BOAT CHAKAVU=CCM
KAGODA=CCM
TWIGA KUPANDA NDEGE=CCM
UJANGILI MENO YA TEMBO=CCM
UFISADI RADA=CCM
WIZI WA KURA=CCM
BARABARA MBOVU=CCM
MEREMETA=CCM
MISHAHARA HEWA=CCM
HUDUMA MBOVU ZA JAMII=CCM
KILA UOVU=CCM.

SASA HAPO MAHAKAMA YA MAFISADI ITOKE WAPI?
Umesahau nyumba za serikali kuna mtu alimpa hadi mchepuko wake. Hivi kile kidude cha Like kiko wapi? Mimi sikioni!
 
hatuwasikilizi,hatuwaamini tena. Mlichonga mambo mengi ya uongo haikusaidia kitu,mmeletea Mkorea kuja kuchonga matokeo pia haikusaidia kitu na hii taarifa pia ni ya kuchongwa na Mkorea mweusi pia hatuiamini
 
Na sio hayo tu, hakuna watakalolitekeleza maybe kushikana uchawi wenyewe kwa wenyewe😀
 
..sheria ya UHUJUMU UCHUMI ipo.

..wananchi/waandishi walipaswa kuhoji ahadi ya Dr kuhusu kuanzisha mahakama ya mafisadi na wahujumu uchumi.

..Kama kungekuwa na debates, au Dr.Magu angefanya interviews na vyombo vya habari, basi kungekuwa na nafasi ya kumuomba ufafanuzi kuhusu ahadi yake hiyo.

cc President Lowassa, sifongo
 
Last edited by a moderator:
Mtaisoma namba imekula kwenu na hakuna zile mil50 kila kijj
 
Yaani... nimechoka na maumivu yamezidi baada ya kumsikiliza Nape leo...!!
 
Kwenye maandiko matakatifu huwa kuna maneno yasiyo na maana ya moja kwa moja, labda na mhe. dr Magufuli alikopi maana hizo ili baadae aje atutafsilie maana, (ni fikra zangu km haitakuwepo)
 
Hilo swala la uundaji mahakama ya ufisadi haliwezekan coz mteule mwnyw ni miongoni mwa watuhumiwa wa ufisadi nchini kwn mpk ss mpk hajakanusha tuhuma dhidi yk juu ya uhusika wake ktk mchakato wa uuzaji nyumba za serikal, mtambo feki na mmbovu wa kukatia tiketi kigamboni, boti mbovu, kutohedhimu utawala wa sheria, tuseme tu lugha moja kwamba hy ilikua trick ya kuombea kura kwn hawezi fanya ilihali nae ni miongoni mwa watuhumiwa
 
Nimerudi tena, hawawezi jenga coz huko si ndio wamejaa:what:
 
Back
Top Bottom