Wanafunzi wa Stashahda ya ualimu masomo ya Sayansi, Hesabu na Teknolojia UDOM warudishwa nyumbani

Wanafunzi wa Stashahda ya ualimu masomo ya Sayansi, Hesabu na Teknolojia UDOM warudishwa nyumbani

Halafu hao Stashahada wa nini sasa UDOM?si kuna vyuo kibao vya Stashahada?sasa hao UDOM wanaanzisha stashahada ya nini sasa?au ndo kuongeza vitega uchumi
 
UDOM, kazi wanapeana, wanafunzi wengi walimu wachache, mnaita watu interview wakati tayari mnawatu wenu...mnawatesa watoto wa watu wanaishi maisha magumu.
wakati uwezo wa kuajiri mnao...Tanzania bila Kupendeleana inawezekana...Epuka Rushwa
Ni kweli mkuu UDOM ni jipu kubwa sana chuo ni kizuri kwa muonekano wa nje lakini taaluma ni mbovu kabisa....kwanini serikali isishughulikie matatizo ya chuo hiki inaumiza sana...serikali imewekeza kwa kujenga majengo mengi likini ovyo tupu mambo ya UDOM...MH waziri nenda ushuhudie mwenyewe mama...why kila siku UDOM UDOM Tunaumia.
 
Prof. Ndallichako yuko sawa. Wewe utamchukuaje form 1V kuchukua masomo ya diploma bila ya kuandaa program na hata kusoma masomo ya Advanced Level?.
Tanzania tumechezea elimu na itakuwa ngumu kupiga hatua kimaendeleo.
Lakini kuna simulizi za nyuma; wanasema utawala wa Mwarabu haukuwa na shida kuelimisha watu kwa vile hikuwa agenda yao maana mwenyeji alikuwa ni mtumwa tu. Alivyokuja Mjerumani akajaribu kuweka mfumo wa elimu lakini kwa vile viwango vya Kijerumani ni vya juu na wako strict na ukijumulisha na 'brain wash' iliyokuwa imefanywa na mtangulizi wake' basi naye akakumbana na mikiki. Sasa alivyokuja Mwingereza akaweka mfumo mmoja kwa East Africa maana zote zilikuwa chini yake. Kenya na Uganda zilienda haraka sana na vizuri na nasikia sehemu kubwa ya jamii zao zilikuwa receptive hadi kujengwa Makerere. Nasikia hapa kwetu tangia enzi hizo, ukiondoa jamii chache na zilizokuwa pemezoni mwa nchi ndizo zilikuwa receptive lakini wengi hawakutilia maanani na bado Waingereza waliweka nguvu kubwa kujenga mfumo ili uendane sawa na member states za EAC (mjue haya mambo hayakuanza leo).
Sasa alivyokuja Mwalimu kwa nia njema tu moyoni lakini iliyo na uhalisia mgumu kivitendo akapindua mfumo huo ambao kama tunavyoshuhudia leo kuwa products nyingi alizotengeneza zimezaa wale Mh. Bashe aliowaita wanafiki na watu wa kujipendekeza ambao wamegeuka tools za underdevelopment badala ya development!

Maelezo marefu lakini hoja yangu ni kusupport hoja ya mkuu koryo kwani nakumbuka Wakenya waliokuwa wakijiunga na vyuo vya Uganda hasa KIU walikuwa wakipewza kozi maalumu ya miezi sita nadhani ili kucover ile dhana ya Wakenya kutokuwa na Form Six. Prof. Ndalichako anaweza akawa sahihi lakini ndio hivyo anajaribu kufanya 'operation ya moyo uliokwisha simama'.
Je, tukiwekana sawa, haya ndio matunda ya Dr. Kawambwa na Division Five zake!? Na je, tunajua waziri atakayekuja baadaya miaka mitano au kumi mingine ataleta division ten!
 
Wanafunzi waliofukuzwa kinyama UDOM hivi sasa wanatangatanga mjini Dodoma! Hawana la kufanya wala hawajui watalala wapi leo hii!

Ni unyama uliopitiliza kufanywa na serikali yetu inayojinasibu kuzingati haki za binadamu!

Wanafunzi 7000 wamefukuzwa bila kuandaliwa usafiri! Mabasi yote yamejaa na itachukuwa siku mbili au zaidi wote kupata usafiri wa kurudi makwao!

Kwa muda wote huo wataendelea kupigwa na baridi kali wakiwa stendi!

Huu ni unyama!!!

Mabasi yamejaa sababu Dodoma kulikuwa na mkutano wa Masecretary toka pande zote za Tanzania. Masecretary waliokosa au kughairi usafiri jana ndio wameondoka leo asubui. Sasa jumlisha na hao wanafunzi na wasafiri wa kawaida. Migomo kwa pande zote yaani walimu au wanafunzi sio mizuri.
 
Ndo hivyo Imeisha tokea wenzao wanapeta form six hivyoo wenda selikali itawapa uhakika but mjue sasa hivi ni uncle magu
 
Ni kweli mkuu UDOM ni jipu kubwa sana chuo ni kizuri kwa muonekano wa nje lakini taaluma ni mbovu kabisa....kwanini serikali isishughulikie matatizo ya chuo hiki inaumiza sana...serikali imewekeza kwa kujenga majengo mengi likini ovyo tupu mambo ya UDOM...MH waziri nenda ushuhudie mwenyewe mama...why kila siku UDOM UDOM Tunaumia.
Nadhani kama Bunge lisinglikuwepo Dodoma nadhani labda hili lisingelifikia hapa. Labda ni mivitano ya wa Chama Tawala na Wapinzani???????. Nadhani kila kundi lina shughulika huko kutumia waalimu au wanafunzi. Kama ni hivyo Mh Rais na Rais Mstahafu pia Uongozi wa Chuo hawana tatizo bali siasa ndio tatizo. Siasa na elimu ni maji na mafuta. Huweza kuleta madhara makubwa Chuoni.
 
Nategemea wabunge wetu watalikomalia hili ili Prof. Ndalichako atoe taarifa ya kiserikali. Haingii akilini kugoma (kama ni kweli) wagome walimu lakini wanaofukuzwa ni wanafunzi. Na cha kushangaza ni pale unapo ambiwa nenda nyumbani na hatma yako tutakueleza ukiwa huko huko. Kuna kipi tusichokijua hapa?

Hii special diploma ni kitu gani? Nani anaisimamia NACTE au TCU.?
 
Kinaharibiwa na wahadhiri wa UDSM
na ndo najiuliza kwani palikuwa na haja ya hao wahadhiri wa Dar kiko-control? Au wanajaribu kupeleka system zao mule. Na kama kina upungufu wa wafanyakazi hata kama watawachukua wengine UDSM kwa nn wasipewe muongozo wa chuo cha Dom kilivyo na kuacha kukiendesha jinsi wanavyotaka. Kile ni chuo kikubwa sidhani kama kulikuwa na haja ya kuajiri watu toka UDSM ni.bora wangechukua watu wengine ikiwezekana hata walimu kutoka nje. Kuna watanzania weengi tu wanafundisha vyuo vikuu mbele.
 
Halafu kumbe ni form four leaver,ilikuwa form four anakwenda kusomea diploma ya ualimu badala ya kusoma cheti cha ualimu?kama ni special program kama wanavyodai kwa nini wasingechukua A level leaver au walimu walioko mashuleni ambao wana cheti tayari?Hapa serikali ilichemsha kwa kweli,au ndo hawa sababu ya TCU vibosile kusimamishwa?
 
Naamini watanzania ni haki yetu kuelezwa kitu gani kinaendelea UDOM na serikali ina role gani kwenye hili? Itakuwaje wagome walimu lakini wachukuliwe hatua wanafunzi. Matatizo ya kufundisha ndiyo yapi? Haya matatizo yako UDOM tu au......? Hii special diploma iko chini ya NACTE au TCU? Inafiti vipi kwenye mitaala yetu. Na ilipoanzishwa UDOM walishirikishwa vipi au ndio walitupiwa zigo la misumari? Hili jambo ukichanganya na yale ya St. Joseph yanaashiria nini kuhusu elimu yetu ya vyuo vikuu? Labda ni wakati muafaka kuwa na HAKI ELIMU ya vyuo vikuu.
 
Back
Top Bottom