Tatizo la upungufu wa matundu ya vyoo katika shule za Manispaa ya Shinyanga, limeendelea kuwa changamoto inayotishia afya na ustawi wa wanafunzi, huku baadhi yao wakilazimika kujisaidia vichakani kutokana na vyoo kujaa, kuchakaa na kutokidhi idadi ya wanafunzi.
Mbali na upungufu huo, baadhi ya...
Licha ya juhudi mbalimbali zinazofanywa na serikali katika kuwekeza na kuboresha sekta ya elimu nchini, hali halisi bado inaonyesha uwepo wa pengo kubwa la miundombinu.
Katika Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga, shule nyingi za msingi na sekondari, zinakabiliwa na changamoto kubwa ya upungufu...
AFYA za wanafunzi wa shule za msingi na sekondari katika Manispaa ya Shinyanga zipo hatarini kutokana na tabia ya kujisaidia hovyo, hali inayochangiwa na upungufu mkubwa wa matundu ya vyoo pamoja na ukosefu wa vyumba maalumu vya kujistiri wakati wa hedhi kwa wanafunzi wa kike.
Uchunguzi...
"Wakulima kutambua kwamba kilimo sasa hivi ni biashara,” huu ni wito wa Afisa Kilimo wa Mkoa wa Geita, Mayunga John, ukibeba majibu ya mojawapo ya changamoto kubwa ambayo imeendelea kuwagharimu wakulima wa mkoa huo kwa miaka mingi, upotevu wa mazao ya chakula baada ya mavuno.
Katika sehemu...
Baada ya kufuatilia namna ambavyo uhifadhi duni unavyoendelea kusababisha upotevu wa mazao na hasara kwa wakulima katika mkoa wa Geita, swali linalobaki ni kwa nini tatizo hili linaendelea kujirudia mwaka baada ya mwaka? Licha ya kuwepo kwa sera ya kilimo, maafisa kilimo pamoja na teknolojia za...
Kwa wakulima wa mazao ya chakula katika wilaya ya Geita, mkoani Geita kuvuna si mwisho wa safari ya kupata kipato. Baada ya miezi kadhaa ya maandalizi, kupanda na kusubiri mavuno, hatua inayofuata ya kuhifadhi mazao ndiyo huamua kama jasho lao litageuka kuwa fedha au kupotea bila faida.
Baadhi...
Baada ya kubaini ukubwa wa tatizo la ukataji wa miti ovyo na kuchambua sababu zake pamoja na wajibu wa wahusika, swali linalobaki ni moja: Je, Tanganyika ina uwezo wa kuokoa misitu yake au itaendelea kushuhudia uharibifu hadi rasilimali hii itakapopotea kabisa?
Uchunguzi unaonyesha kuwa pamoja...
Katika makala iliyopita, uchunguzi huu uliibua hatari inayolikabili eneo la Tanganyika mkoani Katavi, ukataji wa miti ovyo unaotishia si mazingira pekee, bali pia mapato ya zaidi ya shilingi bilioni 29 yatokanayo na biashara ya kaboni.
Lakini nyuma ya miti inayokatwa na mashamba yanayopanuka...
Katika kukabiliana na uhaba mkubwa wa maji safi na salama unaoikumba Kata ya Mkwajuni pamoja na kata nyingine za Saza na Mwambani wilayani Songwe, Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Mkwajuni (MKUWASA) kwa sasa inatekeleza mpango haraka wa kuongeza upatikanaji wa maji kupitia mradi wa...
Katika wodi za uzazi, sauti za uchungu na matumaini hukutana. Wakati mwingine, dakika chache ndizo hutenganisha uhai na mauti. Ndipo upasuaji wa dharura unapokuwa tumaini la mwisho. Lakini nyuma ya kila uamuzi huo, kuna swali lisiloepukika: je, hatua hiyo imechukuliwa kwa sababu sahihi za...
Kilio cha mama kinapochanganyika na sauti ya kwanza ya mtoto, mara nyingi huleta faraja na furaha isiyoelezeka. Lakini nyuma ya pazia hilo la matumaini, kuna nyakati ambazo maisha ya mama na mtoto huning’inia kwenye uamuzi mgumu wa kitabibu; uamuzi wa kufanya upasuaji wa kujifungua ili kuyaokoa...
SAFARI ya uzazi, ambayo kwa familia nyingi hutarajiwa kuwa ya matumaini na furaha ya kumpokea mtoto imeanza kugubikwa na hofu, mashaka na maswali yasiyo na majibu katika baadhi ya hospitali nchini.
Kwa baadhi ya wazazi, chumba cha kujifungulia kimegeuka kuwa eneo la shinikizo, maamuzi ya haraka...
Licha ya kuwepo kwa sheria, kanuni na mifumo ya usimamizi wa sekta ya madini nchini, simulizi kutoka migodi ya wachimbaji wadogo mkoani Shinyanga zinaonyesha taswira tofauti usalama bado ni kitendawili kisichopata majibu.
Katikati ya hali hiyo, sauti ya mtaalamu wa jiolojia, James Kibiti Muiko...
Sauti za vilio, hofu na taharuki zimekuwa sehemu ya simulizi za wachimbaji wadogo katika maeneo ya Nyandolwa na Mwakitolyo, mkoani Shinyanga. Ni maeneo ambayo chini ya ardhi yake kuna matumaini ya dhahabu, lakini juu yake kuna wingu la vifo vinavyojirudia mara kwa mara.
Katika kipindi cha miaka...
Hofu ya Kiafya Inayozidi Kutokana na Maji Yasiyo Salama
Wakati mradi wa maji wa Shilingi bilioni 4, Kata ya Mkwajuni, Wilayani Songwe ukisubiriwa kwa hamu kubwa kuanza kufanya kazi, hofu ya kiafya inazidi kuongezeka miongoni mwa wananchi wa Kata hiyo.
Wananchi wanabainisha kuwa maji...
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.