Kwenye "examination -in-chief" upande uliomleta Shahidi, ndio umwongoza Shahidi kuelezea hoja yenye lengo la kujenga kesi au utetezi kwa upande uliomleta.
Ila kwenye Cross examination upande ambao haujamleta Shahidi uuliza maswali, kubomoa hoja zilizotolewa wakati wa "examination -in - chief"...
Nimefuatilia wadau wengi kwa kutojua au kwa kujitoa ufahamu wanadai, kwamba Lissu atafanya "examination- in -chief" tu na wanadhani hawezi kufanya "cross -examination" wanasahau kifungu cha 163 cha Sheria ya Ushahidi yaani " Evidence Act [Cap. 6 RE: 2019] kitampa ruhusa ya kufanya...
Mfumo wa Tausi kama ukitumika kama ilivyokusudiwa utaleta mabadiliko. Changamoto iliyopo ni ulafi na upigaji kwa waliopewa dhamana, tunarudi kulekule mabwana ardhi kujimilimbikia viwanja.
Ukiona kiwanja kipo eneo zuri na bei yake ipo chini jua kabisa wanachukua wao, lakini pia ukiona eneo...
Binafsi nimeliona hilo mara kadhaa, hata mimi pia niliingia kwenye mfumo dakika tano kabla ya mauzo lakini ulipofika muda wa mauzo mtandao ukagoma.
Hali hii utokea kwenye viwanja ambavyo watu wanakuwa wanamipango yao tayari, kuthibitisha hilo viwanja hivyo vizuri bei ya uwa inakuwa chini sana...
Binafsi ni mdau wa makazi yaliyopangwa na kupewa matumizi kulingana na mpango wa eneo husika.
Kifupi uwa ninahisi kero kupita sehemu ambazo zina ujenzi holela, kwa mantiki hiyo nimekuwa nashawishika kununua maeneo yaliyopimwa. Nilifanikiwa kununua eneo Dodoma (mtumba) na kufanya malipo...
Kelele zinazalishwa na makanisa ya Walokole na shughuli nyingine za kijamii kutokana na usimamizi mbovu wa taasisi za serikali zilizopewa jukumu la kuzuia kadhia hiyo. Walokole na watu mbalimbali wamekuwa wakipiga/kuzalisha kelele kwakuwa wenye mamlaka ya kuzuia hawajui majukumu yao kabisa...
Mfumo wa ununuzi wa viwanja wa Tausi.Tamisemi naamini una changamoto inayosababishwa na watendaji wake. Kwenye mfumo huu viwanja vizuri vinawekwa kiushaidi tu lakini watu wanakuwa wameshajitwalia mapema.
Ukitaka kuamini jaribu kufuatilia matangazo ya viwanja kwenye maeneo mazuri, wanaweza...
Mfumo wa Tausi, Tamisemi ulipozinduliwa nilifurahi sana maana nilijua utatatua changamoto nyingi ikiwemo ununuzi wa viwanja kwa njia ya kielektroniki
Ununuzi wa viwanja umekuwa tangu zamani umekuwa na changamoto nyingi, ikiwemo upotevu wa fedha kutokana na utapeli. Mfumo wa Tausi...
Binafsi ninaamini kuna nguvu kubwa inayotufanya tuwepo Dunia. Ila siamini dini hizi za kidunia ambazo kila kukicha ni malumbano ya juu ya ipi ni bora kuliko nyingine hadi mara nyingine kuleta machafuko.
Dini hizi mbili zimezifunga akili za watawaliwa hususani Nchi za Kiafrika na kuleta mpasuko...
Binafsi ninaamini kuna nguvu inayoendesha dunia tusiyoiona kwa macho ila napinga dini moja kujiona ina haki dhidi ya nyingine hapa naongelea dini hizi za kuletewa ( Uislam = Muarabu na Ukristo= Mrumi).Dini zote ukisoma maandiko ( Biblia na Quran) zina mapungufu.
Mfano mdogo agano la kale...
Kelele za sauti kutoka kwenye mabaa na makanisa hususani ya walokole ni kero kwa wengi si wewe tu. Ila mamlaka husika wanaona na kufumbia macho.
Wanasubiri litokee jambo la uvunjifu wa amani ndio wajitokeze wakijibaraghuza kutaka kuchukua hatua, lakini kwa hali inavyoenda ipo siku balaa kubwa...
Huu mradi ulianza kufa kabla hata ya kuanza kwasababu ya wakubwa kukosa maono. Kwanza eneo walilolichagua kama karakana ilitosha kueleza mradi ungekufa tu mapema punde tu baaada ya kuanza. Serikali siku zote usema tusijenge mabondeni ila ajabu karakana ikajengwa Jagwani sehemu ambayo uathiriwa...
Hao wabunge 19, hawaikomoi chadema hizo hekaheka zao zipo katika kulinda maslahi ya matumbo yao tu. Halima na wenzie wanajua kuwa wakipoteza sifa ya kuwa wanachama basi na ubunge wao utafika kikomo.
Kama ulivyosema hawa hawana mapenzi ya dhati na chama, ila naongezea kuwa wanahangaika kulinda...
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.