Mkuu mi naona mengi ya uliyoandika ni kinyume cha uhalisia. Sisi wanyonge tunaona ni wakati wetu kutesa hasa tunapotenda kama inavyotakiwa. Zamani watu hawa (wakubwa) walijiona miunguwatu leo tunasikia Hosea naye kimenuka!!!!!!!!!!!!!!
Hongera ACT-Wazalendo, ni chama nitakachokwenda ikiniudhi serikali ya CCM maana kwa sasa sina chama baada ya babu kutia maguu chadema. Namkubali sana Magufuli mpaka sasa, nawaomba tumwombee wana jukwaa.
Ndugu si kweli Magufuli ni dictator ila anasimamia zaidi sheria kuliko ilivyokuwa mwanzo tatizo ni sisi bush lawyers tunakurupuka sana maana kabla hatujajua undani wa jambo tunakuja huku kusema/kulalamika. Hata hivyo maendeleo yanakuja kwa chembechembe za dictatorshihip angalia USA-Roosevelt...
Maoni ya wachangiaji wote kabla yangu yako sahihi kama wamejiridhisha kwa usahihi kabisa na mazingira na sababu ya mheshimiwa kuwekwa ndani tusije tukatoa emotions zetu hapa bila uchunguzi wa kina na kumbe siyo sahihi.
Jamhuri ni gazeti linaloisakama sana serikali iliyopo na iliyopita. Mi sipingi kufanya hivyo maana wanatuhabarisha ila nawaombeeni mnijulishe wadau, nani mmiliki wa gazeti hili????????????? Nadhani hii ndo iliyompelelekea mkuu wa kaya kutoa majibu ya hovyo hovyo kwa mwandishi wake.
Ni sahihi kumzuia kama kuna ishu ya msingi lakini hii ni ya KITOTO sijawahi kuona. Kwani mkuu wa wilaya kuipigia kampeni CCM ni kukosa sifa za kuwa mkuu wa wilaya? Hatujui kuwa vyeo hivi vina chembe nyingi sana ya chama tawala???? Nawaombeni sana Watanzania wenzangu; kama kuna kitu kitaturudisha...
Haingii huko yeye ni mwanasiasa na mbunge tu. Majukumu yake ni kuwasemea wananchi na wala si kuwajibisha viongozi. Hawezi kumtaka DED na hapa nadhani tujue mipaka ya kazi kati ya mihimili mitatu ya nchi i.e. mahakama, bunge na serikali.
Hii ni tabia yetu binadamu kumhukumu mtu kwa kosa moja na kufuta mazuri yake yote. Tumeanzia baraza la mawaziri na majibu wakati wa maswali ya waandishi. Hii inaonesha wengi wetu hatumfaham huyu jamaa. Mimi nafuatilia sana utendaji wake. Jamaa yuko vizuri na tusubiri mtaniambia kama hatawagusa...
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.