UMELIA KWA BIDII NA WELEDI MKUBWA?
Jikaze kiume!
Wanaume hawalii!!
Usilielie kama mwanamke!! Na kauli nyingine nyingi zinazoendana na hizo kimekuwa ni kitu cha kawaida sana katika mazingira tunayoishi.
Na halafu? Unalazimishwa kukinzana na mfumo wa maumbile! Unajikuta unakubali kujikaza...
Ni sahihi. Unajua hata wanaotudai mara nyingi sana tunajikuta tunawakwaza kwa mienendo na matendo yetu. Mtu anakudai halafu unaleta njia za kupinda pinda. Nikijuacho, ikiwa unadaiwa, unapaswa kunyoosha sana maneno na matendo yako. Deni halifungi.
Ingawa wengi kati ya hawa wanaouza tumewaona wakiwa na majuto baada ya muda. Hawajuti kwa kuwa waliziuza, wengi wanajuta kwa kuwa waliziuza bila kufikiri sawasawa, au waliziuza kutokana na migogoro, na zaidi sana, baada tu ya kuziuza, hawakufanya maamuzi wachukue hatua inayofuata.
Naam. Na hapo kuna cha kujiuliza. Fikiri thamani ya nyumba pale kariakoo. Mtu anaiuza kwa kuwa na shida, na unakuta anapewa thamani ambayo hata kununua kiwanja Vigwaza au Chanika hawezi. Anapata pesa ambayo hata akiamua kurudi kijijini hawezi kujenga kibanda cha kujisitiri na kuanzisha mradi...
Bila shaka mkuu. Soma andiko langu nimetoa uzoefu hapo juu. Niliuza kiwanja mwaka 2014, eneo ambalo mpaka sasa imekuwa ni sehemu ya majuto makubwa na maumivu yasiyoisha moyoni. Nilipata shida ya kuuguza na kimbilio likawa kuuza eneo. Sitasahau kabisa!!
Mtu anauza jokofu lenye thamani ya laki tano kwa shilingi laki tatu na nusu ili alipe deni la shilingi laki tatu. Elfu hamsini inayobaki anaenda kujipooza moyo kwa kula nyama choma na bia baridi. Kumbe angetuliza kichwa kidogo tu, angeomba muda kidogo wa kujipanga, akaanzisha mradi rahisi wa...
Hili umeliweka vizuri sana. Nitaandika kwa kirefu katika thread nyingine juu ya maamuzi ya kukopa katika taasisi za pesa.
Hakuna sehemu nimeshauri mtu asiuze asset. Umeeleza vizuri sehemu kuwa, kimfaacho mtu chake. Inapotokea umefanyaa tathmini ya kina juu ya kuuza amali yako, ni wazi kuwa...
Sahihi. Na kuwa kuwa kimfaacho mtu chake, si vema kikimletea majuto yanayoweza kuepukika. Tunanunua amali ili zitufae. Sihamasishi mtu mwenye amali yake asiiuze, kuna nyakati tunazinunua ili baadae tuziuze maisha yaendelee. Swali kuu hapa ni, JE, Unauza amali yako wakati gani na kwenye mazingira...
Uko sahihi.. Na hapa ndio tatizo kubwa lilipo. Shida mara zote inakufumba macho, masikio na zaidi sana, AKILI. Mwenye shida yuko tayari kuuza utu na thamani yake, sio tu amali. Biblia inatukumbusha kuwa, Esau aliuza haki yake ya mzaliwa wa kwanza kisa dengu tu... Njaa ilikuwa inakaribia kumuua...
Kuwa nao makini sana mkuu... Nimewahi kuona mtu anauza shamba milioni kumi na mbili wakati kwake zinafika tatu tu. Dalali kaweka kilemba cha maana juu, na mwenye mali hajui
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.