Recent content by News Tz1

  1. N

    JamiiForums Tanzania Dkt. Mashingo: Hakiki taarifa za Afya ya Uzazi unazoziona mtandaoni kabla ya kuziamini

    Dkt. Mashingo Lerise kutoka Marie Stopes Tanzania (MSI) ametoa wito kwa jamii, hususan vijana, kuwa makini na taarifa za afya ya uzazi wanazokutana nazo kwenye mitandao ya kijamii. Amesisitiza umuhimu wa kuhakiki taarifa hizo kabla ya kuziamini ili kuepuka taarifa zinazopotosha na zisizo na...
  2. N

    JamiiForums Tanzania Prof. Godius Kahyarara : Usimamizi mzuri wa usafiri wa majini una nafasi katika kukuza shughuli za biashara

    Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi, Prof. Godius Kahyarara, ameielekeza Mamlaka ya Usafiri wa Majini na Nchi Kavu (TASAC) kuhakikisha inatekeleza kwa ufanisi majukumu yake ya kusimamia na kudhibiti sekta ya usafirishaji, ili kuchangia zaidi katika maendeleo ya kilimo, uvuvi na ukuaji wa uchumi wa...
  3. N

    JamiiForums Tanzania Serikali kuanza ujenzi wa kiwanda cha mbolea hai kwa ajili ya kilimo cha pamba

    Dodoma: Serikali inatarajiwa kuanza ujenzi wa kiwanda cha mbolea hai katika Kijiji cha Nyamatara, Misungwi, Mkoa wa Mwanza, kwa lengo la kuongeza upatikanaji wa mbolea kwa wakulima wa pamba na hivyo kuongeza tija katika uzalishaji wa zao hilo. Hayo yameelezwa na Mhandisi Mkuu wa Bodi ya Pamba...
  4. N

    JamiiForums Tanzania Rais Samia: Ongezeni mabasi ya Mwendokasi, kuna mabasi yapo hayana kazi

    Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan, ameziagiza mamla zinazohusika na uratibu wa mabasi hayo, kuhakikisha zinaongeza idadi ya mabasi katika maeneo ambayo yanauhitaji mkubwa. Ametoa agizo hilo Agosti 7, 2026 katika hafla ya kufungua na kutembelea mradi wa mabasi...
  5. N

    JamiiForums Tanzania BMT yataja fursa 12 AFCON 2027, Wananchi na wadau wahimizwa kujiandaa mapema

    Baraza la Michezo la Taifa (BMT) limetangaza fursa 12 zitakazotokana na Tanzania kuwa mwenyeji mwenza wa Mashindano ya Mataifa ya Afrika AFCON 2027 ambazo zitafungua zaidi milango ya maendeleo ya uchumi, ajira, biashara, utalii na uwekezaji nchini. Akizungumza kuhusu fursa hizo, Mkuu wa...
  6. N

    JamiiForums Tanzania THRDC: Wahadhiri wawili wa St. John wameshikiliwa muda mrefu, waachiwe au wapelekwe Mahakamani

    Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (THRDC) umeeleza wasiwasi wake kuhusu kukamatwa kwa wahadhiri watatu wa vyuo vikuu, huku mmoja wao akifunguliwa kesi ya ugaidi na wengine wawili wakiendelea kushikiliwa bila maelezo. Umesema hali hiyo inaweza kuwa na athari kwa taaluma na kuathiri...
  7. N

    JamiiForums Tanzania Prof. Mkenda: Wiki ya Taifa ya Elimu, Ujuzi na Ubunifu 2026 Kufanyika Tanga Agosti 15 hadi 24

    Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. Adolf Mkenda, amesema Serikali imeendelea kuwawezesha wabunifu wanaoibuka kwa kuwawekea mazingira rafiki, ikiwemo kuwapatia rasilimali fedha ili kukuza bunifu zao. Prof. Mkenda amesema hayo wakati akitangaza kuwa Maadhimisho ya Wiki ya Taifa ya...
  8. N

    JamiiForums Tanzania Makamu wa Rais Dkt. Nchimbi mgeni rasmi kwenye mkutano wa watetezi wa haki za binadamu leo Julai 24, 2026

    Makamu wa Rais Dkt. Emmanuel Nchimbi anatarajiwa kuwa Mgeni rasmi kwenye mkutano wa watetezi wa haki za binadamu ambao ni wanachama wa Mtandao wa watetezi wa haki za binadamu Tanzania (THRDC). Fuatilia https://www.youtube.com/live/PAgUqKix-FA?si=qmd6adR9dT-sOgUH
  9. N

    JamiiForums Tanzania Olengurumwa: Watoto wanaopelekwa mijini kuuza mayai na kazi nyingine wananyimwa Haki ya Elimu

    Mratibu wa Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (THRDC), Wakili Onesmo Olengurumwa, amechangia hoja iliyoibuliwa na mdau katika jukwaa la JamiiForums.com kuhusu wimbi la watoto wadogo kutolewa vijijini na kupelekwa mijini kwa ajili ya kufanyishwa kazi, ikiwemo kuuza mayai mitaani...
  10. N

    JamiiForums Tanzania LHRC: Kuna idadi kubwa ya watu wanaoendelea kukamatwa na kushikiliwa katika vituo vya Polisi bila dhamana au kupelekwa Mahakamani

    Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC) kimelaani vikali hali ya kuendelea kushikiliwa kwa wananchi mbalimbali katika vituo vya Polisi nchini kwa muda mrefu bila kupatiwa dhamana au kufikishwa Mahakamani, licha ya baadhi yao kukabiliwa na tuhuma zinazoruhusu dhamana kwa mujibu wa sheria...
  11. N

    JamiiForums Tanzania Stephen Wasira: Tuache kwanza CHADEMA waridhiane na Mahakama, huwezi kutulazimisha kuachia mtu ambae kesi yake inaendelea

    "Sio lazima CHADEMA wakisema tunakubali, tutakubali mambo ya CHADEMA ambayo yana make sense...kwa sababu huwezi kutulazimisha kuachia mtu ambae kesi yake inaendelea .tena yeye Tundu Lissu rafiki yangu..anajitetea mwenyewe, kila siku anaweka mapingamizi.."-Makamu Mwenyekiti wa CCM Tanzania Bara...
  12. N

    JamiiForums Tanzania Lissu afikishwa mahakamani leo, ulinzi waimarishwa

    Mwenyekiti wa CHADEMA, Tundu Lissu, leo Julai 20, 2026 amefikishwa katika Mahakama Kuu ya Tanzania, Masjala Kuu ya Dodoma kwa ajili ya kesi ya kikatiba inayohusu haki za Mawakili kupata faragha wanapokutana na Wateja wao waliopo gerezani. Shauri hilo limefunguliwa na Mawakili Kulwa William...
  13. N

    JamiiForums Tanzania Zaidi ya Trilion 6 kutumika kujenga kipande cha SGR Tabora hadi Kigoma

    Serikali imeeleza kuwa imepanga kutumia zaidi ya shilingi trilioni sita kujenga kipande cha sita cha Reli ya Kisasa (SGR) kutoka Tabora hadi Kigoma. Akizungumza katika Kipindi cha Jambo Wikendi cha TBC 1, Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Reli Tanzania (TRC), Mhandisi Machibya Masanja, amesema...
  14. N

    JamiiForums Tanzania Balozi Mulamula apokea Tuzo ya Uongozi Bora wa Bodi ya Wadhamini ya Benjamin Mkapa Foundation

    Shangwe na makofi vilitawala ukumbi wa Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Julius Nyerere (JNICC), Dar es Salaam, pale jina la Balozi Liberata Mulamula lilipotajwa kupokea Tuzo ya Uongozi Bora wa Bodi ya Wadhamini ya Taasisi ya Benjamin Mkapa. Ilikuwa ni heshima iliyotambua uongozi wake...
  15. N

    JamiiForums Tanzania MiryMary Travel & Tour yafungua ofisi Mbezi Beach, yajidhatiti kulinda siri za wateja

    Mkurugenzi Mtendaji wa MiryMary Travel & Tour, Miriam Chikoti, amesema kampuni hiyo imefungua ofisi mpya zilizopo Mbezi Beach kwa Zena, katika jengo la J Four Plaza, kwa lengo la kuwasogezea huduma wananchi na kupunguza usumbufu unaotokana na kupata huduma za usafiri na utalii...
Back
Top Bottom