Wewe jamaa nimekufuatilia nimegundua kuwa unafaidika na huu mfumo uliopo na si vinginevyo. Kwa kilichotokea na kinachoendelea sidhani kama mtu Mwenye akili kama zako atakuwa hafaidiki kutoka kwa wenye mamlaka. Maslahi huleta upofu!! Niishie tu hapo.
Yule mama hashauriki na hajutii kilichotokea. Angalia gesture yake utagundua kuwa alitamani afanye zaidi ya pale (mauaji). Bahati mbaya amezungukwa na Watu wanaompoteza mno kiushauri.
Kwa Sheria ipi inayosema kuwa kuna wamiliki wa mji Tanzania. Acha mihemuko kijana hii nchi ni yetu sote, Mimi natokea Tanga naishi Arusha na hata huko nitokako kuna wamasai tena maelfu kwa maelfu lakini hatujawahi kuwabagua. Sasa hoja yako Haina mashiko zaidi ya hisia potofu za utenganifu.
Ili wafanyeje? Watu wanapigania haki na Sheria sio vurugu, sasa wewe kwa muonekano wa hoja yako ni kwamba unataka wajitokeze watu Ili wapambane nao, hilo halikubaliki maana ni uvunjufu wa Sheria zaidi.
Mimi ni Gen z ndugu yangu na hii mada Haina uhusiano na kilichotokea October 29. Kikubwa ni kwamba kila nchi hii ni yetu sote hakuna Mwenye haki zaidi ya Mwingine. Hawa vijana wa kimasai wanadhani hii Arusha ni Mali Yao ndio maana wanakuwa wakorofi
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.