Recent content by murielle

  1. murielle

    Padre aliyeongoza misa kumuaga Jenista Muhagama asikitika 'nilijiuliza ni kwanini kifo chake kitokee wakati huu?'

    Sijui lengo la mtumishi ni nini lakini kwenye suala la kifo hakuna foleni ya umri au hadhi. Sote tutaondoka pale ambapo Mungu aliyetupa pumzi atakaposema imetosha. Ndio maana wapo wanaokufa wakiwa na masaa tu duniani. Kujiuliza kwanini aondoke wakati huu kunaleta maswali ambayo hakuna majibu...
  2. murielle

    PostGE2025 Vijana waendelea kumbana waziri Nanauka: Viongozi mnatumia gari za gharama, nimeangalia gari lako sio chini ya Milioni 500

    Ila viongozi nao wajitathmini,wakati mwingine paki hilo gari sehemu nenda na usafiri wa kawaida kwenye baadhi ya maeneo yanayofikika. Uwaziri si gari. Unaenda sehemu attention inakuwa si hata kwako na kilichokuleta bali gari.
  3. murielle

    PostGE2025 Mshaurini Wanu ajiuzulu angalau kupoza kipengele hicho

    Watu mnashangaza kweli kuamini yeye aliyemuweka hakujua litamletea shida. Mnaamini baada ya haya yote ana watu wengi sana katika wachache wenye vigezo vya kuteuliwa anaowaamini kuwa sehemu ya Baraza la mawaziri? Kuna anayoyajua ambayo wengi pengine hatujui na mkakati wake ni kuwaweka alikowaweka...
  4. murielle

    Kwa hiyo Mwigulu kukutana na Kitima mkajadili muanze na kufungua kanisa la ufufuo? Mwamtega jasusi la mbinguni sio

    Nimewaza sana hii move,nikakumbuka post yako ya juzi kuhusu Gwajima,akili ikasema huu mtego umesukwa kwa akili sana. Mbele ya umma hawana shida nae,nyuma ya pazia ni salama? Yuko salama au Kanisa ndio liko salama? Kazi ipo.
  5. murielle

    PostGE2025 Msigwa: Vyombo vya nje vifuate taratibu za uandishi, walichofanya CNN, Al Jazeera na wengine sio sawa, ni ukiukwaji wa makusudi

    Waligundulika kuwa ni watu wa nje wakiwa tayari wanaandamana? Au tuulize walihojiwa kabla ya kuuawa wakiwa katikati ya maandamano au walihoji maiti zao? Watulie tu
  6. murielle

    PostGE2025 Msigwa: Vyombo vya nje vifuate taratibu za uandishi, walichofanya CNN, Al Jazeera na wengine sio sawa, ni ukiukwaji wa makusudi

    Upande wa pili wa video zinazoonyesha watu wakiuawa ni upi? Kwamba maandamano yalikuwa ya amani?
  7. murielle

    PostGE2025 Serikali ikikanusha ripoti ya CNN, litaangushwa bomu jingine Dunia isimame! Je, Msigwa atasema nini leo?

    Tatizo si tu idadi ya waliouawa bila sababu ya msingi maana hawakuwa na silaha na kulikuwa na option ya kuwatawanya,na kuwakamata,tatizo kubwa ni hatua walizozichukua baada ya kuua. Linaonyesha haya mauaji yalipangwa na waliotekeleza walijiandaa hadi namna ya kuficha ushahidi. Katika kitu CNN...
  8. murielle

    PostGE2025 Samia alikuwa na uwezo wa kujenga kukubalika baada tu ya kuwa rais na angeweza kuwashinda upinzani lakini uwezo mdogo umempeleka pabaya

    Nahisi alibadili washauri akaamini sana waliomsifia ili wale keki ya taifa kupitia yeye na sio wenye uwezo wa kumshauri kwa maslahi mapana nchi na ya legacy yake. Wajanja wakamuweka busy maskini kupambana na legacy ya mtangulizi pamoja na pressure ya kuwa mwanamke kwenye hiyo nafasi. Ninaamini...
  9. murielle

    Mange anadai tar 29/10 askari na wanajeshi wengi walikufa

    Kazi ipo. Nachoamini tu kuna watakaotaka kuwa upande wa wanachi hiyo tarehe 09/12 kujisafisha au kusafisha viongozi wao na yale ya 29/10. Ni ngumu kuwa huru kufanya yaliyofanywa tarehe 29/10 baada ya documentary ya jana na zile video za yaliyotokea,possibility ya kushitakiwa ICC na mengine kama...
  10. murielle

    Anguko la ushawishi na uamuzi wa vijana wa Kitanzania (Gen Z)

    Kuna tofauti ndogo kati ya Gen Z na wengine kwa mtazamo wangu. Wenye kuishi duniani sasa wana access na taarifa nyingi sana na watu wa aina hii huwezi kuwatawala kwa mbinu za kizamani zilizoamini viongozi ni wamiliki wa ukweli, haki na hatma za wananchi kwasababu na wao wana taarifa kwamba...
  11. murielle

    CCM nadhani sasa ile hoja yenu ya CHAMA KWANZA TAIFA BAADAYE mnaiona inavyowatafuna, msilalamike chini chini maana mliaminishana mnaikomoa CHADEMA

    CCM ni taasisi. Maamuzi yangekuwa yanafanyika kuanzia kwenye mashina huko hadi Taifa ingekuwa rahisi kusema wana CCM wengi muelekeo wao unaufahamu. Kwa mfumo wa maelekezo kutoka juu kuja chini unaweza kuwa unawazungumzia kama vile wako milioni 30, kumbe wenye maamuzi hawazidi 10. Tuna mengi...
  12. murielle

    Muke ya Muzungu ndio anatuambia cha kufanya

    Ukitaka kuishi maisha yenye manufaa sikiliza anachosema mtu na sio kuangalia ni nani. Hata mjinga anaweza kuwa na ujumbe muhimu. Hata akili yake ingekuwa mbovu akili za mamilioni wanaomsikiliza combined haziwezi kuwa mbovu kwa pamoja. Sikilizeni hata msiokubaliana nao.
  13. murielle

    CNN na Larry wasema Wana Mamia ya Video na Audio walizozichunguza Kwa Teknolojia.Sasa Gerson Msigwa Njoo na Tamko lako CNN iziachilie zote

    Hili ni gumu sana kulifanya siri. Mnyororo wa watu waliohusika ni mrefu sana. Walioua,waliofiwa,waliopokea maiti na majeruhi,waliokuwepo mahospitalini madaktari,manesi,wafamasia,watunza miili,wafanya usafi,wapishi,walinzi,watafuta miili,wapakia miili,washusha miili,wachimba...
  14. murielle

    Watatusaidia China, Urusi na Waarabu. Nyie Mabeberu msitutishe

    Wakijidanganya hivi tumekwisha. Unaweza waza watakusaidia kumbe wanataka yavurugike wauze silaha zao na muingie mikataba mibovu kwasababu mtakuwa desperate. Matajiri wa dunia hii wanawaza fursa na vizazi vyao mika 100 ijayo. Libya iko wapi? Shamba la bibi. Mungu aepushe aina hii ya mawazo kwa...
  15. murielle

    PostGE2025 Kosa vyote sio akili. Mara walitoka nje ya Nchi, ikaja walifuata mkumbo sasa hivi eti walilipwa

    Nimerudia kuiangalia mara tatu hicho kipengele,alikuwa ana notebook yake mwenyewe anasoma na sio hotuba rasmi. Nimeamini kiongozi ni muhimu ukazungukwa na watu wenye hekima na busara sio tu akili,urafiki,elimu na ukada. Competence ni muhimu sana.
Back
Top Bottom