Ningefurahi sana kusikia Sumaye amesema nini juu ya misaada na masharti yake. Nilidhani hii ingekuwa mada nzito ikigusa yanayoendelea kwa jirani zetu Uganda.
Hayo ya elimu ya Sumaye hata sioni yana uhusiano gani na mada hii.
Mimi natamani maamuzi yooote ya bunge letu yawe ya mfumo wa kura za wazi. Ili tusiendelee kuwa na 'collective responsibility'. Zikipitishwa sheria za kipuuzi basi kila mwananchi ajue nini mchango na msimamo wa mbunge wake katika sheria husika.
Nikiangalia hii nyomi iliyoandamana naye napata picha namna ambavyo Magufuli anajua kucheza na akili za watanzania. Kuna ile nyingine aliamua kupanda kwenye lile bulldozer kabisa, sijui na yeye ni dereva au pozi tu za picha..
Kitila ni msomi katika sekta ya elimu. Hii ni changamoto kwake pia ukizingatia anatoka Singida. Sio kila siku kuichambua CHADEMA mara sijui imefura mara imesinyaa!
Uchambuzi wako umeegemea kwenye umahiri wa kujibu maswali, nakubali hilo ni la msingi kwa mwanasiasa yeyote.
Rais amesema ukweli, he was very honest and not ambitious to impress, hilo huwa ni adimu sana kwa wanasiasa.
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.