Ni kweli ocd Yuko chibi ya hao uliowataja. Lakini nadhani kama atazuia hiyo mikutano ya vyama vya siasa kwa kufuata maagizo kinyume na sheria anaweza kushitakiwa kama eye.
Sitegemei majibu au mtazamo wa Mama kuhusu hiyo kesi ya akina Mbowe uwe tofauti na maelezo ya Polisi, kwani wao ndio wanampa taarifa hizo. Lakini kama nakumbuka vizuri, huko nyuma kuna Kijana mmoja alikuwa anakabiliwa na kesi moja na baadaye alikuja kusema kuwa Polisi walikuwa wanamshinikiza...
Mimi nadhani kwa mikutano ya hadhara ya vyama vya siasa vilivyosajiliwa rasmi, hakukuwa na sababu yoyote muhimu ya kuizuia. Katiba inaruhusu, na ilitamkwa bayana baada ya Sheria ya vyama vingi vya siasa, kuwa mikutano hiyo ya hadhara inawekwa kwenye Katiba ili isiwe rahisi kwa mtu yeyote...
Wangevaa viatu vyake wangeelewa. Kwa mujibu wa maaelezo ya mdude mwenyewe, inaonekana watesi wake walidhamilia kumpa ulemavu wa kudumu kama siyo kummaliza kabisa. Simulizi yake ya aliyofanyiwa akiwa magereza kiukweli inatia hasira.
Katika nchi nyingi za Afrika kuonekana unashirikiana na upinzani ni kama adui wa watawala waliopo. Hata mawakili wanaotimiza wajibu wao kutetea watu wanaoonekana kujihusisha na upinzani huwa kama wanahatasha Kazi zao. Nadhani kwa kuliona hilo ndiyo maana Lisu kaamua kumuweka Wakili ambaye...
Hali hii unatokana na kutokuaminika kwa TUME iliyopo. Ili kuondoa hali hiyo muundo wa TUME unatakiwa uridhiwe na wadau wengi wa uchaguzi yaani kuwe na Tume ambayo kila Chama kitakuwa na Imani nayo kimuundo.
Ukiwasikiliza wananchi waliokuwapo ni kwamba kabla ya msafara wa Lisu kivuko kilikuwa kinafanya kazi bila tatizo. Mara tu ya kufika msafara huo kikaenda upande wa Pili na kusemekana kuwa ni kibovu na kwamba hakiwezi kufanya kazi tena kwa simu ya leo.
Kuhusu Corona tusiwalaumu sana CHADEMA. Wao walifuata ushauri wa wataalamu wa afya kuwa unatakiwa ujilockdown kwa wiki mbili kama utaona kuna dalili za ugonjwa huo. Kwa kipindi hicho huko Bungeni kuna wabunge wetu walifariki na haikuwekwa wazi chanzo cha hivyo vifo. Hiyo ilikuwa ni kuchukua...
Hivi karibuni nilisoma mahali kuwa kuna mgombea mmoja wa udiwani, sikumbuki Chama lakini ni cha upinzani, kajitoa katika zoezi hili. Lakini sikusikia Chama chake kikishirikishwa katika uamuzi huo.
Huo ndiyo ukweli. Katika mfumo tuliokuwa nao tume ya uchaguzi ambao unahusisha vyama mbalimbali wajumbe wake hawatakiwi kuteuliwa na mtu ambaye kuna muda naye au Chama chake wanatakiwa wasimamiwe na tume hiyo hiyo tena.
Ingekuwa unafanyika uchaguzi wa Mbunge tu maneno hayo yangeweza kueleweka. Huu ni uchaguzi mkuu ukijumuisha rais na madiwani. Mgombea wa urais yeyote asijipe uhakika wa moja kwa moja kushinda.
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.