Mkuu hiyo ya kwanza hapo juu, SOHK 'school of hard knocks nilikuwa na T Shirt yake ya Kijivu ina picha ya yule katuni amevaa kofia. Nyumbani wakawa hawaipendi ikabidi niifumue ile pacha ya katuni mana ilikuwa kubwa sana.
Daaaa!!!! C programming unanikumbusha mbali kidogo, hivyo viwalo vinanikumbusha miaka 1991-1994 nikiwa nasoma bweni Moshi nikitokea Dar es Salaam. Kwa wale wa kuelekea pande hizo za kaskazini kituo chetu cha mabasi kilikuwa pale Kisutu, ndinga ilikuwa kuondoka saa kuanzia saa 10 jioni [hakuna...
Mrembo Zabibu anapatikana kwenye kitabu cha NJAMA wengi waliosoma vitabu hivi walivisoma miaka ya 80 -90,
mimi nilikisoma NJAMA mwaka 1989 kama sijakosea
Edmund post yako ni nzuri, mimi mwaka juzi nilishawishika kufanya hicho kilimo lakini eneo lenyewe halikuwa na mto, nilichimba kisima kirefu (bore hole) nikiamini umeme ungefika mapema lakini hadi leo ni bila bila
Ndugu ELNIN0 hongera sana kwa biashara yako ya ufugaji wa kuku, mimi ndio nimeanza maandalizi kwa ajili ya ufugaji wa kuku, nimeweka uzio wa seng'enge kuzunguka eneo la nyumba, nimejenga mabanda mawili, moja ni futi 26x13 jingine ni futi 10x15, nimechimba kisima kirefu cha maji, pia natarajia...
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.