Wakiwa wao ni wamiliki, hapo hakuna riba ila kama na wao wananunua ndio wakupe ulipe kidogo kidogo hapo ndio riba inapatikana. Asante ngoja niwafuatilie nitaleta mrejesho.
Kutokua na pesa ni kwa kipimo gani? Kwa mfano kati ya watoto watano nilionao wanne wameanza shule na hakuna hata mmoja anaesoma st. kayumba. Kwa ufupi hela ya kukidhi mahitaji ya familia inapatikana lakini kupiga hatua kadhaa mbele ndio tunazifosi.
Vipi kama ikawa ni used tayari kwenye good condition halafu ikawa mkataba wa miaka mitatu nayo itakua utapeli? Au umeamua kuchagua upande wa kusapoti pointi yako.
Jina la dhamana linasoma jina la mkopeshwaji, nyumba ya zamani kidogo, ya vyumba vitatu, subule, dining, jiko na choo ndani. Uwanja ni karibu heka moja kasoro ambayo yote imezungushiwa fensi.
Nina ishi maisha ya kipato cha kati lakini malengo ni mengi na umri unasonga. Kuhusu kuwalea biashara inajitosheleza ila kuwatengenezea kesho yao ndio nnaipambania.
Mko
Mkopo wa benk za kiislamu haujatimiza masharti ya mkopo wa kiislamu. Kwa sababu mkopeshaji sio mwenye kumiliki mali anayoikopesha. Kwahiyo zile ni riba zilizojificha kwenye kichaka cha faida.
Alhamdulillah mi ni Sallafy. Lakini suala la kuzaa mpaka biblia imesisitiza “Mungu akawabariki, Mungu akawaambia: Zaeni, mkaongezeke, mkaijaze nchi, na kuitiisha…"
Habari zenu wanajamvi?
Mimi ni Mpambanaji(Muhitimu wa chuo kikuu UDSM) nilimaliza pale 2015. Nina miaka 35, nna familia ya mke na watoto watano. Kwa sasa niko Kilimanjaro.
Katika harakati nyingi nilizofanya (kilimo, ufugaji na graphics na web design) nilibahatika kununua gari aina ya toyota...
Kuna mtu kwenye uzi mmoja alikua anaomba ushauri kuhusu mradi wa kuku.
Nilimpa ushauri huu ambao nimeona niupost hapa huenda wanaofuatilia uzi huu wakapata kitu kidogo cha kujifunza.
👇👇👇
Mwaka 2019 nilikua nna wazo kama lako, na ni mawazo ya wafugaji wengi sana. Tofauti yangu na wewe ni idadi ya...
Mwaka 2019 nilikua nna wazo kama lako, na ni mawazo ya wafugaji wengi sana. Tofauti yangu na wewe ni idadi ya mifugo mi nilitamani nifikishe 1000 ndani ya mwaka mmoja we unahitaji kufikisha 5000 ndani ya mwaka na nusu.
Nilianza vizuri japo sikufikia malengo na nnaendelea kufuga mpaka leo lakini...
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.