Kenya ina viwanda vingi vinavyozalisha bidhaa kuliko Tanzania. Viwanda vingi vya Kenya vinaongeza thamani ya mazao na bidha zao kwahiyo pato lao la Taifa wakiuza ndani na wakipeleka nje wanapata bei nzuri zaidi ya Tz. Tanzania inauza mazao mengi yakiwa hayajaongezwa thamani ( raw materials) bei...
Tuna uhakika gani kuwa mwanafunzi alienda kuiba simu au mwalimu alimdhulumu na kumfanyia kitu mbaya alafu akampatia kipigo cha mbwa mwizi? Marehemu hawezi kujitetea!
Ile vita ya Kagera ilikuwa inatumia dola nyingi sana za kimarekani kwa siku? Kumbuka Tz ilikuwa haitengenezi silaha nyingi za kivita, vyote hivyo vilinunuliwa kwa pesa za Kigeni . Naona wachumi wengi hawajadadavua kwa kina athari ya ile vita kwa uchumi wa Tz. ambao uliporomoka sana baada...
1) Mambo ambayo yapo kwenye vyombo vya sheria Padre makini hawezi kusema chochote. (2) Watu tunaruhusiwa kuwa na mitazamo tofauti, lakini pale ambapo kuna maonezi au kasoro za wazi wazi - Binadamu anatarajiwa kuonyesha huruma,upendo na kupiga kelele ili kasoro hizo ziondolewe. Hapo hakuna...
Mwenye dhamana na macho mengi amemuhamisha wizara, wewe unalilia angebaki pale pale. Siku zote ukitumia ubabe kusuluhisha migogoro lazima matatizo zaidi yataibuka. Acha mwingine achukue nafasi. Tz ina watu wengi wenye uwezo wa kuendesha hiyo wizara - " hakuna mteule"
Uzuri si kigezo cha kujamiana. Kigezo ni hisia za kimwili muda huo jinsia mbili tofauti zinajikuta zipo faragha. Na mara nyingi mhalifu anafanya mambo mabaya mbali na nyumbani kwake.
Kabla ya kumtuhumu mtu aliyefanyiwa kitendo cha kikatili, inabidi kuanza kumsaidia ili afunguke zaidi na kutoa taarifa zaidi. Hakuna faida ambayo mtu aliyelawitiwa anapata akijitojeza hadharani - hili ni jambo la aibu kwake ambalo ataishi nalo maisha yake yote hapa duniani. Kwahiyo kitu cha...
Wanampatia kijana umaarufu - ataandikwa kwenye magazeti, Radio na Luninga. Kama alichoma hadharani basi alikuwa anatafuta jambo! Kama alichoma akiwa peke yake - polisi waendelee kukamata wahalifu hatari.
Viongozi wengi Wa Afrika wanaogopa kuhojiwa wakiwa Madarakani. Kabla ya hapo wengi ni wazungumzaji wazuri sana! Na Waafrika wengi hiki ni kigezo tunachotumia kuwapa Uongozi.
Kuna interview zinakuwa za "bandia"- kuna kuwa na mtu ambaye amepangwa kushinda hiyo interview, Genge lenye nguvu...
Tatizo letu ni viongozi wengi kukumbatia rushwa , wizi na kukosa uzalendo thabiti kwa nchi yao. Tukipata tiba ya hayo magonjwa nchi itaendelea bila kikwazo.. Maswali au mchujo hautasaidia.
Inaelekea wewe hujawahi kuuza kitu chochote, kwa muuzaji makini bei ya kumuuzia mnunuzi inamhusu. Bei uliyopanga ni muhimu kwa kuwa ndio itakayoamua utauza vitu vingapi ( vingi au kidogo). Ukiuza vingi utapata faida kubwa . Ukiuza kidogo faida nayo itakuwa ndogo. Vile vile huwezi...
Siyo kila aliyesoma sana(digrii) ana uwezo wa kuongoza na kukubalika na watu. Wasomi wengi wanakuwa na hulka isiyo rafiki - majivuno, ujuaji, ubishi na kutokubali kushauliwa hasa na raia wa kawaida ambaye si msomi. Tulikuwa na Viongozi wenye PHD ambao walishindwa kuelewa chanjo ni nini? Mfumo...
Kwanza jiulize kwanini kuna diploma? Alafu kuna degree? Sisi waTz tumezoea kutumia vibaya raslimali zetu. Diploma ilikuwa mahususi kwa wanafunzi wenye ufaulu wa chini kwa ajili ya kada ambazo zinawasaidia Mainjinia- "teknishani". Hii kada ya "technician" huwa wanajifunza sana utendaji kwa...
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.