Poleni wote kwa msiba huu. Tuchukue tahadhali tuwapo barabarani, pikipiki kama vyombo vingine vya usafiri zimekuwa tishio kubwa miezi ya karibuni na zinasababisha vifo kwa Watanzania wengi. Pumzika kwa amani katibu.
Ni masikitiko makubwa kuendelea kupoteza maisha ya Watanzania kila siku katika ajali ambazo zinaweza kuzuilika. Usafiri wa bodaboda hasa katika jiji letu la Dar es Salaam bado ni mgeni na kwa kweli madereva wa vyombo hivi wanatia sana mashaka. Tuwe makini hasa kuwakemea pale wanapokiuka sheria...
Asante kwa taarifa hii muhimu, nasi pia tunafuatilia kupata habari zaidi. Wiki moja tu iliyopita ajali zimeua zaidi ya watu 14 Mbeya na Kahama. Hakuna muda wa kumtafuta mchawi ni nani kama sisi wenyewe wahanga wakubwa tutaendelea kubweteka, kunyosheana vidole na kungoja mabadiliko. Tuchukue...
Mwaka huu maadhimisho ya wiki ya nenda kwa usalama barabarani yataadhimishwa rasmi mkoani Iringa kuanzia tarehe 17 hadi 22 Septemba. Kauri mbiu ni "Pambana Na Ajali Za Barabarani Zingatia Sheria". Mkoani Dar es Salaam uzinduzi utafanyika katika viwanja vya Mnazi Mmoja kuanzia sa mbili asubuhi...
Mwaka 2008 asilimia 75 ya ajali za barabarani zilisababishwa na sababu za kibinadamu kama mwendo kasi, uzembe wa madereva, kuendesha ukiwa umelewa n.k , wakati hali ya barabara na ubovu wa magari ulichangia asilia 25 (Chanzo: Ripoti ya Mwaka ya Trafiki Tanzania, 2012) . Sasa tujiulize...
Taarifa hizi za ajali hasa mara tu ajali inapotokea ni za muhimu, hii inawapa tahadhari watumiaji wengine wa barabara husika, ndugu na wale wanaoweza kutoa msaada wa haraka. Ni wazi kabisa kwamba vikosi vyetu vya uokoaji vimelala na ndio maana wahanga hupata msaada masaa mawili baada ya...
Pamoja na mapungufu haya yote bado ni wazi kwamba Watanzania wengi hawana elimu ya kutosha kuweza kujikinga na ajali za kuepukika hasa vijana na watoto. Kwa kuanzia na hili vifo vingi ni vya kuepukika.
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.