Kama wewe hauna hiyo akili usione kwamba kila mtu hana, Mtaani tu watu hawana elimu lakini wanatengeneza magobole, hivi unafikiri wakipata elimu na vifaa hawataweza kutengeneza silaha nzuri zaidi?
Kilichopo ni watu kubweteka na kuridhika na walipo, Kuagiza nje utaagiza mpaka lini. Kama silaha...
Kweli kabisa, watu wanabweteka kwakua wanajua malipo yapo tu.Inabidi kubalika na kuweka mikakati ambayo itasaidia kuongeza ufanisi kwenye sekta za serikali.
Kwa dunia ya sasaivi hakuna anayeunda kitu kipya, wote wanatengeneza na kuboresha vile vilivyoko. Ninachomaanisha tuanze walau kujitengenezea wenyewe vyakwetu ili siku zijazo tupunguze utegemezi wa kununua silaha na hivyo vifaa kutoka nje. Utakuta tu hata visu, kamba n.k vinavyotumiwa jeshini...
Sidhani kama pesa inayohitajika ni kubwa kiasi hicho unachowaza, sio lazima kuanza kwa kutengeneza silaha nzitonzito.
Hivi hata mafunzo kwa wanyama, kutengeneza bunduki na drones ndogondogo inahitajika pesa kubwa kiasi hicho?.
Bado tupo nyuma sana, bado tunaendelea kuamini kua mwanajeshi ni kuvumilia mateso, na ndio maana utaona siku ya maonyesho wanajitahidi kuonyesha mazoezi magumu.
Imekuwa ni jambo la kawaida kila mara zifanyikapo sherehe za kitaifa (Sherehe za Uhuru, Muungano na Mapinduzi ya Zanzibar) kuambatana na maonyesho ya kijeshi. Maonyesho haya yamekua yakionyesha mbinu kadha wa kadha wanazotumia wanajeshi wakiwa vitani. Ni jambo la kuvutia na kusisimua sana...
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.