Eng Victor: Namshukuru Mungu kwa Ujasiri alionipa wa kujiokoa na kuokoa wengine kwenye Ndege, naelekea Muhimbili kwa matibabu zaidi

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
85,399
144,798
Eng Victor amesema baada ya Ndege ya Precision Air kuanguka alijaribu mara 3 kufungua mlango Bila mafanikio ndipo akaja Muhudumu wa Ndege na kubonyeza mahali mlango ukafunguka

Victor anasema muda wote wa Uokoaji alikuwa ameuzuia mlango kwa mkono takribani Dakika 40-60 na baada ya kuhakikisha Watu wote wametoka aliuachia mlango Ukajifunga kwa sababu ni wa hydroulic

Kabla sijauachia mlango nilimtuma mvuvi mmoja " mdogo mdogo hivi" aokoe mabegi yanayoelea ndani ya Ndege na anitafutie na begi langu lakini begi langu hakuliona

Victor anasema anajisikia maumivu ya hapa na pale na amekubaliana na madaktari wa Bukoba aende Muhimbili kwa Uchunguzi zaidi

Victor anasema Wavuvi wote walimfata na kumkumbatia baada ya zoezi la uokoaji kukamilika naye aliwaambia Nguvu walizomuona nazo kule kwenye Maji siyo zake bali ni muujiza wa Mungu.

Victor alihojiwa na Wasafi tv akiwa ndani ya Ndege ya Precision Air alirejea DSM tayari kwenda Muhimbili

Chanzo: WASAFI TV
 
Kwahio Majaliwa alipiga mlango upi kwa kasia ukafunguka?au kulikuwa na milango miwili?
Aaah kijana amekua exaggerated ila waliosaidia ni wengi mnoo kuanzia Hostess aliyefungua emergency exit, raia wa china, wavuvi waliokuja na mitumbwi all in all Majaliwa sio kama alikua better ila kitendo Cha yeye manusura kupoteza maisha sababu ya kujaribu kumuokoa Rubani nadhani ndio wanamfutia machozi nacho.

Pia serikali wamemkuza Ili kuondoa maswali ya wananchi kwenye uzembe wa kuchelewa kuokoa Ili Sasa attention iwe kwenye SHUJAA!! but ukisikiliza manusura wote utaona msaada ulitolewa na watu wengi sana na sio mtu mmoja kuokoa watu 24!!
 
Eng Victor amesema baada ya Ndege ya Precision Air kuanguka alijaribu mara 3 kufungua mlango Bila mafanikio ndipo akaja Muhudumu wa Ndege na kubonyeza mahali mlango ukafunguka

Source: WASAFI TV
Ohoooo ! Kumbe ya Shujaa Majaliwa ilikuwa ni Abracadabra !! Michongo mpaka ajalini. ??!! Sasa ahojiwe na mhudumu aliyebonyeza kitufe cha kufungulia mlango ili tuupate ukweli zaidi !! Vioja na viroja kila pande !!
 
Screenshot_20221114-175844_Twitter.jpg
 
Huenda Dunia nzima walishatushangaa wakachoka wakaona Bora watuache tubaki na upuuzi na ujinga wetu.

Kunakipindi tunageuzwa watoto wa chekechea tunafit tu, muda mwingine vipofu napo tunafit tu, viziwi napo sawa kabisa, tusiojua kusoma na kuhesabu yaani tunafit kabisa. Sasa Dunia itusaidiaje ndugu zangu..........!
 
Eng Victor amesema baada ya Ndege ya Precision Air kuanguka alijaribu mara 3 kufungua mlango Bila mafanikio ndipo akaja Muhudumu wa Ndege na kubonyeza mahali mlango ukafunguka

Victor anasema muda wote wa Uokoaji alikuwa ameuzuia mlango kwa mkono takribani Dakika 40-60 na baada ya kuhakikisha Watu wote wametoka aliuachia mlango Ukajifunga kwa sababu ni wa hydroulic

Victor anasema anajisikia maumivu ya hapa na pale na amekubaliana na madaktari wa Bukoba aende Muhimbili kwa Uchunguzi zaidi

Victor anasema Wavuvi wote walimfata na kumkumbatia baada ya zoezi la uokoaji kukamilika naye aliwaambia Nguvu walizomuona nazo kule kwenye Maji siyo zake bali ni muujiza wa Mungu.

Victor alihojiwa na Wasafi tv akiwa ndani ya Ndege ya Precision Air alirejea DSM tayari kwenda Muhimbili

Source: WASAFI TV
Bwashe huu uzi una kila dalili ya uchochezi. Wenye Majaliwa wao unataka kuwaambia nini?
 
Back
Top Bottom