Papa: Unyanyasaji wa kingono Ufaransa aibu kwa Kanisa

Miss Zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
4,499
9,279
Kiongozi wa Kanisa Katoliki duniani, Papa Francis ameelezea aibu iliyolikumba kanisa hilo pamoja na yeye mwenyewe kutokana na kiwango cha unyanyasaji wa kingono dhidi ya watoto uliofanywa na kanisa nchini Ufaransa.

Matamshi hayo ameyatoa mjini Vatican katika mahubiri yake ya kila Jumatano kwa waumini ambapo amezungumzia takriban watoto 330,000 wa Ufaransa ambao walinyanyaswa na mapadri na viongozi wengine wa kanisa hilo kuanzia miaka ya 1950.

Amesema idadi hiyo ni kubwa na kwamba anaelezea masikitiko yake na mateso ya kiwewe ambayo wahanga hao wamekuwa nayo.

Papa Francis amewataka maaskofu wote na viongozi wa kidini kuchukua hatua zote muhimu ili kuzuia vitendo kama hivyo visijirudie tena.

Aidha, papa pia amewataka Wakatoliki wa Ufaransa kuhakikisha kwamba kanisa linabaki kuwa nyumba salama kwa wote.
 
Sasa wakati huo 'Bikira Maria' na 'Roho Mtakatifu' walikuwa wapi?!
Walitakiwa kuwepo ap sio wawazuie!!!?USIPENDE KUJUMUISHA VITU NA KUSEMA TUU KITU BILA KUFIKIRI VIZUR MANA HAPO UNAKUA SII UNAWAKEMEA WALE WALIOKOSA BALI UNAHUKUMU NA WENGINE WASIOKUWA NA MAKOSA😊
Hyo ni issue binafs ya utash wa mtu mwenyewe ni sawa tuu na Familia nzuri yenye Jitu Pumbavu huwa wanaangaliw Familia lakn so kosa lao bal ujinga wa mtu au watu wachache Na si kwamba wanaSupport mana ipo misingi katik kila din lakin waaminifu wakuifat ndo shughul inaanzia apo....
 
Wakatoliki ni waungwana, na hii ndio maana halisi ya kutubu, sio kulindana lindana
 
Walitakiwa kuwepo ap sio wawazuie!!!?USIPENDE KUJUMUISHA VITU NA KUSEMA TUU KITU BILA KUFIKIRI VIZUR MANA HAPO UNAKUA SII UNAWAKEMEA WALE WALIOKOSA BALI UNAHUKUMU NA WENGINE WASIOKUWA NA MAKOSA
Hyo ni issue binafs ya utash wa mtu mwenyewe ni sawa tuu na Familia nzuri yenye Jitu Pumbavu huwa wanaangaliw Familia lakn so kosa lao bal ujinga wa mtu au watu wachache Na si kwamba wanaSupport mana ipo misingi katik kila din lakin waaminifu wakuifat ndo shughul inaanzia apo....
Aisee wewe jamaa una Hekima km mfalme Sulemani,safi sana.
 
Sipati picha ingekuwa ni ostadhi ndio kasema hivi naona saa hii tungekuwa na page kama zoooteee, tena za kashfa, kweli nimeamini waislam waungwana sana
Big up
Hongereni sana kwa hilo
Kusemwa sana au kidogo hakuondoi kosa lenyewe
 
Kiongozi wa Kanisa Katoliki duniani, Papa Francis ameelezea aibu iliyolikumba kanisa hilo pamoja na yeye mwenyewe kutokana na kiwango cha unyanyasaji wa kingono dhidi ya watoto uliofanywa na kanisa nchini Ufaransa.

Matamshi hayo ameyatoa mjini Vatican katika mahubiri yake ya kila Jumatano kwa waumini ambapo amezungumzia takriban watoto 330,000 wa Ufaransa ambao walinyanyaswa na mapadri na viongozi wengine wa kanisa hilo kuanzia miaka ya 1950.

Amesema idadi hiyo ni kubwa na kwamba anaelezea masikitiko yake na mateso ya kiwewe ambayo wahanga hao wamekuwa nayo.

Papa Francis amewataka maaskofu wote na viongozi wa kidini kuchukua hatua zote muhimu ili kuzuia vitendo kama hivyo visijirudie tena.

Aidha, papa pia amewataka Wakatoliki wa Ufaransa kuhakikisha kwamba kanisa linabaki kuwa nyumba salama kwa wote.
Wakristo ubakaji na kazi za u-house girl ,,

Waislamu wagumu kutapeliwa!, Wagumu kufanyiwa usanii,wepesi kuhamua
 
Hakuna mtakatifu chini ya jua..kanisa limekiri na kuomba msamaha..mnataka nini sana kama sio unafiki...ukitaka kuwashambulia hao mapadri hakikisha na wewe huna dhambi..mana kipimo utakacho wa hukumu nawe ndio hicho hicho utakacho hukumiwa nacho.

#MaendeleoHayanaChama
 
Back
Top Bottom