Seif Shariff Hamadi agoma kumpa mkono wa salamu Rais Dkt. Shein!

BEHOLD

JF-Expert Member
Nov 17, 2013
5,057
10,715
14040098_1044044065715246_756741800607451030_n.jpg


Katika kipindi cha magazetini Leo, imeripotiwa kuwa Maalimu Seif alikwepa kusalimiana Dkt Shein walipokutana kwenye maziko ya Aboud Jumbe.

Hii inapeleka ujumbe gani kwa wana-Zanzibar?!
=============
Maalim Seif Kukataa Mkono wa Dr.Shein kwenye Mazishi ya Al-Hajj Aboud Jumbe Mwinyi. Ujumbe mzito Umetumwa. Kama ni Uchochezi kafanya Uchochezi mkubwa kuliko angefanya mikutano kumi ya hadhara. Watafute basi kifungu cha kisheria kumshtaki kwa Uchochezi wa kutopokea Mkono wa Rais Shein.

Utasikia Oh Ilikua Msibani. Nani aliwaambia Marehemu ndie anapaswa kutumika kama jukwaa la kuhallisha Unafiki halafu baadae ushiriki Ibada ya Kumuombea au Kuombea familia faraja? Utamuomba mungu wa Unafiki labda kama yupo!

Wale wanaomkasirikia Maalim Seif wakae hapa, Tena Watulie ! Kimyaah Kisha waulize Maswali badala ya kujipa vidonda vya Tumbo (Ulcers)Unnecessarily!

Siandiki kwa Sababu pia mimi ni Extremist linapokuja suala la kutetea haki au kupinga Uonevu katika mazingira kama ya Seif au Raila Odinga kule Kenya 2007 au Chifu Mashoud Abiola wa Nigeria mwaka 1993,Ideas na mambo Mengine. Na siandiki kwa sababu namhusudu Maalim Seif kwa kuwa ni Extremist (Mwenye Misimamo Mikali) kutetea haki yake.

Kushikana mikono ni utamaduni utokanao na Tamaduni mbalimbali na pia katika medani ya Diplomasia. Wanafunzi wa Masomo ya Diplomasia wanajua na walishawahi kufundishwa kuhusu Diplomatic Gestures(Ishara za Kidiplomasia).

Kwa mfano Wajapani ni Wanadiplomasia hatari kihistoria. Kwanza kukunja Mikono na kukutanisha viganja up-ward Straight na kuinama kidogo kama wafanyavyo Altar-Boys wa kanisa Katoliki ni Diplomatic Gesture ya kusalimiana kwa Wajapani.

Kwamba kuna Kusalimiana kwa kushikana mikono,Kukumbatiana,Kupungiana ,Tabasamu n.k

Nigusie la kushikana mikono..

Katika kushikana Mikono ni lazima uzingatie yafuatayo;

Kama unataka kusalimiana Professionally na kuonesha ukomavu kidiplomasia utafanya hivi;

-Ukimshika mtu Mkono tena ukisalimiana nae kwa tabasamu la bashasha na viganja vyenu vikakutana kwa ubapa inaonesha ninyi Mko Sawa(Equal) na mnafanana katika mambo mengi na kupendana pia.

Salamu ya aina hii ni lazima mshikane mikono kwa muda ukiwa unamuangalia mwenzako usoni straight na tabasamu.Tena Mkono wenyewe ushike Tight.Kinyume na hapo unatuma ujumbe wrong kidiplomasia kuwa ni dharau, Jeuri, Chuki, kutomtilia maanani unayemsalimia. Huwezi kupeana vidole ikawa salamu bali ni kejeli.

- Kiganja kikikaa juu ya kiganja cha Mwingine maana yake wewe ndio unamtawala mwingine,Superior and Dominant. Kiganja kikikaa chini ya cha Mwingine maana yake wewe ndio Inferior na Umeji-Submitt kwake.

Halafu Ukaaji. Kama wewe ni kiongoz au unataka kutuma ujumbe kuwa wewe ndio dominant katika Upigaji Picha ni lazima uwe Smart.

Ukae Upande wa Kushoto wa Mwenzako.Kama mtashikana mikono ataleta mkono wake na wewe utafanya Counter-Touch na mkono Wako Mwingine unaweza kumgusa kwenye Elbow,mkono mwingine, Bega n.k.

Ina maana wewe ndio Superior na unam-control mwingine

Hapo ni kwa ufupi..

Sasa katika Diplomasia kali unaweza ukaacha kushikana mikono na Adui/hasimu wako kupinga unachoamini juu yake.Ni mbinu powerful kuliko kutumia vifaru na majeshi hasa ikiwa abayetumia nguvu kajileta.Hiyo ni golden chance ya kummaliza.Hakuna Dikteta smart anayeweza kufanya kosa hilo labda Dikteta Uchwara ambaye yupo desperate kutumia kila njia kujihalalisha. Ni kosa kubwa Mno!

Kama ni Dikteta anayepora haki yako na ya wengine unaweza ukaamua kumpuuza na kuacha kabisa kushikana nae mikono as a protest. Unapinga unafiki.

Unaposhikana nae mikono na kutabasamu maana yake unakubaliana nae au mna deal ambalo mmejadiliana na mtawekana sawa soon.

Kwa siasa za Zanzibar unatuma ujumbe kuwa mambo yalikua shwari na mimi kiongozi wenu ninakubaliana na namtambua Shein kama kiongozi halali na yale masuala ya kufuta uchaguzi halali oktoba 25 ilikua sahihi na hakuna shida kabisa kabisa kwa hiyo wafuasi wangu nao waungane na wale waliofikiriwa kuwa washirika wa ubakaji wa demokrasia

Ndugu za wale waliowekwa ndani,waliochomewa nyumba zao na Mazombi,waliovamiwa na Green Guard, Waliotukanwa na hata kujeruhiwa walie tu.

Katika Somo la Diplomasia kuhusu case hii tulikutana na Case Study ya Mwanadiplomasia tishio Henry Kissinger aliyekuwa Waziri wa Mambo ya nje wa Marekani .Marekani ilikua inapanua himaya yake Chile na Latin America wakati huo huo inamuandalia Mazingira ya kumruka Rais wa Chile kwenye mapinduzi.

Alikua akitumia mbinu hii dhidi ya Dikteta Augusto Pinochet wa Chile alipokua akitaka kufikia deal fulani tu.

Waziri Mkuu wa Uingereza Neville Charmbalain aliwahi kushikana mikono na Hitler kwa sababu serikali ya NAZI ilitaka kupata sehemu ya Jamhuri ya Sasa Zcechslovakia.Na ni for the sake of peace tu .Akaandaa Mazingira ya kujipanga .Neville akaondolewa akaja Churchill akapeleka a bit prepared Combative army ya Uingereza Vitani .Vita kuu ya Pili ya Dunia.

Reagan na Marcos walishikana mikono kwa sababu walitaka kufikia makubaliano.

John McCain na Muammar Ghaddaffi kama mkakati wa ku-negotiate mambo kadhaa na kulegeza msimamo wa Ghaddafi kisha akaja kumalizwa.

Madikteta nao hupenda sana kushikwa mikono na watu wanaoongoza kuwapinga ili kujihalalisha mbele ya wafuasi pinzani.

Ndio maana kwenye Diplomasia inafundishwa namna ya ku-deal na Magaidi na hata wauaji katika mission za kidiplomasia.Gaidi humtamkii kuwa you're terrible and a murderer.Anataka aitwe Freedom Fighter,Akumbatiwe na upige nae Picha.Kuna tactics za kukwepa hizi mkiwa kwenye negotiation.

Jan Egeland ambae ni Balozi wa UN katika masuala ya kiutu(Humanitarian) aliwahi kukutana na Joseph Kony ,Kiongozi wa kundi la waasi la Lord's Resistance Army la Uganda ambaye alikua akituhumiwa kwa Kuteka maelfu ya watoto kuwatumikisha vitani na hata kuteka wanawake na kuwabaka.

Jan Egeland kwa sababu alikua kwenye Mission ya kidiplomasia alilazimika kukutana nae lakini katika zoezi la kupiga picha aligoma kutabasamu kama ishara ya kutuma gesture kuwa hakubaliani nae kwani kama angetabasamu maana yake wale ndugu wa watu waliotekwa na hata kuuawa na wengine kubakwa wangevunjika Moyo na ingeweza kutafsiriwa kuwa Kony ni mtu mzuri tu hadi yupo na watu wazuri hivi wanacheka?

Katika fitna ya Siasa.Kwa jamii inayokubalika kiislam au kikikristu mwanasiasa smart anaweza kutumia viongozi wa Dini kuonekana nao hadharani ili kutuma ujumbe wa kiushawishi kwa jamii ya dini husika hata kwenye Soka.

Hata hivyo,Mbinu hii ya kushikana mikono katika Diplomasia inatumika kumchanganya Adui hasa adui asiye na madhara makubwa

Barack Obama alimshika Mkono Raul Castro Hivi majuzi.

Lengo ni nini? Lengo ni kumuweka Castro Dillemma.

Kaka yake yaani Fidel alikuwa Adui wa America kwa miaka zaidi ya 50 wamewekewa Vikwazo. Leo Obama anafanya handshake?

Leo kwa wasomi wa Diplomasia wajiulize Msimamo wa Cuba dhidi ya Marekani ukoje wakati hata vikwazo havijaondolewa? Confussion Tactic.

Maalim Seif Shariff Hamad alikua sahihi na nampongeza

Koffi Annan kwenye kitabu chake "Interventions- In the Time of War and Peace" aliandika kisa kimoja jinsi ambavyo alikuwa akikutana na viongozi wa Taleban na jinsi alivyotumia Umaahiri katika kuwasoma na kukwepa baadhi ya matukio na ishara .

Kwenye Ukristu Yuda Iskariot alienda kumsaliti Yesu kwa Kumbusu.Yesu hakumkawiza akamuuliza "Unamsaliti Mwana wa Adamu kwa Kumbusu"?

Alikataa Unafiki wa Yuda aliyekwisha waambia wayahudi kuwa nitakayemkumbatia na kumbusu ndie

Alikua akitoa ishara ya kiuadui ambayo ilikua kwa faida ya Yuda na Wayahudi na Hasara kwa Yesu

Sitaki kuandika kuhusu mabusu,Kukumbatia na kukataza watu kushikana viuno na nyonga.

Naenda Zangu

Aluta Continua,Victory Ascerta.....

Ben Saanane
 
Back
Top Bottom