Nifanyeje wadogo zangu wajenge interest ya kupika?

TheChoji

JF-Expert Member
Apr 14, 2009
5,014
15,402
Mimi ni mwanaume, nna mke na watoto lakini pia naishi na wadogo zangu wawili wa kike (miaka 18 - 21) na msichana wa kazi. Binafsi najua kupika vizuri na pia napenda kula vyakula vitamu. Mke wangu ni mtu wa kuchelewa kurudi na akirudi yuko hoi.

Kinachonisumbua ni kwamba, hawa ndugu zangu ninaoishi nao ni HAWAJUI KABISA KUPIKA na hawana interest hata ya kujifunza! Yaani mi naenda mjini narudi na sato, au kuku, maini, nyama, nk natia kwenye friji.

Viungo vyote, nazi, kila kitu nahakikisha kipo. Matarajio yangu nikija nikute chakula kizuri ila sasa hayo makorokocho ntakayokuta hata hamu ya kula inaniishia. Chuzi la nyama utalikuta jekunduu limejazwa mimaji na mimafuta, nyanya zinaelea, vitunguu havijaiva, halafu eti wamepika na ugali! Siku zikipikwa mboga za majani utadhani zimekatwakatwa kwa panga.

Yaani vululu vululu. Cha ajabu wao wanaona poa tu. Nimejaribu kuongea nao na mara moja moja hua naingia mwenyewe jikoni nakorofisha misosi ya nguvu. Lengo ni ili na wao watamani kujua kupika lakini naona interest hawana kabisa. Imefika mahali hata kuleta vitu tena naona haina haja bora niwe nakula mitaani.

Nawaza sijui wakija kuolewa itakuaje na kwakweli sijui niwasaidieje.
 
Inasikitisha na Pole! Samaki mkunje angali mbichi ila hujachelewa! Jaribu kuwapa changamoto mfano wakihitaji kitu kutoka kwako wape sharti la atakayepika chakula siku hiyo vizuri ndo unampa kitu anachohitaji. Basi wataingia hata Youtube kuangalia na wataimprove.
 
Shida kidogo tu unakuja kutangaza ndugu zako JF eti hawajui kupika.
 
Pole ila mwombe wife wako atafute muda walau jmos na pili awafundishe kupika yeye, hao miaka 18 ni wakubwa sana walitakiwa wajue kupika.
Wife akiwepo hua anapika lakini cha ajabu wakati wife yupo jikoni anapika, wao wanakua sebleni wanaangalia TV. Sasa wife hawezi kuwalazimisha maana unajua tena mambo ya ndugu hawakawii kuanza kusema wananyanyaswa. Wangekua interested kujua kupika wangeenda kuangalia anavyopika ili wajifunze lakini wao waala.
 
Wakiwa kwa maboyfriend zao wanapika vizuri tu na kufua pamoja na usafi wa kiwango cha Maglev train system
 
Wakiwa kwa maboyfriend zao wanapika vizuri tu na kufua pamoja na usafi wa kiwango cha Maglev train system

Kwamba hapa nyumbani wanapika vibaya makusudi? Mbona na wao wanakula hicho hicho wanachopika?
 
Wafukuze waambie waende jikoni kumsaidia wifi yao kupika badala ya kuangalia TV na mwambie mkeo achukue jukumu kila anapopika wawe naye jikoni ili wajifunze kupika.
Wife akiwepo hua anapika lakini cha ajabu wakati wife yupo jikoni anapika, wao wanakua sebleni wanaangalia TV. Sasa wife hawezi kuwalazimisha maana unajua tena mambo ya ndugu hawakawii kuanza kusema wananyanyaswa. Wangekua interested kujua kupika wangeenda kuangalia anavyopika ili wajifunze lakini wao waala.
 
Back
Top Bottom