Nifanyeje wadogo zangu wajenge interest ya kupika?

Pole sana yaan wamepoteza Bikira zao wakat hawajui kupika wakaona kupigwa ukuni ni bora kuliko kujifunza kupika,,hawa ndionwateja wakuu wa chips zege pindi wakianza kujitegemea
 
Ni rahisi kwako ku deal na mdogo wako wa kike kuliko mimi. Wangekua wa kiume mbona ningeshawalamba mangumi mda tuu..

Kumbuka pia sio kwamba hawataki kupika, kupika wanapika kila siku sema ndio hivyo wanapika makorokocho
Nilileta mfanyakazi wakiume kutoka Tanga, alikua hajui kupika chochote, lkn mimi sijaoa bado, kwahio nilikua naishi nae yeye, huyo mdogo wangu wakike alikua chuo bado, anakuja nyumban weekend. Dogo huyo kutoka Tanga alikua hajui kupika chochote, lkn nilikua namwita namuinesha vituguu tukata hivi,nyanya tunasaga hivi, kesho Nikitaka kupika namwambia akate kwaanza vituguu nione, na nyanya,naviungo vingine akifanikiwa kukata vzr, keshokutwa yke namwambia tunaunga hivi mboga namwambia haya unga anaunga nimemsimamia na alijua, same case kwenye ugali,wali,tambi,ndizi navinginevyo ilimchukua miezi 3 akawa anajua vzr tu. Sasa sijui wewe unawasimamia viipi.
 
Wewe ulifundishwa na mama yako. Sasa kwani mimi ni mama yao
wanaweza kufundishwa na yeyote maisha sio ya kukariri siku hizi kuna mpaka madarasa ya mapishi pesa yako tu, kuna wengine wamefundishwa na mashangazi, mabibi etc
 
Wasichana wa umri huo hawajui kupika?

Mlaumu aliyewalea lakini bado wana nafasi ya kujifunza maana elimu haina mwisho
 
Bado unao muda kidogo wa kuwaelekeza mkuu. Ingawa soon watakuwa wake za watu hao.
 
Wanawake wengi hawajui KUPIKA.. 70%

Nb:
Kuna kujua kupika Chakul kikaiva..

Na
Kujua kupika Chakul kilichoiva na KITAMU.

wengi wanajua kuivisha tu
 
Kuna uwezekano tatizo kubwa ni wewe Chief!

Hebu kuwa mkali na mfatiliaji wa karibu wa mienendo yao yote!

Wawekee zamu za kupika, dada wakazi afanye kazi nyingine jikoni hasikanyage!

Na kila wakitoa boko wape adhabu kama za kuwanyanganya simu even for a couple of days, or no watching tv for a week, ama hakuna personal allowance for a month, ama kuosha kuta za ndani ya nyumba, or tending the garden and sweeping the compound every day at down (alfajiri) kwa zamu pia!! Wanyooshe, wasaidie!

Watoto wa kike to have such traits at such a tender age is almost a misfortune!

And tell your wife to step up, lawama hazikwepeki ila pia pongezi when things turn out good atazifurahia! She is their “sister-in-law” anyway, so basically ni kama dada yao mkubwa tu!
Nimependa English yako

Naomba nifundishe
 
Wife kupika anajua sema muda ndio hua hana. Na siku akiwepo wao hawaangaiki kujifunza wanamuachia jiko wanapandisha miguu kwene makochi.
Wewe kaka yao mwenye nguvu nao ungewaambia wachacharike..kiafrika haijakaa poa wadogo zako wa umri huo wameweka miguu juu ya makochi wanasubiri wifi aivishe...
 
Mkuu unaweza kunilaumu lakini kwangu wamekuja tayari wakubwa, sio kama nimewalea tangu utoto. Kikubwa kilichowaleta ni shule. Mdogo yupo A level na dada yake yupo chuo
Kwa hiyo kama umewakuta hivyo unatamani kuendelea kuwaona hivyo hivyo? Bro...hebu wakazie kidogo daah...
 
Chief, it’s either unatuchora hapa ama unatukomba kama kiporo cha maharage na wali!!

Chips gani inavutika kama nyama?

Kiazi mbatata kikaangwe, kikikauka ni kavu ama ngumu,....kisipokauka ni rojo ama mvimbo...!

Nielekeze wanafanyaje kiazi kinavutika kama nyama, Please!
😂😂 imebidi nicheke..bro kapeleka viazi gani hivi nyumbani kuishia kulaumu watoto hawajui kupika?
 
Mimi ni mwanaume, nna mke na watoto lakini pia naishi na wadogo zangu wawili wa kike (miaka 18 - 21) na msichana wa kazi. Binafsi najua kupika vizuri na pia napenda kula vyakula vitamu. Mke wangu ni mtu wa kuchelewa kurudi na akirudi yuko hoi.

Kinachonisumbua ni kwamba, hawa ndugu zangu ninaoishi nao ni HAWAJUI KABISA KUPIKA na hawana interest hata ya kujifunza! Yaani mi naenda mjini narudi na sato, au kuku, maini, nyama, nk natia kwenye friji.

Viungo vyote, nazi, kila kitu nahakikisha kipo. Matarajio yangu nikija nikute chakula kizuri ila sasa hayo makorokocho ntakayokuta hata hamu ya kula inaniishia. Chuzi la nyama utalikuta jekunduu limejazwa mimaji na mimafuta, nyanya zinaelea, vitunguu havijaiva, halafu eti wamepika na ugali! Siku zikipikwa mboga za majani utadhani zimekatwakatwa kwa panga.

Yaani vululu vululu. Cha ajabu wao wanaona poa tu. Nimejaribu kuongea nao na mara moja moja hua naingia mwenyewe jikoni nakorofisha misosi ya nguvu. Lengo ni ili na wao watamani kujua kupika lakini naona interest hawana kabisa. Imefika mahali hata kuleta vitu tena naona haina haja bora niwe nakula mitaani.

Nawaza sijui wakija kuolewa itakuaje na kwakweli sijui niwasaidieje.
Miaka 18-21 hawajui kupika??? Binti yangu 8yrs anajua kupika vyakula vyote isipokua ugali unamshinda kusonga, na akipika familia inakula inafurahia, ni kwamba tu anahitaji msaada mdogo kama kuepua jikoni au msimamizi wa karibu kwa sababu mazingira ya moto ni hatari kwa mtoto especially kwa umri wake

Sijajua walipata malezi gani lakini moja ya malezi ya mtoto ni pamoja na kumfundisha shughuli za nyumbani kama usafi,kupika, kusimamia nyumba, kuangalia watoto nk, kipindi cha likizo au eeekend na hata weekdays kama homework zimeisha kwa wakati

Kama hakufundishwa hiyo spirit tangu wadogo, sasa wamekua watu wazima ni ngumu sana though kama wana nia basi ni rahisi wao kujua

Mkeo nae ni ubize gani huo unaomzuia kuingia jikoni japo kila jioni, kwani kazini anaenda kulima? Kama ni ofisini kukaa kwenye computer tu jamani akirudi anashindwa hata kuandaa chakula cha familia?
Zungumza na wadogo zako, kuna siku wataolewa na watatakiwa kutimiza majukumu kwenye ndoa zao ikiwa ni pamoja na kupika, waambie wapende jikoni maana jiko ni sehemu ya maisha ya mwanamke wa kiafrika
 
Pole sana...

Wadogo zako hawana makosa... wakumnunuia ni mkeo...

Kazi ya kukupikia utakavyo wewe ni ya mkeo, siyo wadogo zako...

Mkeo atakua hajui kupika na mvivu sana...



Cc: mahondaw
 
Back
Top Bottom