Nifanyeje wadogo zangu wajenge interest ya kupika?

Wife akiwepo hua anapika lakini cha ajabu wakati wife yupo jikoni anapika, wao wanakua sebleni wanaangalia TV. Sasa wife hawezi kuwalazimisha maana unajua tena mambo ya ndugu hawakawii kuanza kusema wananyanyaswa. Wangekua interested kujua kupika wangeenda kuangalia anavyopika ili wajifunze lakini wao waala.
Kwa hii comment yako, naomba niseme wazi kwamba wewe sio kaka mzuri kwa malezi. Na yawezekana wewe ndie umeshindwa kuwasimamia wadogo zako kutokana na malezi mabovu walio yapata kabla ya kuishi kwako.
 
Wife kupika anajua sema muda ndio hua hana. Na siku akiwepo wao hawaangaiki kujifunza wanamuachia jiko wanapandisha miguu kwene makochi.
Lahaula......
Kumbe nimeamini wanaume tumetofautiana kwenye malezi aiseeee.
Mkuu umenisikitisha zaidi
 
... tatizo unalijua halafu unalea upumbavu. Fukuza wakapange wajifunze maisha watatia akili. Ukiwaendekeza kinachofuata watakuletea wajomba hapo nyumbani; soon very soon.
Wanasoma mkuu siwezi kuwatimua
 
Mbona wakubwa watu wazima hao? Umeanza kuishi nao wakiwa na umri gani? Wamekulia kwako au kwa mama yako? Kuna shida kwenye malezi katika ukuaji wao. Binti anatakiwa aanze kujifunza kupika akiwa na Umri wa miaka 12. Sasa hao dada zako Sijaelewa ilikuwaje Hadi wakafikia hatua hiyo.
 
Kwa hii comment yako, naomba niseme wazi kwamba wewe sio kaka mzuri kwa malezi. Na yawezekana wewe ndie umeshindwa kuwasimamia wadogo zako kutokana na malezi mabovu walio yapata kabla ya kuishi kwako.
Mkuu unaweza kunilaumu lakini kwangu wamekuja tayari wakubwa, sio kama nimewalea tangu utoto. Kikubwa kilichowaleta ni shule. Mdogo yupo A level na dada yake yupo chuo
 
Kuna uwezekano tatizo kubwa ni wewe Chief!

Hebu kuwa mkali na mfatiliaji wa karibu wa mienendo yao yote!

Wawekee zamu za kupika, dada wakazi afanye kazi nyingine jikoni hasikanyage!

Na kila wakitoa boko wape adhabu kama za kuwanyanganya simu even for a couple of days, or no watching tv for a week, ama hakuna personal allowance for a month, ama kuosha kuta za ndani ya nyumba, or tending the garden and sweeping the compound every day at down (alfajiri) kwa zamu pia!! Wanyooshe, wasaidie!

Watoto wa kike to have such traits at such a tender age is almost a misfortune!

And tell your wife to step up, lawama hazikwepeki ila pia pongezi when things turn out good atazifurahia! She is their “sister-in-law” anyway, so basically ni kama dada yao mkubwa tu!

Daah.. kweli mimi niache shughuli zangu nianze kukimbizana na wamama kama hawa kuwafundisha kupika wakati wao wenyewe hawataki....?
 
Mimi nimeongea nao naona hawanielewi. Wife pia kashajitahidi kuwashawishi lakini wapi bana

Mimi nimeongea nao naona hawanielewi. Wife pia kashajitahidi kuwashawishi lakini wapi bana.
Yan jitahid hata kwa fimbo. Ndio wanakua hivyo. Au kwenu hiyo tabia ipo so wameirithi tu
Kama wanapika chakula kibaya wafundishe kinguvu sababu kwa sasa wataona unawatesa waache wafikirie hivyo, lakin wakiwa na nyumba zao watarud kukushukuru.

Ngoja nikupe mfano nilikuwa na mdogo wa kiume hapendi kufua lakin mwanzo nilikuwa sijui, kafika la 4 Nampa nguo anafua, unajua nilikuwa namsimamia, anafua haraka Ili awahi katuni, hivyo nguo zinatoka chafu. Nilikuwa namrudisha hata Mara 6, na fimbo juu,na remote hapati, ananuna lakini namkazia.

Yupo mtu mzima Sasa hiv, anafua nguo zake vzr tu, lakin Kama wanaume wengi mnavyojijua hampend kufua,
Lakin hanipi shida, kufua anajua ila mvivu wa kufua, ninachomshukuru Mungu kufua kaweza huo uvivu wa kufua akipata mke atapambana naye.


Sasa hata Kama Ni wavivu hao wadogo zako au hawajui hakikisha wajue kupika vzr kwanza halafu huo uvivu watapambana na waume zao huko, lakin mvivu halafu kupika hajui Hilo Ni bomu
 
Tatizo linaweza kuwa ni wao kutokujua kama hawajui kupika, wanahisi wako sawa. Ushawahi kuwadokeza kuhusu hili tatizo ?
 
Daah.. kweli mimi niache shughuli zangu nianze kukimbizana na wamama kama hawa kuwafundisha kupika wakati wao wenyewe hawataki....?

Hakuna sehemu nimesema uwafunze kupika Chief!

Skiza, when you decide to take over taking care of someone, most especially your siblings then you have to take 100 percent responsibility! Otherwise kama wamekuja kwa ajili ya shule tu then wapangishie ghetto kabisa!

Vinginevyo mdharau mwiba miguu huota tende!

Wasaidie waepukane na aibu za ukubwani lakini pia waondoshe hatari ya wanao kufuata nyendo zao, kwa sababu amini husiamini wanao hao “ma auntie” zao ndio kioo cha kwanza kabisa kwao even before you as their dad or mkeo as their mom, considering the fact that wako nao muda mrefu zaidi yenu na umri kati yao ni rafiki zaidi!

Help them achieve their potential & their given powers by separating them from a virtual world (maisha ya kufikirika) and real life!

Besides real life is almost the nightmare we are all trying to escape by using either TVs, phones, na starehe nyingine !

Wanyime hizo starehe kwa kuwaamulia how to control their given 24hrs of the day, in the long run utakua sawa na anaechenjua dhahabu kwa kuipitisha kwenye tanuru la moto for the final & beautiful product!

Wasaidie, watakukumbuka milele! Even way into their generations!
 
Kwani background ya familia ipoje? sababu unaweza laumu kumbe kwenu mmekuzwa kwa michemsho? Unajua kuna watu wanapiga BSc in Food and Technology hapo SUA miaka mitatu(3)?, mapishi haya yana art na science na vyote vinahitaji exposure.

Unaweza kuta na wao wanasemezana humu ndani mbona wanapika msosi wa hovyo?, Anyway hao ni watu wazima kwa mujibu wa katiba ya Tanzania.
 
Kwani fackground ya familia ipoje? sababu unaweza laumu kumbe kwenu mmekuzwa kwa michemsho? Unajua kuna watu wanapiga BSc in Food and Technology hapo SUA miaka mitatu(3)?, mapishi haya yana art na science na vyote vinahitaji exposure.

Unaweza kuta na wao wanasemezana humu ndani mbona wanapika msosi wa hovyo?, Anyway hao ni watu wazima kwa mujibu wa katiba ya Tanzania.

Sikufahamu hili la SUA na hiyo dep. I will definitely check it out! Ubarikiwe!
 
Mkuu unaweza kunilaumu lakini kwangu wamekuja tayari wakubwa, sio kama nimewalea tangu utoto. Kikubwa kilichowaleta ni shule. Mdogo yupo A level na dada yake yupo chuo
Kwakua wamekuj kwako, basi acha kulalamika na chukua hatua. Weka sheria za nyumbani kwako ikiwamo kufua, kupika na kufanya kazi za nyumbani kwa ujumla. Usimuachie mkeo awanyooshe wadogo zako, maana anaweza akahofia kwa kuogopa kuingia kwenye lawama za mawifi. Wawekee utaratibu ambao utakua ndio sheria ya hapo nyumbani kwako kama mkeo akiwa anapika lazima wawepo na washirikiane nae ili next time wapike kama walivyo ona kwa mke wako. Ama wakati mwingine usiingie jikoni wewe bali ingia nao jikoni na wapike kwa kufuata maelekezo yako.
Tena yawezekana mkeo hajiskii vizuri kwa kuona wadogo zako wamepata malezi ya hovyo hata leo hawajui kupika, na yawezekana hata anajiona kama hawezi tena kufanya wajibu wa alie walea hakuwajibika vilivyo.
Mwisho kabisa, sio jukumu la mke wako kuwafundisha wadogozako kupika.
 
Ukweli ulio wazi! Cooking is an art & technology is the future of all foods!

Nakumbuka dada yangu ikifika zamu yake ya kupika, kwenye wali/ubwabwa/mchele lazima utoke na kiini (mbichi fulani hivi unatafunika kama soft groundnuts!) Basi baba alikua anasema “ wali wa leo kama kikundi cha muziki cha wangoni na vikaputula vyao!”

*Don’t mean to disrespect any tribe!
 
Back
Top Bottom