Zitto: Sitagombea ubunge 2015, Nitagombea Urais kupitia CHADEMA...

Status
Not open for further replies.
I am getting to a point I am starting to question this guy Mkandara's educational credibility. Naskia kwamba jamaa anafundisha chuo kikuu. Kwa akili za namana hii nilitegemea awe kiongozi siyo mfuasi. Kwani Mkandara hajui kwamba Zitto ni CCM? Mkandara hajui kwamba kundi la Membe linamtumia Zitto kulichafua CDM?

Tanzania kila ni cha kufoji, sitahangaa huyu mkandara amefoji kitu sehemu. I am very doubtful of his interlectual might and integrity. CCM tunajua kwamba Zitto ni Kibarka. Yeye anachopinga ni nini?

Bw. Mkandara wewe hauoni kwamba hii kauli ni tata? unadhani professa Muhongo au Magufuli wamezaliwa lini? Kwa nini wasiwe kwenye uongozi? Kwamba zitto kasema? You need to evaluate things you post here. Be serious
Duh eee bwana wee mimi mhuni tu wa mujini sina uwezo wa kufundisha elimu UDSM wala sina mahusiano na mtani wangu yule Mukandara. Na kweli sina elimu hivyo nilisoma tu madrasa.. na wala elimu yangu haiwezi kunisaidia kumjua Zitto kama kibaraka au laa. Magufuli na Muhongo wote wameukuta Uhuru tayari umeshaandaliwa na wazee. Wote hawa wamesomeshwa na kukuzwa na UHURU.

Usijipe ugonjwa buree, Mimi mtu mdogo sana mbemba box tu. Ukipima watu kwa elimu yao basi utapotea kabisa maana Mugabe ana digrii 8 na nchi yake hohehahe unadhani sababu nini? - UZEE nguvu hana na kichwa hakifanyi kazi sawasawa tena.
 
Honourable Ladies and Gentlemen, the Great Friend of Truth is Time. In the future (2015>) we people should look for a True Leader who will keep our Hopes Alive and not a destructor and despot President.
 
Sipingi zitto kugombea urais lakini hii kauli haijengi bali ina bomoa
mambo ya kusema kuna watu wanajifanya wanaijua cdm si kauli nzuri, naona niya jazba tuu.

#AMPLIFAYA Sep27 #2 ZITTO
KABWE: nitagombea Urais 2015
sitogombea tena Ubunge, kuna
watu wanajiona ni CHADEMA zaidi
kuliko mimi lakini hawajui.

Source: Amplifaya - Clouds fm.
 
Ushabiki wa CDM sijaupenda...vitu vingine tuamue na Tumjadili mtu Binafsi ...izi Yes YeS kuteTeana mtakuja Kulaumiana..

Sent from my BlackBerry 9900 using JamiiForums
 
Nashukuru kwa uungawana wa kunielewesha hilo.Ngoja nifanye mpango wa kuisoma katiba hiyo ili nione kama ninaweza kuachana na ushabiki na niwe mwanachama.Lakini kama huyo aliyenijibu ndo mwanachama,hao wanaharibu chama.Ndo hao wanaojidahi ni chadema humu lakini hawana uvumilivu na wanawabeza watu wengine hata imani zao na mengine.Mtu akinijibu kwa style ile huwa najuliza mara mbilimbili kuhusu uanachadema wake.Especially given the fact that niliuliza swali ili nieleweshwe.

Mkuu,
Usishangae sana, Watanzania wengi hasa wale wanaoishi 'bongo' bado wako nyuma sana linapokuja swala la kisiasa. Tatizo kuu, wengi wao ni 'washabiki wanachama' na siyo wanachama hasa ambao pia wanaenzi demokrasia ya kweli. wakati mwingine siyo makosa yao kwa sababu wazee ndani ya CCM walitaka kuwaaminisha wanachama wao kuwa wapinzani ni adui na hizi kauli ndizo wengi ndani ya CCM waliziamini na haya ndiyo matokeo yake.

Huu ugonjwa wa hizo fikra finyu ndiyo pia umetapakaa kwa wanaojiita wanachama wa chama vya upinzani ili kupambana na wanachama na wapenzi wa CCM.

Watu wengi humu janvini hawakubali kutokubaliana badala yake wanabakia kurushiana matusi tu
 
Hizi tabia za kijinga za huyu Zitto zinanikumbusha JK naye alikuja kwa gia hizi hizi, ila Nyerere alisimama imara na Watanzania hatukumuelewa Nyerere kwa nini alimkataa JK, ila leo kila mtu anashuhudia matatizo anayotuletea huyu mtu, sasa imagine kama angekadhiwa hii nchi mwaka 1995 ingekuwaje?

Ndio sasa nimeshaelewa vizuri ni kwa nini CCM wanatamba watashinda 2015 na ni kwa nini wana mitandao ya kuusaka Urais kwa sababu Agent wao ndani ya Chadema anairatibu kazi vyema kabisa. Nasikitika sana kusema kwamba Chadema isahau kuingia madarakani 2015 kwa sababu ni Chadema wenyewe ndio wameamuwa kwamba hawahitaji kukabidhiwa nchi.

Hivi Chadema inashindwa vipi kuiga hata mazuri kutoka NCCR? kwani huyu pacha wake na Zitto huyu Kafurira na yeye si alishaanza kuitamani nafasi ya Mbatia? mnaweza kuniambia Kafurila ameishia wapi? hayo ndio maamuzi, mbona CUF wamemfuta Uanachama Hamad Rashid wakati ni mwasiasa mkongwe? who is Zitto?
 
Zitto anatumia discrimination based on age.Angekuwa na mawazo mazuri ya kiuchumi ya kulisaidia taifa,anatakiwa ajipange halafu ayapambanue kwa wananchi ili wamwelewe.

Lakini mambo ni tofauti kwasababu anafahamu watanzania ni washabiki shabiki tu,wanasikiliza chochote kama vile ni mpira wa miguu na wao kudandia tu na kuamini kabisa kuwa eti mtu mzee hana mawazo ya kuweza kulisaidia taifa kwenye uchumi.

Yani kauli hizi zinashangaza sana.Na hata kama alitaka kuitumia hoja hiyo,there is ways to get your message through kwa wanachadema wenzake,sana sana kauli hiz ni divisive.
 
as if Zitto is not entitled to own make statements. I don't think that everytime Zitto makes a statement then we should correllate to Chadema operations. We should also understand this person is a Tanzanian too, he has equally all rights as any other Tanzania citizen....Give him a break neh!

Wachaga wanataka maneno hayo angeyasema Lema ndo wangesema lema ni jembe lao!
 
Miaka 65 aliyanayo babubaba Slaa ni miaka 17 tu ndio katumikia chadema na miaka 48 katumikia ccm.Slaa aliondoka ccm baada ya kubwagwa kula ya maoni ndani ya ccm sasa huyu babubaba ni mpinzani kweli wa ccm?
Namwita babubabu maana miaka65 anamtoto wa mwaka mmoja sasa(junior).
 
Wakuu,

Sekunde chache zilizopita nimemsikia zito kwenye exclusive interview na Millard Ayo wa clouds fm akitamka yafuatayo ..."Wazee wetu walitusaidia kutupatia maendeleo ya kisiasa, sasa ni jukumu letu kuleta maendeleo ya kiuchumi. Ila naomba nisisitize, jukumu hili haliwezi kutekelezwa na mtu yeyote aliyezaliwa kabla ya uhuru.."

Swali: Zitto anataka nini hasa?ana haja gani ya kuendeleza siasa za controversy namna hii kila siku?Je anatafuta umaarufu?

Binafsi ninamshauri aamke. Sisi ndio wapiga kura, atuache tuamue.

Zitto ana haki zote za kutamka maneno hayo kama mawazo yake. Hivyo ndivyo yeye anavyoyaelewa maendeleo ya kiuchumi yatavyoweza kutekelezeka.

Kifupi, Zitto haamini kuwa Changamoto ya kiuchumi katika utandawazi unaweza kutatuliwa Tanzania na kiongozi aliyezidi miaka 50.

Ninamuelewa vizuri kabisa NA ANAWEZA KUWA YUPO SAHIHI, kwa sababu kiongozi anayesimama mbele ya watanzania milioni 35 na kuwaahidi kuwapa elimu bure bila kuonyesha hizo pesa atapata wapi n kitendawili.

Viongozi kama hao wamepitwa na wakati na wanatakiwa wawajibishwe kwa kigezo cha UMRI WAO. SI KOSA LAO, NI KOSA LA UMRI WAO NA KWA HILO HATUWEZI KULIBADILI.
 
Inawauma sana Zitto akiondoka na toto lenu na Mujini eeeh!.. Msijali Zitto bado hana umri wa kugombea lakini haina maana haruhusiwi kusema wazee wang'atuke. Ubaguzi gani wakati umefika kweli wang'atuke? Je wao sio wabaguzi kung'ang'ania nafasi za juu ktk uongozi kwa miaka zaidi ya 50 wakiwaachia vijana makapi!.. Wengine tutakula wapi aaah! Mpaka Mungu awalazimishe kwa vifo jamani..

Tumeshakshtukia, unakuwa na ushabiki wa kipumbavu kama siyo wa kijinga. Kama Zitto ndio Rais wako, basi usitupotezee muda kuchangia kwenye hii thread. Sisi ndani ya Tiss tuiochoka na CCM ndio tunaomjua Zitto. Wewe haumjui. Kwa hiyo nyamaza. Be careful kwenye vitu unavyopost humu ndani mkuu
 
UDINI itakimaliza CHADEMA tatizo la zitto ni uislam wake chama anachokipigania kina mrengo wa kueneza UKRISTO na misaada wanapokea CDU ya ujerumani.
Mkuu acha kuingiza mambo ya udini katika agenda hii, Tanzania tangu uhuru imeshakuwa na viongozi wa dini mbili ngeni labda ni dini ya jadi tu hatujapata kiongozi, na hatudai maana dini siyo inayotuongoza, tunataka kiongozi. Kuhusu hoja sasa, ni kweli tunahitaji ukombozi wa kiuchumi, kama vile ukombozi wa kisiasa ulivyoletwa na vijana wa wakati huo waliokuwa na uchungu wa nchi zao na mawazo ya ukombozi kama akina Nkrumah, Nyerere, Kaunda, Lumumba, Ngwabi nk, nyakati hizi tunataka "vijana" wenye mawazo hayo, na hapa sisemi idadi ya miaka ama kuzaliwa kabla ama baada ya uhuru bali mwenye mawazo ya ujana, yaani kujua hitaji la sasa kuwa nu ukombozi wa kiuchumi. Hili halihitaji namba ya miaka bali linahitaji mapinduzi ya kifikra, maana unaweza kuzaliwa baada ya uhuru lakini ukawa na mawazo ya ukibaraka, na ubinafsi hata usisaidie ukombozi wa kiuchumi.
My take: Umri si tatizo, tatizo ni mapinduzi ya kifikra na muono wa hitaji la sasa kuwa kinachohitajika ni siasa uchumi, yaani ukombozi wa kiuchumi ili tupate uhuru wa kiuchumi baada ya uhuru wa kisiasa wa 1961. Kumbe basi si kuzaliwa baada ya uhuru bali mapinduzi ya kifikra kadiri ya hitaji la sasa, tutajidanganya tukiangalia umri kama ndiyo muhimu kuliko kuangalia fikra zetu zikoje, bahati mbaya wengi wetu tunachukulia ujana kama ukombozi bila kuangalia ujana wetu tunaufanyia kazi gani. Ukitaka kujua hili, angalia idadi ya mawaziri waliopo sasa waiozaliwa baada ya uhuru ni wangapi wamefanya kitu kwa kigezo hiki cha kuzaliwa baada ya uhuru.
 
Mkuu,
Usishangae sana, Watanzania wengi hasa wale wanaoishi 'bongo' bado wako nyuma sana linapokuja swala la kisiasa. Tatizo kuu, wengi wao ni 'washabiki wanachama' na siyo wanachama hasa ambao pia wanaenzi demokrasia ya kweli. wakati mwingine siyo makosa yao kwa sababu wazee ndani ya CCM walitaka kuwaaminisha wanachama wao kuwa wapinzani ni adui na hizi kauli ndizo wengi ndani ya CCM waliziamini na haya ndiyo matokeo yake.

Huu ugonjwa wa hizo fikra finyu ndiyo pia umetapakaa kwa wanaojiita wanachama wa chama vya upinzani ili kupambana na wanachama na wapenzi wa CCM.

Watu wengi humu janvini hawakubali kutokubaliana badala yake wanabakia kurushiana matusi tu

Sidhani kama itikadi za chama ni kuwa na wanachama wanaokipigia kura ili kuchukua dola, ninachojua ni sera ndizo zinazokipa chama hali ya kukubalika. Wapiga kura ni wote wanachama na wasio wanachama, na mara nyingi wasio wanachama ndio walio wengi zaidi wenye kujaza kapu la kura.

Nakumbuka sera za mataifa makubwa kutoendekeza mambo ya chama, bali chama huwa ni mhimili wa watu kadhaa ambao huonyesha itikadi ambazo wenye kuzifuata huelekea kule wanakovutiwa, na ndicho kinachoendelea nchini sasa hivi.

Huko vijijini wanakoelekeza nguvu kwa wapiga kura ni kutengeneza mashina hata kama ni ya watu watano tu lakini watafikisha jumbe mitaani kwa wenzao.

Wengi wenye tafakazi za upande usioegemea ko kote hupenda kubaki neutral na itikadi zile zenye mvuto kwao huzikubali na kuzieneza kwa wengi. Hii ya kushabikia rangi ya sima au yangu ndio haya tunayokuta kama watu hawana akili vile kuimbia na kumchezea wasivyovijua.
4_%2BJK%2Bakisakata%2Bmuziki%2Bwa%2Bhamasa%2Bya%2BChama%2Bna%2BVijana%2Bwa%2BCCM.jpg
 
Zitto ana haki zote za kutamka maneno hayo kama mawazo yake. Hivyo ndivyo yeye anavyoyaelewa maendeleo ya kiuchumi yatavyoweza kutekelezeka.

Kifupi, Zitto haamini kuwa Changamoto ya kiuchumi katika utandawazi unaweza kutatuliwa Tanzania na kiongozi aliyezidi miaka 50.

Ninamuelewa vizuri kabisa NA ANAWEZA KUWA YUPO SAHIHI, kwa sababu kiongozi anayesimama mbele ya watanzania milioni 35 na kuwaahidi kuwapa elimu bure bila kuonyesha hizo pesa atapata wapi n kitendawili.

Viongozi kama hao wamepitwa na wakati na wanatakiwa wawajibishwe kwa kigezo cha UMRI WAO. SI KOSA LAO, NI KOSA LA UMRI WAO NA KWA HILO HATUWEZI KULIBADILI.

Wachangia karibu wote hapa hakuna anayesema Zitto hana haki ya kutamka, ila tunachojadilia nafasi gani kwa busara kama kiongozi anatakiwa ayatamke na wapi kwa kuyatamka. Kuna mlolongo wa mengi unaoonyesha Zitto kukosa busara ila kufikiria matamko ndio jambo la msingi.
 
ananitia mashaka sana uyu kijana! uwezekano mkubwa akawa fraud leadr!
 
kwa sisi wana falsafa 'KUZALIWA KABLA YA UHURU ' lina maana nyingine kabisa na wala si maana ya umri!
Kauli hiyo haina tofauti na msemo katika biblia:-
“ mambo haya wamefichwa welevu lakini wamefunuliwa WADOGO hawa” usipokuwa na elimu ya filosofia unaweza kusema 'wadogo hawa' ni watoto!
 
Tumeshakshtukia, unakuwa na ushabiki wa kipumbavu kama siyo wa kijinga. Kama Zitto ndio Rais wako, basi usitupotezee muda kuchangia kwenye hii thread. Sisi ndani ya Tiss tuiochoka na CCM ndio tunaomjua Zitto. Wewe haumjui. Kwa hiyo nyamaza. Be careful kwenye vitu unavyopost humu ndani mkuu
Hee imeshakuwa Upumbavu mara?.. Kwa hiyo unataka kunambia Zitto haruhusiwi kugombea Urais Chadema sio? haya nani anayefaa kugombea nipe list yako ya wagombea na isiwe upumbavu ama ujinga..
 
kwa sisi wana falsafa 'KUZALIWA KABLA YA UHURU ' lina maana nyingine kabisa na wala si maana ya umri!
Kauli hiyo haina tofauti na msemo katika biblia:-
" mambo haya wamefichwa welevu lakini wamefunuliwa WADOGO hawa" usipokuwa na elimu ya filosofia unaweza kusema 'wadogo hawa' ni watoto!
Werevu inaweza kuwa wenye umri mkubwa pia ama matured.Maturity comes with age.Kwasababu neno la kwenye sentensi ya kwanza ni "werevu",inawezekana kabisa sentensi ya pili ikawa udogo wa akili,pia inawezekana werevu ikawa ni wenye vyeo na mamlaka na wadogo ikawa ni your ordinary people.Inaweza kutafsiriwa in many ways.Ndo maana hata kwenye madhehebu watu wana tafsiri za tofauti,hence madhehebu hayo,licha ya kwamba kitabu ni kimoja.
 
Status
Not open for further replies.

Similar Discussions

Back
Top Bottom