Zitto: Sitagombea ubunge 2015, Nitagombea Urais kupitia CHADEMA...

Status
Not open for further replies.
Siwezi kupoteza muda wangu kumjadili Zitto ni afadhali hata kumzungumzia Lowasa kuwa Rais linaweza kuwa jambo la maana sana. am tired with the same stupidity every time from the Man who think he is Genius na sisi wengine wote mazezeta.

5+copy.jpg

4+copy.jpg

ndio mkuu hebu check hapa
#AMPLIFAYA Sep27 #2 ZITTO KABWE: nitagombea Urais 2015 sitogombea tena Ubunge, kuna watu wanajiona ni CHADEMA zaidi kuliko mimi lakini hawajui. (Post sponsored by ZANTEL )
 
Jamani anaweza kuwa akimaanisha kuwa sisi vijana tuna jukumu kubwa la kufanya kazi ili uchumi ukue kwani hao wazee umri umeenda
 
Hapa hata mimi sioni tatizo kwani tunachotaka ni kuona uhai zaidi wa chama na maendeleo kwa watanzania kupitia chama!

Kwa hili niko Upande wa Zitto maana hata Mzee Mtei hadi leo angekuwa mwenyekiti ningepiga vita akapumzike. Chama kimeshikwa na vijana tunayaona matunda sasa tunaingia ktk Utaifa...Tunataka watu wapya wenye nguvu, mawazo mapya na fikra mpya maana wazee wetu wameanza kukusanya mali za kurithisha watoto zao.. Na umaskini huu watatumaliza. Je naweza kumpa kura yangu Zitto kuwa rais? hapo tutaanza mjadala mpya!
 
At best as simplistic as saying "vijana bado hawajakomaa kisiasa".

Different ends but the spectrum is the same.

This immature diction, plagued with a panache of plaques immersed in relentless abandon to common decorum and a knavery full of wanton reductivism is unbefitting a gentleman simpleton, let alone an aspiring statesman of supposedly Herculean proportions.
 
Kama haujamuandika "out of context" Zitto anapaswa atuombe radhi tuliozaliwa kabla ya Uhuru, awaombe radhi na wazazi wake ambao bila wao, nna uhakika wote walizaliwa kabla ya Uhuru, asingekuwepo hapo alipo.
Asante zomba!!sasa umeweza kuona aina ya gugu mnalotaka kulipanda shambani mwenu,huyu wala hafai siasa,labda ile kwaya ya mzee komba ingemfaa.
 
Last edited by a moderator:
Ninaamini demokrasia nayo ina taratibu na busara pia mkuu. Kwanini asitangazie kwenye vikao mahsusi vya chama??ama basi hata akasubiri kidogo walau 2015 ijongee karibu ili kama chama kiamue kwa pamoja?...

Hilo neno, kwani kukimbilia vyombo vya habari ndivyo vitakavyo mpa ridhio kupeperusha bendera ya chama au hatua za vikao vya chama? Jambo ukilishupalia sana hatimaye hata ubongo unaanza kukosa nguvu ya kufanya kazi ipasavyo, hatushangai sasa kwa kukazana kuendesha kurusha air plane kuelekea upande unakoelekea upepo badala ya unakotoka upepo.
 
Mkuu,
Siyo lazima uwe kwanza kiongozi wa chama ili upitishwe kuwa mgombea wa nafasi ya urais. Katiba ya CHADEMA inaruhusu mwanachama yeyote kugombea nafasi ya Urais pale atakapopitishwa na vikao maalum vya chama.
Nashukuru kwa uungawana wa kunielewesha hilo.Ngoja nifanye mpango wa kuisoma katiba hiyo ili nione kama ninaweza kuachana na ushabiki na niwe mwanachama.Lakini kama huyo aliyenijibu ndo mwanachama,hao wanaharibu chama.Ndo hao wanaojidahi ni chadema humu lakini hawana uvumilivu na wanawabeza watu wengine hata imani zao na mengine.Mtu akinijibu kwa style ile huwa najuliza mara mbilimbili kuhusu uanachadema wake.Especially given the fact that niliuliza swali ili nieleweshwe.
 
Alichokuwa anajaribu kusema ni kwamba Dr. Slaa asitegemewe katika kuleta mabadiliko za kiuchumi...
 
Zitto ni tatizo ni tatizo, Chadema wawe makini sana.

mkuu kweli kabisa zito ni tatizo tujiulize kwanini JK akitaka kuchukua wapinzani zzk lazima awepo? kwanini zzk hashiriki m4c? kwanini wenzake walipokuwa arumeru yeye aliibua mambo ya uraisi? hapa kunsa kitu naanza kuamini ile habari ya mwanahalisi
 
ndio mkuu hebu check hapa
#AMPLIFAYA Sep27 #2 ZITTO KABWE: nitagombea Urais 2015 sitogombea tena Ubunge, kuna watu wanajiona ni CHADEMA zaidi kuliko mimi lakini hawajui. (Post sponsored by ZANTEL )
Inawauma sana Zitto akiondoka na toto lenu na Mujini eeeh!.. Msijali Zitto bado hana umri wa kugombea lakini haina maana haruhusiwi kusema wazee wang'atuke. Ubaguzi gani wakati umefika kweli wang'atuke? Je wao sio wabaguzi kung'ang'ania nafasi za juu ktk uongozi kwa miaka zaidi ya 50 wakiwaachia vijana makapi!.. Wengine tutakula wapi aaah! Mpaka Mungu awalazimishe kwa vifo jamani..
 
AANZE Kusema serikali ya kikwete na pinda haijafanya kazi na haifai kwa sababu wamezaliwa wakati wa ukoloni, la sivyo itadhiirisha kuwa zito hafai kuwa mbunge, CDM kama wanataka kuongoza lazima nafasi ya uraisi asimame slaa, au tundu lisu, zito kama anaitaka hiyo nafasi ahamie ccm, kijana mdogo anawaza uraisi unataka uraisi wakifalme kama hawa wanaotuongoza?, hapana mtu mwenye uchu kiasi hicho hatuwezi mwachia nyama akachome tutaletewa mifupa
 
Hata JK amewaambia wazee wa CCM wakae pembeni, tehe tehe tehe, CDM lazima muende na kasi mpya!
Zitto for Presideny 2015
 
Kwa hili niko Upande wa Zitto maana hata Mzee Mtei hadi leo angekuwa mwenyekiti ningepiga vita akapumzike. Chama kimeshikwa na vijana tunayaona matunda sasa tunaingia ktk Utaifa...Tunataka watu wapya wenye nguvu, mawazo mapya na fikra mpya maana wazee wetu wameanza kukusanya mali za kurithisha watoto zao.. Na umaskini huu watatumaliza. Je naweza kumpa kura yangu Zitto kuwa rais? hapo tutaanza mjadala mpya!

I am getting to a point I am starting to question this guy Mkandara's educational credibility. Naskia kwamba jamaa anafundisha chuo kikuu. Kwa akili za namana hii nilitegemea awe kiongozi siyo mfuasi. Kwani Mkandara hajui kwamba Zitto ni CCM? Mkandara hajui kwamba kundi la Membe linamtumia Zitto kulichafua CDM?

Tanzania kila ni cha kufoji, sitahangaa huyu mkandara amefoji kitu sehemu. I am very doubtful of his interlectual might and integrity. CCM tunajua kwamba Zitto ni Kibarka. Yeye anachopinga ni nini?

Bw. Mkandara wewe hauoni kwamba hii kauli ni tata? unadhani professa Muhongo au Magufuli wamezaliwa lini? Kwa nini wasiwe kwenye uongozi? Kwamba zitto kasema? You need to evaluate things you post here. Be serious
 
Wakuu

Katika hii post niliandika yafuatayo kuhusu huyu little boy power monger ZZK:


https://www.jamiiforums.com/jukwaa-la-siasa/327494-jinsi-ccm-itakavyomtumia-zitto-kushinda-urais-2015-a.html




Nadhani wote tunajua kuwa CCM inapanga kutumia kila mbinu on earth ili kuendelea kutawala mwaka 2015 kihalali au kwa zuluma. Sasa hivi, Chama Hiki (ambacho kwa sasa ni marehemu) kiko kwenye mikakati mikubwa na madhubuti ya kuhakikisha kitaendelea kutawala hata kama hakitapata kura za kutosha mwaka 2015. Baadhi ya mikakati hiyo ni pamoja na:

Kumteua Lubuva kuwa Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi kwa makubaliano maalumu kuwa atapewa ulaji huo only if atakubali kuitangaza CCM kuwa mshindi wa Urais 2015 hata kama itapata asilimai 10 tu ya Kura (Lubuva Ameshakubali na atafanya hivyo)

Kuruhusu matokeo ya Urais kupelekwa mahakami ili kuja kumnyang'anya Slaa urais kupitia mahakani in case things fall apart and somehow someway CCM looses. So Lubuva Akishindwa kazi Othman Chande atafanya kazi ya kutangaza CCM kuwa mshindi no matter what.(Chande ameshakubali na atafanya hivyo)

Kupanga ugomvi wa CHADEMA na polisi ili watu wauliwe na hivyo kuwatisha watu kuwa CHADEMA ni wagomvi na ikiwezekana kuifuta CHADEMA kupitia kwa Tendwa. (Tendwa amekubali na yuko tayari kufanya hivyo ikibidi)

Na kama haya yote yakishindwa (Yaani Lubuva, Othman na Tendwa) then karata kubwa ya Mwisho ni Zitto Zuberi Kabwe.
Sijui kama yeye anajua hili ila CCM watakuja watamshawishi Zitto Kabwe agombee urais kama mgombea binafsi. Ushawishi huu utafanywa directly na CCM yenyewe na indirectly kwa CCM kuwapa hela rafiki zake Zitto wajerumani ili wajidai wanampsonsor ili agombee Urais kama Mgombea binafsi.

Lengo kuu la CCM katika hili ni kugawanya kura za CHADEMA ili kuishinda. Wanachotaka CCM ni hiki - Zitto akigombea basi Slaa anaweza kupata asilimia 37 za wapiga kura wote Tanzania na Zitto akapata kama asilimia 25 huku CCM ikiambulia kama asilimia 38. Mpaka hapo (Japokuwa CHADEMA itakuwa na asilimia 62) Mgombea wa CCM atakuwa ameshinda (ukichukulia watachakachua kura pia). Hii ni trick ya kudivide kura za CHADEMA na kuwafanya wagombea wote wa CDM wasipate kura za kutosha ilihali angegombea Slaa peke yake angepata asilimia 62. Kama hili litafanikiwa Zitto atakuwa ametumiwa kumnyang'anya Slaa kura huku akiipa CCM ushindi thru this divide and continue to rule trick. Tricky hii huwa inatumiwa sana Marekani na ndio kete ya mwisho ya CCM kuiangusha CDM thru Zitto Zuberi Kabwe.


Naye Zitto Akanijibu hivi

Hii ni hadithi ya kijinga tu isiyo na maana.

Naomba niseme, mimi ni mwanafunzi wa historia. Kamwe siwezi kuifanya historia inihukumu kwa mabaya. Siwezi kuwa sababu ya Taifa letu kushindwa kuandika historia mpya ya kuiondoa madarakani CCM iliyochoka na kutufukarisha. Historia ya maisha yangu imeandikwa kwa harakati za mageuzi na ndio maana sijawahi kuwa mwanachama wa chama chochote zaidi ya CHADEMA. Wakati vijana wasomi wengine walikwenda kutafuta mkate makazini au kwenye vyama vingine vya siasa vilivyokuwa vinang'ara wakati huo, mimi nilijiunga CHADEMA na kushiriki kukijenga mpaka hapa mnapokiona. Siwezi kufuta matumaini ya mabadiliko ya Watanzania.

Napenda ifahamike kuwa CHADEMA haina mgombea Urais wa mwaka 2015. Muda utakapofika taratibu za chama kupata mgombea zitatangazwa na tunaotaka kugombea tutajitokeza au tutaombwa na vikao vya chama.

Yeyote atakayeteuliwa na chama kupeperusha bendera ya chama chetu ndiye atakuwa mgombea wa chama chetu. Mimi binafsi nitamwunga mkono mgombea yeyote atakayepitishwa na chama. Kama CCM wanakuwa kama fisi kusubiri mkono udondoke wasahau. CHADEMA hatutogombana kwa sababu ya Urais. Kwangu mimi Urais sio an End. It is just a means to an end. Malengo haya haya niliyonayo yanaweza kutekelezwa na Rais Mbowe, Rais Mkuumbo, Rais Slaa au hata Rais Lissu. Uwezo na maarifa yangu siku zote nimeyaweka katika kuhakikisha Taifa letu linakuwa bora zaidi kiuchumi, kijamii na kisiasa. Urais ni dhamana tu ya kufikia malengo hayo.

Mada kama hizi badala ya kujenga chama zinabomoa kwa kupandikiza mbegu za chuki miongoni mwa viongozi. Mwandishi wa makala haya angetumia akili zake hizi kuandika mradi wa maendeleo ya kijiji ingesaidia sana badala ya kumwaga chuki na kuleta mfarakano.

Yeyote anayedhani kwamba ataivuruga CHADEMA kupitia kwa Zitto aandike maumivu. CHADEMA ni movement. Zitto ni sehemu ndogo sana ya CHADEMA kama ilivyo kwa mwanachma mwingine yeyote. Wengi tulioanza nao hatunao, na wengi tulionao sasa hatukuwa nao.
 
Naomba ninukuu maneni ya Ernesto Sheka kwenye maandiko yake ya The Moment Of Truth:

Can CDM give that a chance to someone from nowhere?

kama kweli zito kabwe anautaka uraisi basi ahamie ccm kwa sababu huko ndo kwenye viongozi wanaomiliki mitandao ya kuusaka uraisi na pia ndicho chama kilichojihakikishia kutawala milele. Kama ccm itatawala milele na yeye anautaka uraisi basi huku cdm anapoteza muda wake bure!!!!!
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom