Zitto: Sitagombea ubunge 2015, Nitagombea Urais kupitia CHADEMA...

Status
Not open for further replies.
mkuu chama chetu kinaongozwa na katiba ya chama, so hakuna kipengele chochote ambacho Zitto amevunja, pia inabidi tufike mahali tusiwe sensitive sana ktk kila neno koz tutajikuta tunapoteza lengo la kupigana na adui (CCM).

Plz lets buld our CDM.

Well said!
Bora wanaCDM wote wangekua na mawazo ya aina hii tungekua hatupotezi muda kubishana hapa bali tungekijenga chama huku tukisubiri muda useme!
Once again, thank you Shardcole.
 
Na vipi aliyezaliwa tarehe nane mwezi wa kumi na mbili mwaka elfu moja mia tisa sitini na moja, 8/12/1961?
Umemsoma vizuri Zitto kasema nini? Wazee wetu walituletea Uhuru ina maana wale waliopigania Uhuru wetu wakapumzike na waache waliofuata waijenge nchi kiuchumi maana kazi yao ilikwisha kamilika.. No offense hata kidogo kina Wasira wanalala tu bungeni, isipokuwa huwa namkatalia Zitto pale anaposema Vijana kina Makamba na yeye ndio wanatakiwa kuongoza nchi akiwaona hata kina Jasusi ni wazee hawawezi wakati ukiwatazama vijana hawa hawajaweza kujenga Hekima wala Busara, bado wahuni tu. ahaha Ahaha!
 
hebu mpeni haki yake mh Zitto naye ajaribu....mh Mbowe alijaribu akashindwa.......dr Slaa naye vilevile.....tunahitaji sura mpya.....tena itaondoa dhana ya udini ndani ya cdm.....siyo kila siku walewale....tuko watanzania zaidi ya milioni 40...hakuna chuo kinachotoa elimu ya urais
Sitaki kusikia ETI mtu fulani agombee urais ili tuone SURA MPYA.kuna mambo yanahitaji umakini mkubwa kuyajadili.
 
Si alisema hatagombea uongozi chadema?Ama urais chadema unagombewa bila kuwa kiongozi?

Hivi wewe unaijua vizuri katiba ya CDM? Hebu kasome vizuri katiba ya CDM ndio uje kuandika up.u.pu wako.
 
as if Zitto is not entitled to own make statements. I don't think that everytime Zitto makes a statement then we should correllate to Chadema operations. We should also understand this person is a Tanzanian too, he has equally all rights as any other Tanzania citizen....Give him a break neh!

Elimu ya uraia muhimu!
 
freedom of expression mkuu. kwani kavunja sheria kusema hvyo?

Masuala ya uongozi si shauri ya kugusa sheria tu au uhuru wa kuongea, kuna mambo ambayo tunaangalia ni kutumia kwanza kitu kinaitwa common sense kabla ya kutoa kauli. Tamko la Zitto si la mtu aliyefikiria kwanza adhari yake binafsi, chama na watanzania, zaidi ya hiyo uzito kutoweka kwenye maana ya mshikamano katika chama na uongozi.

Ubaguzi wa waziwazi aliouonyesha kwamba ni vijana tu ndio wanaotakiwa kuongoza nchi wakati falsafa ya uongozi mzuri ni kuchanganya mapya na ya kale ndio kujenga uonozi bora. Afanyacho zito ni sawa na kudharau na kudhalilisha wazazi ambao wametukuza na kuturithisha mengi tunayojivunia na tunafurahia hekima na busara yao kwa uzoefu wao wa maisha. Hizi papara za Zitto kung'ang'ania urais ni walakini na kitu cha kujiuliza hatima yake akishika nchi mambo yatakuwaje. Badala ya kutuliza kichwa na kusubiri kuwadia kwa muda wake ndipo aone kama chama na wananchi wanamkubali au la.

Nimeliona hili muda mrefu na kunzisha mada kadhaa kulijadili kuonyesha udhaifu ambao Zitto anaonyesha kama mambo kadhaa ikiwepo uongozi ndani ya Chadema. Uongozi si uwakilishi kama tunavyoona Kikwete anavyofanya kuongoza nchi ni kuwakilisha nchi katika kuzunguka kwenye matukio duniani wakati tunao wawakilishi mabalozi na kama kuna jambo zito waziri wa mambo ya ndani anaweza kufanya, lakini leo Kikwete anafanya shughuli za waziri wa mambo ya nje badala ya urais.

Zitto ni jeuri na mjanja, anatumia kila njia kupenya kwa ajili ya nafasi ya Urasi lakini haangalii kwamba wananchi ndio wenye kujua nani anafaa kuwa rais.

Sikutegemea kama anaendeleza ndoto hizo wakati hata mwenyekiti Mbowe alishawahi kusema kwa sasa hawafugi kundi la wenye uchu wa madaraka bali kundi la waendesha vuguvugu la mabadiliko, kauli hiyo ya Mbowe ilimaanisha jambo fulani ambalo baadhi ya viongozi ndani ya Chadema wanahangaikia uongozi badala ya kuhangaikia kukipenyesha chama huko vijijini kuivunja ngome ya CCM.

Zitto badala ya kuhaha kama wenzeke kuelimisha Umma vijijini yeye yupo kujiweka kwenye vyombo vya habari kujinadisha kuhusu Urais badala ya kufanya kazi ya kukijenga chama.

Tuwe makini, kuna mkuu fulani serikalini na pia ndiye mkuu wa CCM ndiye anayempa kichwa hivyo ili kuleta mtafaruku na migongano ndani ya Chadema, shikeni neno langu hili, ukweli utakuja kujulikana, huyu jamaa ana mambo ya chini chini katika kueneza sumu. Oneni chama chake kinavyozidi kusambaratika na sasa kundi lake amelipenyesha kushika hatamu na wale aliowaambia ndani ya siku 90 wawe wamejiondoa chamani la sivyo fagio litawakubwa, nini kinaendelea sasa kama si kuwakumbatia na kuwatupa nje wapigania haki?

Jamani, kama tunajicho la kuona mbali, Zitto ni tatizo ni tatizo, Chadema wawe makini sana.
 
Mi naona hii sio inshu kuuubwa, japo Mkandara ameonekana kukomaa nayo sana,yuko upande wa Zuberi
 
Kauli yake ni nyepesi saana, why this much attention!? binafsi sioni cha kuumiza kichwa hapo. tumekuwa wa kutishwa na kuchanganywa na vimaneno vilivyotolewa na mtu mmoja, just as an individual kwenye kipindi kinachoendeshwa na mtu "FLANI",!!? come on, Zitto has that right. mnaanza ya ccm kuiga fikra za mwenyekiti!? tunakosea sana kwa kufikiri kuwa kila tuliyenaye ni lazma awe na mtazamo FLAN na kinyume na hapo si mwenzetu. Think twice, think big, ,People's power!!!
 
Tatizo sio kuutaka urais anamipango gani ya kuyabadilisha maisha ya Mtanzania masikini, kupambana na rushwa, mikataba mibovu na viongozi wasio na uzalendo kwa Taifa letu watachukuliwa hatua gani.

Hakuna kitu kizuri kama rushwa as a matter of fact. Rushwa is the time saving instrument. Kuna huduma ambayo ungepoteza wiki nzima na gharama kibao kuipata ukitoa hongo unaipata within a half an hour na kusepa zako. Ubaya uko wapi?
 
Hivi wewe unaijua vizuri katiba ya CDM? Hebu kasome vizuri katiba ya CDM ndio uje kuandika up.u.pu wako.
Sifahamu katiba ya CDM,na ulitakiwa unieleweshe kwasababu niliuliza swali,chungu mdomo wako.
 
Siwezi kupoteza muda wangu kumjadili Zitto ni afadhali hata kumzungumzia Lowasa kuwa Rais linaweza kuwa jambo la maana sana. am tired with the same stupidity every time from the Man who think he is Genius na sisi wengine wote mazezeta.

5+copy.jpg

4+copy.jpg

Mkuu matola Leo UMENIKOSHA KWA BUSARA ZAKO.
 
Mi naona hii sio inshu kuuubwa, japo Mkandara ameonekana kukomaa nayo sana,yuko upande wa Zuberi
Kwa hili niko Upande wa Zitto maana hata Mzee Mtei hadi leo angekuwa mwenyekiti ningepiga vita akapumzike. Chama kimeshikwa na vijana tunayaona matunda sasa tunaingia ktk Utaifa...Tunataka watu wapya wenye nguvu, mawazo mapya na fikra mpya maana wazee wetu wameanza kukusanya mali za kurithisha watoto zao.. Na umaskini huu watatumaliza. Je naweza kumpa kura yangu Zitto kuwa rais? hapo tutaanza mjadala mpya!
 
MBONA watu wanapandisha presha haraka sana? Mwacheni Zitto ajitangaze hata kugombea U-PAPA wa Vatican.

Kama katiba inamruhusu basi mwacheni aende. Ila wapiga kura tunajua nani anakihangaikia chama kila siku.

Watu mikoani na hasa kwenye M4C wanawaona ni akina nani wanapigwa Mabomu wakati wengine wameenda Majuu kutalii na kula maraha na viongozi wa CCM.

Hapa kuna ka ukweli kwa mbaali. Msiwe na wasiwasi kwa hili......

From: https://www.jamiiforums.com/jukwaa-la-siasa/298724-kura-ya-maoni-zitto-vs-dr-slaa.html


Ni nani ungependa agombee urais mwaka 2015 kwa tiketi ya CHADEMA?

Vot979.
This poll will close on 25th October 2012 at 09:52

Zitto Z. Kabwe (kura)151 15.42%

Wilbrod P. Slaa (kura)828 84.58%


Mkuu,
Sikujua pia kama Wilbrod P. Slaa amejitangaza kuwa atagombea Urais na watu wameanza kuchukua maoni kwa kupiga kura.
 
Mwisho wa yote, chama kitaamua!

Ndio siasa za Tanzania katika vyama vyote, mtu anaweza kuhangaika na kutoa povu jingi, tumeona yaliyojilia Dodoma sekunde tu imezima ndoto za watu wazimawazima si wazee wala vijana.

Mara kadhaa tulishamtahadhalisha kujifunza kwa akina Walid Kaburu na wengineo waliopaparika na kuishia kuwa ndoto za kufikirika.

Wakati wenzake wanaendesha vita vya msituni kumtoa nduli anayeharibu nchi, padala ya kuelekeza nguvu huko yeye anakazana na ndoto ya kufikirika kushika dola, dola itashikwa bila kumtoa adui tunayepigana naye?

Zitto alitakiwa ajitahidi kuwa na mshikamano, ushirikiano mzuri na viongozi wenzake na kugawana majukumu katika shughuli za kawaida katika utendaji wa kukiimarisha chama, na wakati mwafaka angeweza kupenyesha hoja yake anapohitajika mtu kutangaza nia ya kugombea muda ukiwadia ndipo maoni ya wananchi na uongozi wa chama ungeona kama anafaa au mwingne apeperushe bendera hiyo.

Kauli yangu:
Kuwa kijana si ticket ya kujihalalishia kuwa unafaa kuongoza nchi, uwezo wa mtu awe mzee au kijana ndio unaomwezasha kuaminiwa na wananchi kuongoza nchi.
 
Hahahaa Mkandara,

Angalia bana, usijeshangaa kuwa huyu ndiyo Firstlady wa Tanzania mwaka 2016.......

WEMA2.jpg

........... isipokuwa huwa namkatalia Zitto pale anaposema Vijana kina Makamba na yeye ndio wanatakiwa kuongoza nchi akiwaona hata kina Jasusi ni wazee hawawezi wakati ukiwatazama vijana hawa hawajaweza kujenga Hekima wala Busara, bado wahuni tu. ahaha Ahaha!
 
wakati watu wako arumeru akaja na kauli ya kugombea leo hii m4c imeshika kasi anakuja na kauli hii hii ambayo mbowe kama mwenyekiti ali tolea ufafanuzi. watu wako kwenye m4c yeye anatoa mikauli ya kutatanisha. naanza kuhisi zitto anatumiwa na ndio maana mkulu anambeba kwenye safari zake ili ajioshe utawala wake unawajali wapinzani. Zito inabidi ujirekabishe kwanini hujiulizi kila siku watu wanakusema wewe tu na ccm jf ndio wanakusupport wewe tu kuwa makini
 
Nimemuelewa kuwa kundi la wachapa kazi ambao wanaweza kuleta maendeleo ya kiuchumi kwa nchi yetu ni wale waliozaliwa baada ya uhuru (vijana) , wazee walipambana na kufanikiwa kisiasa, sasa ni zamu yetu vijana, na kuhusu kugombea uraisi ni haki yake kikatiba, kama chama chake kikimpitisha wananchi wataamua
 
Si alisema hatagombea uongozi chadema?Ama urais chadema unagombewa bila kuwa kiongozi?

Mkuu,
Siyo lazima uwe kwanza kiongozi wa chama ili upitishwe kuwa mgombea wa nafasi ya urais. Katiba ya CHADEMA inaruhusu mwanachama yeyote kugombea nafasi ya Urais pale atakapopitishwa na vikao maalum vya chama.
 
Status
Not open for further replies.
12 Reactions
Reply
Back
Top Bottom