MAGAMBA MATATU
JF-Expert Member
- Jul 2, 2011
- 646
- 1,174
HATMA ya Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe (CHADEMA) aliyelituhumu Baraza la Mawaziri kushawishiwa kubadili msimamo wa kubariki azimio la kuongeza muda wa uhai kwa Shirika Hodhi la Mali za Mashirika ya Umma (CHC) kwa miaka mitatu kinyume cha mapendekezo ya Bunge itajulikana leo.
Hatua hiyo inatokana na Spika wa Bunge, Anne Makinda, kumwagiza Zitto kuwasilisha utetezi wake hadi kufikia leo baada ya agizo lake la mara ya kwanza alilolitoa Juni 23 kumtaka mbunge huyo kuwasilisha utetezi huo hadi kufikia Juni 29 kugonga mwamba.
Hata hivyo, ulishindwa kutolewa uamuzi siku hiyo (Juni 29) baada ya siku ya kwanza ambayo Zitto alitakiwa kuthibitisha kauli yake kuwasilisha barua kwa Spika akiomba amsaidie kupata nyaraka kutoka Baraza la Mawaziri na Wizara ya Fedha zinazohusu mjadala wa CHC ambazo zitamsaidia katika utetezi wake, jambo ambalo Spika alisema alishindwa kumsaidia kwa kile alichoeleza kuwa nyaraka za Baraza la Mawaziri ni siri.
Baada ya tamko hilo la Spika bungeni kumtaka Zitto kuwasilisha utetezi wake, mbunge huyo alimzunguka na kuamua kuwasilisha utetezi wake na vielelezo Alasiri ya siku hiyo (Juni 29).
JE ATANUSURIKA NA HUO USHAHIDI WAKE LEO BUNGENI ATAKAPOKUWA ANAUSOMA MBELE YA BUNGE?