Zitto na ushahidi wake Bungeni (Mawaziri kushawishiwa kutoa maamuzi)

Labda kutakua na tatizo kwa mama hebu review cv yake mtaona kua makinda hakustahili na by tha way hawezi tena hapana spika hapo
 
Amwite kwa lipi coz utetezi kwasilisha tangu june 29,akiamua kumuita inamaana ausome mbele ya bunge na hii ni kuiaibisha serikali pamoja na baraza la mwawaziri.hakuna jipya ataukalia utetezi kama kawa.
 
hakuna kitu alitakiwa kuthibitisha punde baada ya maswali
 
mambo ni yale yale tulitegemea SPIKA angemuhitaji ZITTO kuthibitisha kauli yake lakini naona muda wa maswali umepita na ZITTO hajaitwa kuthibitisha,
hamna spika pale bali kuna mzigo mzito kwa watanzania na mtu mzuri kwa mafisadi so msitegemee miujiza....... prepare yourself for the worst from her
 
HATMA ya Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe (CHADEMA) aliyelituhumu Baraza la Mawaziri kushawishiwa kubadili msimamo wa kubariki azimio la kuongeza muda wa uhai kwa Shirika Hodhi la Mali za Mashirika ya Umma (CHC) kwa miaka mitatu kinyume cha mapendekezo ya Bunge itajulikana leo.


Hatua hiyo inatokana na Spika wa Bunge, Anne Makinda, kumwagiza Zitto kuwasilisha utetezi wake hadi kufikia leo baada ya agizo lake la mara ya kwanza alilolitoa Juni 23 kumtaka mbunge huyo kuwasilisha utetezi huo hadi kufikia Juni 29 kugonga mwamba.


Hata hivyo, ulishindwa kutolewa uamuzi siku hiyo (Juni 29) baada ya siku ya kwanza ambayo Zitto alitakiwa kuthibitisha kauli yake kuwasilisha barua kwa Spika akiomba amsaidie kupata nyaraka kutoka Baraza la Mawaziri na Wizara ya Fedha zinazohusu mjadala wa CHC ambazo zitamsaidia katika utetezi wake, jambo ambalo Spika alisema alishindwa kumsaidia kwa kile alichoeleza kuwa nyaraka za Baraza la Mawaziri ni siri.
Baada ya tamko hilo la Spika bungeni kumtaka Zitto kuwasilisha utetezi wake, mbunge huyo alimzunguka na kuamua kuwasilisha utetezi wake na vielelezo Alasiri ya siku hiyo (Juni 29).
JE ATANUSURIKA NA HUO USHAHIDI WAKE LEO BUNGENI ATAKAPOKUWA ANAUSOMA MBELE YA BUNGE?
hakuna kitu akimbana zito basi alete na ushahidi wa lema vs pinda na msigwa vs pinda la sivyo patachimbika...
 
Spika ni msanii leo tena utaona atajitia kumpa onyo! Na hivi juzi kaongea mama ya Zitto bungeni
 
Inasemekana kuna ka sheria kanakokataza kuwa na 'siri' za serikali. Vpi kama kweli kapo kakitumiwa kumnanihii Zitto?! iwapo tu ni kweli kaanika nini Baraza la Mawaziri liliazimia!
 
Hakuna jipya na sina uhakika kama utasomwa bungeni huo ushahidi, labda spika anaweza kuwafurahisha wapinzani leo kitu ambacho ni kigumu ikizingatia ni spika wa kuambiwa na kuelekekezwa afanye hili au afanye lile!!!
 
Back
Top Bottom